Mwalimu Mishael Muze alikataa uteuzi wa Rais ili aendelee na kazi ya Ualimu

bangusule

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
291
190
Mwalimu.jpg

Wengi wamekuwa wakiuliza kama kuna Mtanzania mwenye ujasiri wa kukataa uteuzi wa Rais.

Ukweli ni kwamba wapo na imepata kutokea kwa Mwalimu Mishael Muze ambaye alikataa uteuzi wa kuwa mkurugenzi wa maendeleo na kuendelea na kazi yake ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida.

Kutokana na uamuzi wake huo Mwalimu Mishael Muze alipewa karipio kali na akapunguzwa mshahara. Pamoja na tukio hilo miaka michache baadae Mwalimu Muze aliteuliwa kuwa Kamishna wa Elimu Tanzania.

Historia ya Mtanzania huyu ambaye alitumikia kama mwalimu na mhadhiri wa vyuo mbalimbali Tanzania, Kenya, Uganda, Zimbabwe, na Marekani, unaweza kuisoma hapa chini.


cc Saint Ivuga, Mpuretamu , Dingiswayo,
King'asti , SMU, Mtambuzi, Companero, Nguruvi3
 
1620866353152.png


Mishael Shogholo Muze kitaaluma ni mwalimu wa hisabati. Anayo historia ya kufundisha shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati, na vyuo vikuu. vilevile alitumikia kama kamishna wa elimu tanzania. Ni mwanataaluma mwenye shahada ya uzamifu PhD,na ameandika vitabu mbalimbali vya hisabati.
 
Ni jambo la kufikirisha sana kwa Mwalimu Mkuu / Headmaster wa Mwenge Sekondari kukataa uteuzi wa kupanda cheo kuwa Mkurugenzi wa maendeleo wa mkoa. inaonyesha jinsi waalimu wa miaka ya zamani walivyokuwa wanaipenda kazi yao. pia inaonyesha heshima / prestige ya kazi ya ualimu miaka hiyo.

Bila shaka kazi ya ualimu ilikuwa na heshima na fahari ndiyo maana Mishael Muze akaona inampendeza zaidi kuliko mamlaka ya ukurugenzi wa maendeleo na uteule wa Rais. lingine ni kwamba waalimu wetu wa zamani kama Mishael Muze walikuwa na wito wa ualimu, hivyo haikuwa rahisi kushawishika kwa vyeo na madaraka serikalini na ktk chama.
 
Wote watatu katika picha hapo juu waliwahi kuwa waalimu wakuu wa shule za sekondari.

Tabitha Siwale alikuwa mwalimu mkuu korogwe girls.

Mishael Muze mwalimu mkuu mwenge sekondari.

Donald Kusenha mwalimu mkuu forodhani sekondari.
 
funzo kubwa hapa ni watu kupenda taaluma zao, na kutokulazimika kufanya kazi wasizoziweza, au wasizozipenda, kwasababu tu wameteuliwa na wakubwa.
 
Mark Mwandosya alitakiwa kuwa Rais wetu awamu ya Nne, tusingekuwa tumefikia hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom