Mwalimu Lukindo atupwa jela miaka mitatu kwa kumpa mimba mwanafunzi.

gumzomatata

Member
Sep 26, 2012
9
0
MWALIMU wa Shule ya Msingi Magamba, wilayani Handeni, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na kumpa mimba mwanafunzi.

Mwalimu huyo, Daniel Lukindo (24), alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumpa mimba mwanafunzi Halima Rashidi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kwaluguru.

Akisoma mashitaka katika shauri hilo namba 240 la mwaka huu, Mwendesha mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibaliki Polangyo, alieleza mahakama kuwa kati ya Novemba mwaka jana na Februari mwaka huu katika Kijiji cha Magamba, mwalimu Lukindo alikuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo na baadaye, kumpa ujauzito.

Katika kesi hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana, mshtakiwa alikiri kosa lake, akikubaliana na maelezo yote yaliotolewa na mwendesha mashitaka. Kufuatia hatua hiyo, Hakimu Maligana, alimtia hatiani na kumhukumu kutumikia adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Akifafanua kuhusu adhabu hiyo, Maligana alisema mshtakiwa alitenda kosa baya na hasa ikizingatiwa kwamba ni mwalimu anayepaswa kuwa mfano mzuri katika jamii, kwa kuzuia na kukomesha wimbi la matukio ya wanafunzi wa kike kupata mimba.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI
 
Miaka mitatu ni michache sana. Alitakiwa apigwe Kama minimum miaka 10 na kazi ngumu huko jela. Halafu akitoka jela awe anakaa mbali mita 100 na watoto wenye umri wa chini ya miaka 18. Nyang'au mkubwa huyo.
 
Hamna kitu hapo kwani alimkuta huyo binti akiwa bikra na miaka yote 3 ya nini wakti anatakiwa alee mtoto? Hizi sheria zifanyiwe mabadiliko maana wanafunzi wengi wa sekondari wanakubwa na matatizo haya
 
...Hivi hii sheria ya Kumdunga mimba mtoto wa shuleilibadilikaga?? Si ilikuwa ukifanya kosa hili Unatungikwa miaka SABA ama??
:A S 39:
 
Miaka mitatu ni michache sana. Alitakiwa apigwe Kama minimum miaka 10 na kazi ngumu huko jela. Halafu akitoka jela awe anakaa mbali mita 100 na watoto wenye umri wa chini ya miaka 18. Nyang'au mkubwa huyo.

naona hii post ingehamie kule kwenye jukwaa la sheria ili tufafanuliwe, hivi hapa, victim amevunja sheria ipi; kwani huyu binti ni "under 18?",
 
Back
Top Bottom