Mwalimu Mkuu ajiua baada ya kutuhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za ujenzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Iringa. Mkuu wa Sekondari ya Mbalamaziwa, Roida Mbalwa amefariki dunia kwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa mkutano na kiongozi mmoja kutumia fedha vibaya za ujenzi.

Mume wake, Sharif Utenga alisema kiongozi huyo alifanya mkutano wa hadhara kata ya Mbalamaziwa na wananchi walieleza kuchangishwa michango mingi.

“Ninachokifahamu alikuja (anamtaja) alizungumza na wananchi walidai michango imekuwa mingi kitu ambacho kiliamsha kwenda kumkagua mwalimu baada ya ukaguzi waligundua kuna hasara takriban Sh200 milioni,” alisema Utenga.

Alisema mara kwa mara wakaguzi wa halmashauri ya Mufindi walikuwa wakifika shuleni na kukagua ujenzi kwa sababu majengo hayo yanatarajia kuzinduliwa na Mwenge.

“Mke wangu alikuwa akipata presha ya kazi kutoka kwa viongozi waliofika kuwa wakali na kumtuhumu kutumia fedha vibaya, alikuwa akiwaambia walimu wenzake kuwa ipo siku nitakuja kujiua,” alisema Utenga.

Hata hivyo, diwani wa Mbalamaziwa Zubeir Nyamolelo alisema mwalimu huyo hajawahi kutuhumiwa kwa lolote.

“Mikutano yote nilikuwa na (kiongozi huyo) hakuwahi kumtuhumu kwa ubadhilifu na hakuna mkaguzi yeyote aliyewahi kuja,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema mwalimu huyo waliyemzika jana walikuwa wanamtegemea na amefanya kazi vizuri kwa miaka 12.

“Sina taarifa yoyote ya matumizi mabaya ya fedha ambayo inaweza kusababisha anywe sumu, hapana kabisa!” alisema William.

Mmoja wa walimu wa shule hiyo, Philipo Mkandawile alisema kifo hicho kilitokea Jumatano iliyopita.
 
Muke ya jamaa yangu Ngunyali hiyo. Tulimzika kijijini kwa mumewe Ikongosi! Apumzike kwa amani.
 
Muke ya jamaa yangu Ngunyali hiyo. Tulimzika kijijini kwa mumewe Ikongosi! Apumzike kwa amani.
Aisee nawafahamu wote wawili, Ngunyali na Mbalwa ingawa sijaelewa hapo wanaposema mume wake ni Sharifu Utenga (au ni jina la huyohuyo Ngunyali?)..

Nimesikitika sana kupata taarifa hii ya kifo.
 
acha ujinga ata kama ni chuki hii imezidi sawa hatumpendi lakini sio kwa stahili hii chuki izo zisizo na maana zitageuka sumu kwenu
Serikali ya jiwe mtajibu nini mbinguni
Watu mpk wanajiuwa
 
Aisee nawafahamu wote wawili, Ngunyali na Mbalwa ingawa sijaelewa hapo wanaposema mume wake ni Sharifu Utenga (au ni jina la huyohuyo Ngunyali?)..
Nimesikitika sana kupata taarifa hii ya kifo.

Sharif ni jina lake la kwanza bila shaka. Hilo la Utenga huenda ni official name yake tofauti na lile la Ngunyali ambalo wengi ndiyo tumelizoea.

Jamaa ni mtu poa sana kwa kweli ukimlinganisha na huyo mke wake aliyefariki mbaye wadau wengi walimchukulia kama mkuda fulani vile.
 
Utakuta waliomtuhumu ni wale waliokuwa wanampa maelekezo off record

William Mgimwa alikuwa Waziri wetu wa Fedha

Daud Balali alikuwa Governor wetu
 
Sharif ni jina lake la kwanza bila shaka. Hilo la Utenga huenda ni official name yake tofauti na lile la Ngunyali ambalo wengi ndiyo tumelizoea.

Jamaa ni mtu poa sana kwa kweli ukimlinganisha na huyo mke wake aliyefariki mbaye wadau wengi walimchukulia kama mkuda fulani vile.
Usemayo ni kweli kabisa aisee, hakika unawafahamu vyema hawa watu.
 
Back
Top Bottom