Mwalimu Mkuu anapomtusi Rais kupitia gazeti la Jamhuri, makala yake ya tarehe 25 Feb

Ahsante Kwa kumsaidia Mzee Mayega kutukana maana wengi hatusomi hayo magazeti hivyo hatukujua kama katukana hadi ulipotukana wewe ndio tumekusoma, tukiwa wadogo mwenzetu akitukana tunaenda kushitaki na kusema katukana hututaji tusi, ukitaja tusi unapigwa wewe uliyekwenda shtaki, hivyo wewe bila haya umemtukana na kumkashifu Raisi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
jaman mbona zamani mlikuwa mnakosea wahenga walisema mjumbe hauwawi ila nyie mlikuwa mnamuua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaomba kwanza niseme wazi sina nia ya kumchongea Mzee wangu Pascally Mayega kwa Rais wetu mpendwa, wala sina nia ya kuligombanisha gazeti pendwa la Jamhuri na Rais wetu ambaye siku za nyuma aliwai kulisfia Gazeti ili.

ila kupitia gazeti la Jamhuri la tarehe 25,mwezi huu ukurasa wa kumi na tano miwandishi niliyemtaja hapo juu aliandika makala yenye kichwa cha habar NDUGU RAIS,UPANGA UNA MAKALI KUWILI

kupitia makala hiyo aliandika hoja nzito na nzuri uitimishwaji wa makala hiyo haukuwa mzuri na haukumtendea haki Raisi wa Tanzania kwani uliambatana na TUSI zito ambalo limenifanya niandike jambo ili ninanukuuuu tusi ilo

"Hatumshangai Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwamba pamoja na kwamba ndiye Raisi mwenye umri mdogo zaidi bado anaonekana ndiye Rais anayeongoza kwa busara zaidi kuliko hata wanao onekana kumzidi umri.Hii yote si kwamba Uhuru hana ushamba urais wala hana ushamba wa Ikulu. Amezaliwa ikulu amekulia Ikulu.

Amekuwa akiyaona madaraka makubwa ya urais aliyokuwa nayo baba yake Rais Jomo Kenyatta shida ni kwetu sisi hatuna historia ya kukulia nyumbani kwa mwenyekiti. Kwetu mpaka tunaingia Ikulu ndiyo tunapata anwani. Ukiingia Ikulu lazima utakuwa mshamba. Wengi huzuzuka baada ya kutambua kuwa wamebbeba mamlaka makubwa ambayo mwanzo hawakuyafahamu"
mwisho wa kunukuuu tusi zito, sina nia au lengo la kumchochea moto ili mzee wetu awekwe korokoloni ila nina nia ya kutaka kuheshimika kwa Uraisi wa Rais wetu hata kama ametokea matopeni tuheshimu Utaasisi wa Urais huo.

Nitoe rai kwa mwariri wa jamhuri ni mhm kuhariri makala za namna hii kwani kwani sisi vijana tunaitaji kujifunza mambo mengi kutoka kwa wazee hawa ila kwa matusi haya tunaomba wabakie nayo vifuani mwao na wafe navyo ila wasivitoe.
kwa hatua zitakazochukuliwa kwa huyu mzee kutoka serikalini baada ya Bandiko ili mimi kulifikisha hapa nipo tayari kubeba lawama. kwa kuamsha walio lala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kesho usirudi hapa kama Pascal Mayalla kujiosha k'nafk' kwamba hahusiki na kukamatwa kwa kabendera wakati kimsingi makala za pascal zinamchango mkubwa sana na kuwekwa korokoroni bw kabendera.

Wakati ukijinasibu kwamba huna lengo lakumchonganisha muandishi na dola unajigamba kwamba uko tayari kubeba lawama kama muandishi wa makala hio akiwekwa korokoroni na dola.

Kwani kama umeamua kuwa mbeya na mchonganishi unaogopa nini kusema mimi ni mbeya?
Tujifunze kuacha unafki.
 
Yeyote mwenye hekima aliyesoma makala hiyo, aeelewa ujumbe. Suleiman ( Solomon) aliposimikwa kuwa mfalme wa Israeli alitoa sadaka ya ng'ombe 1000 ili Mwenyezi Mungu amkirimie hekima ya kutawala watu. Vivyo hivyo kila anaepewa madaraka yoyote kwa ngazi yoyote atafute hekima. Vinginevyo mamlaka aliyoyapata yatakuwa adui yake wa kwanza. Hakuna tusi katika makala hiyo. Bali pana somo kubwa lililojificha katikati ya maandishi/maneno.

..kama Suleiman alitoa sadaka ya ng'ombe hapa inatolewa sadaka ya wapinzani.

..Alphonce Mawazo ndiyo alikuwa sadaka ya kwanza kutolewa.
 
Kwa maoni hayo na ushauri wa kishamba zaidi wanaotakiwa ikulu ambao wamekulia huko na kuwa wazoefu wa ikulu uraisi Tz ni
1. Makongoro wa JK Nyerere
2. Hussein wa AH Mwinyi
3. Ridhiwani wa JM Kikwete
Wengine nendeni kwenye sanduku la kura kuchofua kidole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini mambo ya ukweli msiyotaka kuambiwa mnaya badili na kuyaita matusi? Je,huyo Rais hakuna mambo mabaya aliyowatendea watanzania zaidi ya matusi? Unatambua kuwa kuna watu wamepoteza Maisha sababu ya kuvunjiwa Nyumba zao? Unafahamu kuwa wengine hawakuvunjiwa nyumba zao sababu walimpigia kura RAIA?Unafahamu kuwa kuna watu wanadhalilishwa majukwaani? Hivi unafikiri hao hawaumii?
Ninaomba kwanza niseme wazi sina nia ya kumchongea Mzee wangu Pascally Mayega kwa Rais wetu mpendwa, wala sina nia ya kuligombanisha gazeti pendwa la Jamhuri na Rais wetu ambaye siku za nyuma aliwai kulisfia Gazeti ili.

ila kupitia gazeti la Jamhuri la tarehe 25,mwezi huu ukurasa wa kumi na tano miwandishi niliyemtaja hapo juu aliandika makala yenye kichwa cha habar NDUGU RAIS,UPANGA UNA MAKALI KUWILI

kupitia makala hiyo aliandika hoja nzito na nzuri uitimishwaji wa makala hiyo haukuwa mzuri na haukumtendea haki Raisi wa Tanzania kwani uliambatana na TUSI zito ambalo limenifanya niandike jambo ili ninanukuuuu tusi ilo

"Hatumshangai Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwamba pamoja na kwamba ndiye Raisi mwenye umri mdogo zaidi bado anaonekana ndiye Rais anayeongoza kwa busara zaidi kuliko hata wanao onekana kumzidi umri.Hii yote si kwamba Uhuru hana ushamba urais wala hana ushamba wa Ikulu. Amezaliwa ikulu amekulia Ikulu.

Amekuwa akiyaona madaraka makubwa ya urais aliyokuwa nayo baba yake Rais Jomo Kenyatta shida ni kwetu sisi hatuna historia ya kukulia nyumbani kwa mwenyekiti. Kwetu mpaka tunaingia Ikulu ndiyo tunapata anwani. Ukiingia Ikulu lazima utakuwa mshamba. Wengi huzuzuka baada ya kutambua kuwa wamebbeba mamlaka makubwa ambayo mwanzo hawakuyafahamu"
mwisho wa kunukuuu tusi zito, sina nia au lengo la kumchochea moto ili mzee wetu awekwe korokoloni ila nina nia ya kutaka kuheshimika kwa Uraisi wa Rais wetu hata kama ametokea matopeni tuheshimu Utaasisi wa Urais huo.

Nitoe rai kwa mwariri wa jamhuri ni mhm kuhariri makala za namna hii kwani kwani sisi vijana tunaitaji kujifunza mambo mengi kutoka kwa wazee hawa ila kwa matusi haya tunaomba wabakie nayo vifuani mwao na wafe navyo ila wasivitoe.
kwa hatua zitakazochukuliwa kwa huyu mzee kutoka serikalini baada ya Bandiko ili mimi kulifikisha hapa nipo tayari kubeba lawama. kwa kuamsha walio lala.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesho usirudi hapa kama Pascal Mayalla kujiosha k'nafk' kwamba hahusiki na kukamatwa kwa kabendera wakati kimsingi makala za pascal zinamchango mkubwa sana na kuwekwa korokoroni bw kabendera.

Wakati ukijinasibu kwamba huna lengo lakumchonganisha muandishi na dola unajigamba kwamba uko tayari kubeba lawama kama muandishi wa makala hio akiwekwa korokoroni na dola.

Kwani kama umeamua kuwa mbeya na mchonganishi unaogopa nini kusema mimi ni mbeya?
Tujifunze kuacha unafki.
hahahaha hahahaha haya mimi ninakili ni mbeya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom