Mwalimu ndelichako, kutana na walimu wenyewe, sio maafisa wao

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako amesema vyeti vya elimu vya Tanzania vitakosa heshima kimataifa endapo suala la udanganyifu wa mitihani litaendelea, huku akieleza kuwa mmomonyoko wa maadili katika jamii umechangia kukithiri kwa udanganyifu huo.

Aidha, amependekeza Serikali kuibadili sheria iliyounda baraza hilo ili liwe na ‘meno’ ya kuchukua hatua kwa wadanganyifu wa mitihani kwa kutumia sheria zake bila kusubiri vyombo vingine kuwashughulikia.

Dk. Ndalichako aliyasema hayo mwishoni mwa wiki ofisini kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam, katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya kutangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne ambayo yameonesha kuwa watahiniwa 3,303 wamefanya udanganyifu na kufutiwa matokeo yao.

“Watu wengi hawaangalii mbali, wanaangalia hapa karibu, lakini kwangu mimi athari za siku za usoni za udanganyifu wa mitihani ni vyeti vya Tanzania kukosa heshima kimataifa kwa sababu vinaweza kuwa na grade (daraja) zuri, lakini mhusika akashindwa kuonesha umahiri wake anapopewa kazi.


Mimi ningemshauri Katibu akutane na waalimu wenyewe, na sio maafisa wao. hapo ataweza kupata taarifa sahihi.

“Itafika mahali Watanzania wote watawekwa katika kundi moja la wababaishaji na hili halitakuwa jambo zuri kwetu. Hivi sasa Tanzania inaheshimika na kuaminika kimataifa. Mimi nimevutiwa na kazi nzuri aliyofanya Dk. Migiro (Asha-Rose, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa) kwa sababu ya sifa zake,” alisema Dk. Ndalichako akizungumzia athari za udanganyifu katika mitihani.

“Hatari ninayoiona ni kwamba Watanzania wote tutawekwa katika kikapu kimoja, watu hawaangalii athari zake za muda mrefu, wanatazama hapa (karibu), lakini madhara ya muda mrefu ni makubwa sana.”

Alisema suala hilo la udanganyifu linawatia hofu Baraza kwa sababu wanajiuliza kama vyeti wanavyotoa ni halali kwa baadhi ya wahitimu kutokana na jinsi udanganyifu unavyoonekana kukithiri nchini.

Katibu Mtendaji huyo wa Necta alisema suala la udanganyifu kwa kiasi kikubwa linachangiwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii, kiasi kwamba wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe wanashirikiana katika biashara ya kununua mitihani kwa baadhi ya wazazi kukubali kuchangishwa kugharimia uovu huo.

Wafanyabiashara wa mitihani

“Mmomonyoko wa maadili ni chanzo kikuu cha udanganyifu wa mitihani, wapo wazazi wanaoshirikiana na walimu katika baadhi ya shule kuchangishwa ili kuwezesha kupatikana kwa mitihani. Hivi mzazi unawezaje kuchangia ili mwanao atafutiwe mitihani huoni unashiriki katika vitendo vya udanganyifu?” alihoji.

Akitoa mfano, alisema katika mitihani ya mwaka jana, walipewa taarifa na wasamaria wema kuhusu baadhi ya shule wilayani Geita mkoani Mwanza kuchangisha wazazi ili kushiriki katika udanganyifu huo na Necta kwa kushirikiana na maofisa elimu wa Wilaya na Mkoa walizuia mpango huo katika shule saba za wilaya hiyo.

Alisema maandalizi kama hayo yalifanyika pia katika shule tatu za Mkoa wa Kilimanjaro, lakini huko pia baraza lilichukua hatua za haraka na kuzuia udanganyifu huo.

Adhabu za papo hapo

Dk. Ndalichako alipendekeza kubadilishwa kwa sheria iliyounda baraza hilo ili wadanganyifu wa mitihani wachukuliwe hatua za haraka badala ya kusubiri kupelekwa mahakamani ambako kesi zinachukua muda mrefu.

“Inabidi sheria yetu iimarishwe sasa na kutoa adhabu yenyewe badala ya kusubiri watu kupelekwa mahakamani ambako kesi huchukua muda mrefu. Kwa mfano, wenzetu wa Rwanda, Malawi na Ghana sheria zao zinaruhusu wahusika kukamatwa papo hapo na kuhukumiwa.

“Kwa mfano, kule Masama, Sirari (Tarime) kuna mwalimu alikamatwa ‘live’ na askari akiwa na karatasi za majibu anayafanya kwa ajili ya kumpa mwanafunzi…sasa pale ushahidi upo tayari, unampeleka mahakamani ambako kesi hadi leo inasikilizwa. Unataka ushahidi gani tena hapa?” alihoji Dk. Ndalichako.

Alisema tayari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeunda Tume maalumu ya kutathimini tatizo hilo la udanganyifu na anatarajia kuwa licha ya kuchukua hatua kali kwa wahusika wakiwemo wasimamizi wa mitihani na maofisa wengine, suala la sheria iliyounda Necta, litaangaliwa ili kuwapa nguvu zaidi.

*Walioandika matusi kukiona

Aidha, alisema kuanzia wiki hii, anatarajia kukutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili kupata ushauri wake juu ya wote waliohusika na wadanganyifu katika mtihani huo wa Kidato cha Nne mwaka jana, wakiwamo wanafunzi walioamua kuandika matusi kwenye karatasi za majibu.

*Utata taarifa za maendeleo

Dk. Ndalichako pia alieleza masikitiko yake juu ya kutokuwepo kwa uhalisia wa taarifa za maendeleo za kila mwaka za mwanafunzi na mitihani yao ya mwisho, jambo aliloeleza kwamba linawagombanisha wao (Necta) na wazazi kutokana na wanachokipata wanafunzi katika mitihani hiyo ya mwisho.

“Hili ni eneo ambalo mwaka huu nitalifanyia kazi sana. Kwa kweli hakuna uwiano wa alama za maendeleo ya masomo ya mwanafunzi na matokeo ya mwisho. Tunajiuliza hivi alama za shule kazipataje? Na kwa muda mrefu sasa hili linatugombanisha sana na wazazi.

“Unakuta alichokiandika mwisho mwanafunzi hakiwiani na alichokuwa akifanya katika masomo yake. Nahisi mitihani yao inaweza kuwa na matatizo, hivyo nataka nizungumze na walimu kuona tatizo liko wapi,” alieleza Dk. Ndalichako ambaye kitaaluma ni mwalimu na amekuwa Necta tangu mwaka 2005.

SOURCE: HABARI LEO, 13/2/2012
 
Kwa maoni yangu ni bora ukutane na walimu wenyewe, ukikutana na maafisa elimu na viongozi wengine wala hawatakupa taarifa sahihi mama.
 
Back
Top Bottom