Mwalimu Mkuu Afrika Kusini amlazimisha mwanafunzi kutafuta simu kwenye shimo la Choo

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,758
20,150
Mwalimu mkuu wa shule moja nchini Afrika Kusini amesimamishwa kazi kwa madai ya kumlazimisha mwanafunzi kijana wa miaka 11 kutafuta simu kwenye shimo la choo.

SA headteacher 'made pupil dig in poo for lost phone'

Inadaiwa kwamba mwalimu huyo alimshukisha mwanafunzi huyo kwenye shimo la choo kwa kutumia kamba akimuahidi randi 200 sawa na dola 14 za Marekani.

Bibi ya kijana huyo amesema mjukuu wake anaogopa kwenda shuleni kwasababu wanafunzi wengine wanamdhihaki.

Bodi ya elimu ya eneo imezungumza na gazeti la TimesLive na kusema tukio hilo ni “aibu”.

Vyoo vya mashimo nchini Afrika Kuusini ambapo mwaka jana vilikadiriwa kuwa sudusi au moja ya sita ya shule zote bado vinatumika licha ya kwamba ni hatari.

Afisa wa juu wa elimu eneo la Mashariki la Cape, Fundile Gade, amewaambia wananahabari kuwa tukio hilo lilikuwa “zaidi ya aibu” na atamtembelea mwanafunzi huyo nyumbani kwao kuomba msamaha.

Mwalimu mkuu anayedaiwa kutekeleza hayo katika shule ya Luthuthu Junior sasa hivi anachunguzwa na idara ya Cape ya Mashariki na hatua stahiki zitachukuliwa.

Inasemekana kuwa pia alihamasisha watoto wengine kusaidia kutafuta simu hiyo ambayo inadaiwa ilianguka kwa bahati mbaya katika choo cha walimu mwanzoni mwa Machi.

Vyombo vya habari vya eneo vimesema tukio hilo lilijulikana baada ya shirika lisilo la serikali ambalo linafanyakazi ya kuhamsisha umuhimu wa kwenda shuleni kusikia kuhusu kisa hicho.

Petros Majola, kutoka shirika la jamii la Khula aliweka video mtandaoni ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha kuwa utafutaji wa simu hiyo uliendelea kwa saa moja.

Baada ya baadhi ya wanafunzi kutumia ndoo kupunguza kinyesi ndani ya shimo hilo la choo, Bwana Majola amenukuliwa akisema kwamba kijana huyo alishukishwa kwa kamba hadi “magoti yake yakawa yameingia ndani ya kinyesi”.

“Alitumia mikono yake kutafuta simu hiyo huku kinyesi kikimfikia juu ya mikono yake na kiwiko cha mkono.”

Kulingana na taarifa za News24, baada ya simu hiyo kukosekana, mwalimu mkuu alimpa mtoto huyo randi 50 kwa juhudi zake.

Bibi yake kijana huyo amesema kuwa mjuu wake aliona aibu sana kurejea shuleni baada ya kitendo hicho.
 
Back
Top Bottom