Mwalimu kweli uliondoka na chako........haya ni dhihaka kwa watanzania!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu kweli uliondoka na chako........haya ni dhihaka kwa watanzania!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaKiiza, May 3, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  NHC tunauza nyumba kwa bei nafuu..milioni 119,000,000/= Zakitanzania!!!
  Hapo ndipo nimekumbuka Hayati Mwalimu Nyerere aliyeweka misingi bora kwakuanzisha makampuni mbalimbali kati ya makampuni hayo nayoweza kukumbuka ambalo mpaka leo linaendelea kuneemesha wachache na kutupilia mbali madhumuni ya kuanzisha shirika hilo ni hili hapa lijulikanalo..National Housing Corporation (NHC)au kwalugha raisi ni Nasho Hauzingi kwakusema kweli shirika hili lilikuwa lakuwakomboa wa lalahoi tofauti na sasa!!
  Sidhani kama inamuingia hakilini mtu wakawaida anaposikia eti tuna nyumba tumejenga za bei nafuu zinauzwa kwa shiling milioni 119.000,000/=
  Kama mtanzania wakipato cha kawaida kweli atapata wapi uwezo wakuwa na kiasi hicho chapesa??au ni mipango yao kujinyakulia viwanja vizuri vya magomeni na kwingineko??
   
 2. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  wew mfuasi wa chadema huwezi lakini magamba hiyo kwao ni kama tone la maji.
   
 3. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Mwl tunakukumbuka sana leo.Leo NHC nayo imegeuka genge la mafisadi la ten % na kupoteza dhana nzima ya kuwepo kwake tangu mwalimu ataifishe nyumba za wahindi.Hivi kweli nyumba vyumba 3 gharama TZS 163,000,000 hiyo kweli hata kama kuna margin profit ya 30%.?.Naamini sasa kushindina kufisadi menegment inahangaiaka kuibua miradi mingi hata kama itakuwa ni white elephant ili mradi wao wamevuta chao na kutokomea na baadaye shirika litakuwa kwenye matatizo ya kifedha na kujifanya kukopa fedha benki kwa ajili ya kuendelea na miradi huku nymba nyingi zikiwa hazijanunuliwa.Kuboresha makazi na utu wa mtanzania shirika ili lingeweza kujenga nyumba za kisasa kwa wananchi nyumba bora kwa wale wenye viwanja vyao na wanaweza kulipia kwa makubaliano na nyumba hizo zinakuwa collateral.KULIKO UFISADI HUU,HIVI KIKWETE NA PROF WAKE TIBAIJUKA WANA VISION KWELI ?
   
 4. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hili shilika ni suggest libadilishwe jina halifai tena kuitwa NHC kwa maana maudhui ya NHC hayapo tena.. waliite NOA(NOBLE ONLY ALLOWED) kidogo litaleta maana, huwezi kuliita shirika la nyumba la taifa wakati wapangaji wote matajiri...
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Himi kinacho nishangaza ni huyu Waziri Anna Tibaijuka huyu alikuwa Executive wa UNHABITAT Duniani kajenge watu kule Nairobi,Rio de jenairo Colombia,bogota na kwingineko kwingi kweli hajisikii unyonge mawazoni kuona shirika ambalo lipo chini yake linafanya wizi wa mchana kweupe eti lina wasaidia watu wachini kwa kuwauzia nyumba TZS 163,000,000 wakati hili shirika linakua ruzuku kibao kutoka serikalini mimi sijui kwakweli hii nchi sijui niwapi walipo wenye uchungu sijawaona!!

  Tutawashitaki kwa wananchi 2025!

  Wanamipango mibaya kama ya kuuza viwanja na nyumba za serikali za Obay ambako nenda uendako huwezi kupata kiwanja obay kama huna mabilioni!!lakini CCM walijichukulia kwa bei chee!!
  Eemungu tunusuru!!
   
Loading...