Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nzasa aonywa kwa kumwalika Amber Rutty kama mgeni shuleni

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,189
103,710
Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke umeeleza kuchukizwa kwake na kitendo cha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nzasa kumualika Amber Rutty kama Mgeni rasmi na kuongea na Wanafunzi.

Pia soma > Mkuu wa Mkoa, tunaomba Walimu waliohusika kumwalika Amber Rutty Shuleni wachukuliwe hatua


Uongozi wa Manispaa ya Temeke umesema haya

“Kumekua na taarifa zinazosambaa kupitia kipande cha video mitandaoni zikimuonesha Mtu mmoja akitembelea Shule ya Msingi Nzasa iliyopo Temeke, akiwa amevaa mavazi yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania”

“Tunapenda kutoa taarifa kwamba uongozi wa Manispaa ya Temeke umechukizwa na ugeni huo, umemuonya Mkuu wa Shule kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kutokana na kitendo kilichotokea na Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza”

Amber.jpg

 
Back
Top Bottom