Mwalimu Mei Mosi '95: "Watanzania Mjomba wenu ni nani?"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya hotuba aliyoitoa Baba wa Taifa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995. Tunapokumbuka miaka nane tangu Mwalimu Nyerere afariki hatuna budi kupitia japo kwa hatua hazina ya hekima yake.

Wakati anatoa hotuba hii mwaka 1994 kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi, na mwaka 1995 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi na huo ukiwa ni uchaguzi wa kwanza baada ya kurejesha tena mfumo wa vyama vingi. Hivyo, Mwalimu alipokuwa anatoa hotuba hii watu wengi walikuwa wanaonesha nia ya kutaka kwenda Ikulu na alitumia nafasi hiyo pia kuliasa taifa.

Hotuba hii imekuwa ikinukuliwa na watu wengi ila wengi wetu hatuna uhakika Mwalimu alisema nini hasa siku hiyo. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba nzima. "Kuna nini Ikulu?" Ni mojawapo ya maswali ambayo Mwalimu aliuliza siku ile... sisi leo hii tumeanza kupata majibu..

Sikiliza: KLH Exclusive.
 
Mkuu hiyo hotuba nimekuwa nikiisaka kwa udi na uvumba as niliambiwa ina mambo mengi ambayo ni kama utabiri wa hali halisi ya sasa.
Mungu amlaze mahara pema peponi baba yetu
Ntashukuru kama ukitupatia na nyinginezo nyingi ili tuweze pata maneno ya busara ya mzee wetu.
Keep it up Mwanakijiji
 
Mheshimiwa mwanakijiji ahsante sana kwa kutukumbusha hayati J.K.Nyerere Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema, Amina.

Unajua mwalimu anazungumza vitu ambavo kama huelewi au havikuingii basi....!

Anazungumzia umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana kama wafanyakazi, lakini pia nimekumbuka labda alikuwa akizungumzia jinsi wafanyakazi wanavoweza kuunda umoja mpya kwa kutetea maslahi yao.

Nasubiri hotuba ingine mkuu.
 
Mkombozi sijui vipi kwa upande wangu inasikika vizuri, tatizo ni kuwa kuiweka katika audio kutoka VHS ilikuwa ni kasheshe, natumaini sehemu ya pili na ya tatu nitaweza kuifilter vizuri katika digital format..
 
Ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya hotuba aliyoitoa Baba wa Taifa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995. Tunapokumbuka miaka nane tangu Mwalimu Nyerere afariki hatuna budi kupitia japo kwa hatua hazina ya hekima yake.

Wakati anatoa hotuba hii mwaka 1994 kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi, na mwaka 1995 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi na huo ukiwa ni uchaguzi wa kwanza baada ya kurejesha tena mfumo wa vyama vingi. Hivyo, Mwalimu alipokuwa anatoa hotuba hii watu wengi walikuwa wanaonesha nia ya kutaka kwenda Ikulu na alitumia nafasi hiyo pia kuliasa taifa.

Hotuba hii imekuwa ikinukuliwa na watu wengi ila wengi wetu hatuna uhakika Mwalimu alisema nini hasa siku hiyo. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba nzima. "Kuna nini Ikulu?" Ni mojawapo ya maswali ambayo Mwalimu aliuliza siku ile... sisi leo hii tumeanza kupata majibu..

Sikiliza: KLH Exclusive.

Vyama vya wafanyakazi Tz havihitajiki . Havina maana kwa mfanyakazi wa Tz., Kwishne.
 
Back
Top Bottom