Mwalimu mkuu na msaidizi wabambwa wakitengeneza majibu ya mtihan wa darasa la saba;shame

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,699
2,000
WATU wanne akiwamo Mwalimu Mkuu na Msaidizi wake wa Shule ya Msingi ya Kagwe kijijini Kagwe, katika Kata ya Siloka, Bukombe mkoani hapa, wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa wakiandaa majibu ya mtihani wa darasa la saba.

Watuhumiwa hao ambao ni pamoja na Msimamizi wa mtihani huo, wanadaiwa kuandaa majibu ya mtihani wa Taifa wa Kiswahili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Diwani Athumani, alisema ofisini kwake jana, kwamba watu hao walikutwa na maofisa wa Kamati ya Kusimamia Mitihani ya Taifa wa Elimu ya Msingi kwa kushirikiana na wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kirima Robert (36), Msaidizi wake, Samson Ngozi (27), Msimamizi wa Mitihani, Peter Matipa (24) na mkulima, Kuya Kunyango (24).

Kamanda Athumani alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 8.50 mchana nyumbani kwa Mwalimu Ngozi wakiandaa majibu hayo wakati mtihani ukiendelea.

Alisema mgambo aliyekuwa akilinda mtihani huo, Mpemba Kachere, alitoroka baada ya kubaini kuwa Mwalimu Mkuu, Msaidizi wake, Msimamizi wa Mtihani na mkulima huyo, wamekamatwa kwa tuhuma hizo.

“Juhudi za kumtafuta mgambo huyo kwa kushirikiana na Takukuru na Kamati hiyo zinaendelea ili kuhakikisha kuwa anakamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na wenzake,” alisema Kamanda Athumani.

Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi nchini ulianza Jumatano na kumalizika jana ambapo wanafunzi zaidi ya milioni moja walikuwa wakitarajiwa kuufanya nchi nzima.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,373
2,000
Mkulu anauza twiga , swala, dhahabu, tanzanite. Mkulu wa mitutu analamba ma-trilion sijui kwa kuuza milipuko au la. Wengine wanaingiza wa-pakistani kwa USD 10,000na mmwalimu anakula kichwa cha darasa la saba..............haya endelezeni single hii, ninauhakika itauzika.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,699
2,000
Nzova anakamata madawa atujui yamechomwa lini endeleeeeeeeeeeeeeeeaaaaaaaaaaaaaaaa
 

MWENDAKULIMA

JF-Expert Member
Jul 17, 2009
953
195
Katibu mkuu wa wizara anaandaa mpango wa kuhonga wabunge ili bajeti ipite anasimamishwa kupisha uchunguzi na ikulu,anarejeshwa kazini na ikulu ndani ya masaa 24 anasimamishwa tena na ikulu.Duh
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,327
2,000
Waziri anapoamua kuwahadaa wananji bila aibu na kutengeneza majibu feki yenye mbwembwe na utamu kuyasikiliza ili bajeti ipite akijua ni uongo mtupu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom