Mwalimu mstaafu apata kichaa baada ya kudhulumiwa milioni 20

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
TAKUKURU mkoa wa Katavi imefanikiwa kumrejeshea kiasi cha shilingi milioni 20, Mwalimu mstaafu George Kanyukamalunde, ambaye ameugua ugonjwa wa kuchanganyikiwa mara baada ya kudhulumiwa pesa zake na mtu ambaye alimkopa kiasi cha shilingi milioni 10 baada ya mafao yake kuchelewa.

MWAL%20TAKU.jpg

Kushoto ni mwalimu mstaafu George Kanyukamalunde, akikabidhiwa pesa zake na TAKUKURU
Wakizungumza mara baada ya pesa hizo kukabidhiwa mtoto wa Mwalimu huyo anayeitwa Genuine Kanyukamalunde, pamoja na mke wa mwalimu huyo wamesema kuwa fedha hizo zitamwezesha kuendelea kupata matibabu mara baada ya kupata matatizo hayo.

Kwa upande wake mwalimu huyo mstaafu alipopewa nafasi ya kuishukuru TAKUKURU kwa kumrejeshea pesa zake lakini kutokana na hali yake ya kiafya, alishindwa kuzungumza chochote na badala yake aliangua kilio kwa uchungu.

Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Christopher Nakua, amesema mkopeshaji huyo alichukua kiasi cha shilingi milioni 25 kutoka kwa mwalimu huyo na alifanikiwa kuzichukua kwa sababu kadi ya benki na namba ya siri alikuwa nayo.

EATV
 
Hata sehem za migodini kama geita nyamongo 'buzwagi kuna watu wanaishi kwa huo mchezo anakukopesha kaki unarudisha laki na 30000 na card anapatiwa
Hivi unalazimishwa kuchukua huo mkopo wa dhuluma, hayo ni masharti ya mkopeshaji. Kama huwezi unaacha, sasa mtu kaweka masharti yake na hajakuita uende kwake.. then mnataka apangiwe masharti. Ingawa pia riba kama hizo ni kinyume na sheria
 
Tz nzima..ila huwa mnakopaga za nn sasa? Maana mnalalamika na huku ww mwenyewe umekuja kukopa...lol
Wewe mjinga kabisa, hujui watu uko vijijini wanapata tabu sana, inawezekana mwl alipata tatizo kubwa sana, hata angekuwa wewe, mtoto anaumwa au ndugu yako huna pesa unaweka chochote hili mtoto wako apone,au ndugu yako, hivyo wakopeshaji wanachukuwa hiyo fursa kukandamiza watu.
 
Wewe ndo kilaza..kwan hizo riba hazijulikani? Unapewa 100 unarudisha 130...ishu nayosema ww mwenyewe unajua vigezo kwann ukqchukue mkopo?...acha mkopo tafuta side hustle basi...kila sehem kuna shida...mxiew
 
Nyiye watoto wa side Chick , chips mayai, umekulia magwepande ina maana huoni watu wanavyopata taabu uko mitaani, side hustle zaweza buma,utafanyaje Moroni,
 
Nyiye watoto wa side Chick , chips mayai, umekulia magwepande ina maana huoni watu wanavyopata taabu uko mitaani, side hustle zaweza buma,utafanyaje Moroni,
Hivi umeelewa point yangu?. Shida imekukuta umeenda kopa hela...sasa why uanze kulalamika?dawa ni kulipa ....hauna jins .hutak MKOpo USIKOPE. Mie sio side chick wala nini nyie si mnataka uanze biashara jana, feb usimame! Na bado mtatukopa tu.
 
Back
Top Bottom