Mwalimu Hemed Mwaipopo achinjwa kama kuku Mbeya

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
Serikali mkoani Mbeya, imelaani vikali mauaji ya Mwalimu Hemed Mwaipopo (54) wa shule ya Msingi Mwenge wilaya ya Kyela anayedaiwa kuchinjwa shingoni na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kutelekezwa pembezoni mwa barabara kuu ya Ipinda Matema Wilayani humo.

Mwalimu Mwaipopo alikuwa mkazi wa Kitongoji cha Mpanga Kijiji cha Mpunguti Kata ya Ikama anasadikika kuchinjwa na watu wasiojulikana kwa sababu za mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya marehemu na familia iliyomuuzia eneo alilojenga nyumba yake.

 
Mwili waliutelekeza hapo hapo nyumbani...si barabarani Kama habari ilivyoandikwa
 
nasadikika kuchinjwa na watu wasiojulikana kwa sababu za mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya marehemu na familia iliyomuuzia eneo alilojenga nyumba yake.

Wanajulika hapo
 
Police: Tunafanya uchunguzi na tunawakamata

Wanandugu: Chukua mchanga na nguo zenye damu tukafute kizazi chote cha waliohusika kwa namna moja au nyingine.
 
...sasa kama ni Familia iliyomuuzia kiwanja alichojengea nyumba yake, kulizuka mgogoro gani tena uliopelekea kifo chake??
Hao wajinga waliofanya hivyo walifikiri kweli kuhusu maumuvi ya Wanawe na Mkewe?
 
Watu wana roho ngumu a see, apumzike tuu kwa amani japo ameuwawa kwa mateso na unyama wa ajabu,R.I.P mwalimu
 
mbeya pamoja na kuwa na madhehebu 400 tofauti ya dini lakini ndio mkoa unaooongoza kwa matukio ya kutisha dini haijasaidia kabisa jamii ya watu wa mbeya
Nyingi ya dini za Mbeya sio za ki taasisi. Ni Kama haya maigizo ya gwajiboy, mzee wa upepo, mzee wa mafuta, mwampussy. Ni wapiga dili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom