Mwalimu na mwanafunzi wabambwa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu na mwanafunzi wabambwa!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Wa mmoja, Aug 25, 2010.

 1. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanafunzi asimamishwa masomo, lakini mwalimu wake aachwa akipeta

  Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ya wasichana Maswa Chacha Mussa (28) amekutwa na mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka (16), wakijiandaa kufanya mapenzi.

  Tukio hilo lilitokea Agosti 7, mwaka huu saa 7:45 mchana baada ya uongozi wa shule hiyo kupata taarifa kwamba mwalimu Chacha alikuwa nyumbani kwake na mwanafunzi.
  Baada ya taarifa hizo, Mkuu wa Shule Msaidizi, Paschal Athanas na mwalimu wa zamu waliamua kwenda nyumbani kwa mwalimu na kumbamba akiwa chumbani kwake na mwanafunzi huyo.

  Aidha, kutokana na tukio hilo mwanafunzi huyo amesimamishwa masomo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuruhusu uchunguzi kufanyika.
  Hata hivyo, mwalimu wake bado anaendelea na kazi ya kufundisha kama kawaida na hakuna hatua yoyote ya kisheria ikiyochukuliwa dhidi yake.

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishina Msaidizi Daudi Siasi alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea polisi walipewa taarifa na kwenda kwenye shule hiyo ambapo mwanafunzi huyo alipelekwa kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Maswa na kuonekana kuwa alikuwa hajafanyiwa kitendo chochote na mwalimu huyo.

  Huu ni uchu au kitu gani?! Na kwa nini mwalimu asichukuliwe hatua yoyote au ndio sheria inavyosema?!
   
 2. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona siku hizi walimu wengi wana uchu sana? watoto wa shule nao wanayaweza.
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kwa umri huo alitakiwa awe shule huyo, maana naona kama wote ni watoto
   
 4. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuporomoka kwa maadili ni janga kwa jamii nzima, ni profession gani wanaoweza kusema ni salama? Waalimu kwa kuwa ni wengi kuliko wafanyakazi wengine na wanafanya kazi karibu sana na jamii ndo maana wanaonekana zaidi kuliko fani nyingine. mambo yanayofanyika maofisini ni ya aibu hata kuzungunza hapa, AIBU TUPU.

  Yote kwa yote uadilifu umepungua sana kwenye hii taaluma ya ualimu ikichangiwa na mambo mengi:-
  (1) Uelewa mdogo wa waalimu wenyewe na wakufunzi wao, hivyo kujikuta mwalimu hajaiva kisaikolojia kabla ya kuvikwa jukumi hili kubwa la kulea Taifa.
  (2) Kuchanganyikiwa kwa waalimu kutokana na hali ngumu ya maisha, hivyo wanatafuta namna ya kujiliwaza. Maskini wengi raha yao ni ng****, wakati wenye fwedha zao wana njia nyingi za refreshment.
  (3) Wanafunzi kukengeushwa na wazazi wao, hivyo kuwatia waalimu majaribuni. Nimefundisha kidogo na kuona jinsi baadhi ya mabinti walivyo na mbinu nyingi za kuwanasa waalimu wao, mara nyingine wanatumwa na wazazi wao.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kutokana na hii stori sioni kama kuna kosa lolote hapa, huyu kamanda wa polisi alikuwa na kiu ya kuandikwa gazetini na alikuwa na hamu ya kuongea na waandishi.
   
 6. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kwanini mwanafunzi arudishwe nyumbani na mwalimu aachwe?!
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nadhani proffessionally sio vizuri kwa mwalimu kumfundisha mpenzi wake ( labda ndo sababu) wanataka akatafute shule sehemu nyingine lakini kisheria hakuna jinai hapo
   
 8. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  wanafunzi wanapenda sana kumegwa na walimu...! enzi zetu shuleni mbona ilikuwa kawaida ..! walimu kibao wameoa wanafunzi wao.....hata vyuo vikuu..!

  waacheni wamegwe...!
   
 9. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Walimu wa voda fasta hawa watatuharibia watoto. Hawakupata muda wa kufundishwa maadili ya kazi ya ualimu.
   
 10. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tehe tehe koh!!!siyo mbaya maana kama mwalimu lazima amfundishe mwanafunzi nyanja zote na kuna practical nyingine hazifanywi darasani.
   
 11. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Jamani acheni kabisa, mimi nimefundisha sana hizi shule za sekondari, unakuta kibinti kinakaa nyumaaaaa! harafu muda wote ni kulembua macho. Ukionekana kushabikia hayo macho kanaweza kukufunulia hata chuchu zake kidogo ili kukuchanganya zaidi.
  Hata kama umesoma maadili ya kazi miaka saba, kuna siku utaingizwa mkenge tena kwa kulazimishwaaaa jamani yamemkuta rafiki yangu. Ngoja niishie hapo kwanza.
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  I doubt!
   
 13. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Midhali hilo tendo halikutendeka na daktari amethibitisha, kulikuwa hakuna haja ya kukuza hii stori magazetini. Huyu bwana Mussa Chacha anekuwa anajuwa haki zake angeweza kufungua kesi ya kuvunjiwa heshima na wahusika (gazeti husika na vyombo vya dola).
   
 14. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inategemea waliwakuta kwenye hali gani. Hata hivyo kama hakuwa amefanya tendo lolote llile huna namna ya kumshitaki. Unataka ashitakiwe kwa kosa gani? La kumuingiza mwanafunzi chumbani kwake? Je tuition haiwezi kufanyiwa chumbani kwake? Kimsingi hakuna shitaka ambalo Jamhuri inaweza kumfungulia ila uongozi wa shule unaweza ukamwadhibu kwa kumpeleka mwanafunzi wake chumbani kwake. Hao waliokwenda kumfuatilia walifanya kosa wangetakiwa wasubiri mpaka aanze shughuli au pengine walitaka kumnusuru huyo binti kutoka mikononi mwa Fataki. Msiseme huu ni uchu kwani umri wa huyo kijana bado ni umri wa kurukaruka hovyo.:becky:
   
 15. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakijiandaaaa!!!!mmmh tata hii mkuu
  mix with yours
   
 16. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUMBE KUNA KUONEKANA KUSHABIKIA PIA.....kumbe kuna choice sio kwamba unakuwa umekuwa constrained moja kwa moja eeeeh...
  hao ni wanafunzii hbu tupe na ya walimu pia wai hufanya nini ......kitu gani ambazo wanafunzi nao wakionekana kushabikia.....
  mwanamke jicho babu!!!! acheni kushabikia
  mix with yours
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  28 mtoto? kweli JK bado kijana:eyeroll2:
   
 18. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mfanyia hekaluni hula hekaluni!
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnh,
  sie wazazi tunaosomesha watoto wa kike kazi tunayo.
  Mpaka siku unaozesha ndio .....pheeeeewwww!.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mod bana..

  Sasa kama walimu wenyewe mnawalipa ndururu za kichuuzi mnadhania 'hasira' zao watazimalizia wapi? Principle ya anarchy ni kila mtu kumtafuta mnyonge wake!
   
Loading...