Mwalimu elimu, tingatinga bomoa bomoa

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Kuna methali inasema "Jina humuua mwenyewe",
Tuliwahi kuwa Na kiongozi aliyeitwa "Mwalimu". Matokeo ya jina hilo in wananchi waume, wake na watoto kupatiwa Elimu bure kupitia program mbali mbali. Mamilioni ya watu wazma ambao hawakubahatika kusoma katika utoto wao walipatiwa Elimu nchi nzima.

Watoto wrote waliweza kuandikishwa darasa la kwanza kupitia mpango was UPE.
Ni katika nyakati hizo ambapo Elimu toka chekechea hadi chuo kikuu ilikuwa bure. Na Elimu ya juu iliku
wa inatolewa katika mazingira yenye hadhi ya kutosha

Kiongozi wetu was sasa anaitwa Tingatinga (Bulldozer) Mashine maalum za sekta ya ujenzi, ambazo pia hutumika kubomoa Nyumba.

Toka aingie madarakani nchi imetawaliwa Na bomoa bomoa ya Nyumba za wananchi, hususan katika maeneo yanayoongozwa wabunge, madiwani Na wenyeviti wa vijiji Na mitaa kutoka upinzani.

Chini ya utawala huu wananchi wameonewa sana Kwa kubomolewa Nyumba zao, kupokwa Ardhi zao Na kurejeshwa katika umaskini wa kutupwa Kwa kisingizio eti in wavamizi.

Kama ambavyo zama za 'Mwalimu" nchi ilivyoendea Kielimu. Zama za Bomoa bomoa mwenyezi mungu amechoshwa Na uonevu huu unaoendelezwa Na utawala huu Na hivyo ameanza kutoa adhabu Kwa kuteremsha gharika linalobomoa bomoa miundombinu Tingatinga aliyojivunia kuijenga.

Kwa Mara ya kwanza toka baadhi vituo vya kupima viwango vya mvua kujengwa mwaka 1918 haijawahi kunyesha mvua kama iliyonyesha jijini Dar es Salaam tarehe 25-26 Okt 2017 Na kuzoa madaraja, barabara n.k. Gharika hili limevuruga mfumo mzima wa miundomninu hapa jijini, hivyo kumvurugia Tingatinga utekelezaji was ahadi zake Kwa sababu atalazimika kutumia mabilioni ya shilingi kurejesha miundombinu husika.

Je ni kwanini gharika hili litue Dar peke yake. Ni kwa sababu jiji hili linaongozwa Na kiongozi aliyebariki wananchi kuonewa Kwa kubomolewa Nyumba zao, kuporwa Ardhi zao n.k. Yeye ndio ametoa askari wa kusimamia bomoa bomoa hizi.

Hili linatakiwa kuwa funzo maaluma Kwa Tingatinga Na kiongozi wa Dar kuwa uongozi in dhamana. Lakini mungu yupo. Na akichoshwa Na udhalimu wa viongozi hupitisha adhabu yake. Kama ilivyokuwa kwenye enzi za Gharika katika vitabu vya dini wanaoumia ni waliohusika Na dhambi Na wasiohusika. Kwa sababu wakazi wa Dar walikuwa wanashabikia bomoa bomoa hizi dhalimu ndio maana itawapasa kuteseka Kwa hii hukumu ya mungu.

Hili liwe fundisho Kwa Tingatinga Na kiongozi was Dar kuwa wao sio Alpha Na Omega.
 
Enzi za mwalimu Tanzania ilikaribia kufika literacy level 100%, watu kujua kusomana kuandika.

Mpaka wazee walisomaelimukwa watu wazima.

Siku hizi hata watoto wanaomaliza shule wengine kusoma hawajui.
 
Enzi za mwalimu Tanzania ilikaribia kufika literacy level 100%, watu kujua kusomana kuandika.

Mpaka wazee walisomaelimukwa watu wazima.

Siku hizi hata watoto wanaomaliza shule wengine kusoma hawajui.
Hayo ndio mafanikio ya kiongozi kujikita katika kukuza Elimu had I kuitwa Mwalimu. Sasa tuko zama za bomoa bomoa ndio maana Na mungu anatuongezea ubomoaji was miundombinu
 
Sasa wewe mtoa mada mtu wa ajabu kabisa unasifia mvua wakati imeleta madhara makubwa sana kwa wananchi nyumba nyingi zimebomoka na kutengeneza nyufa.
 
Soma thread vizuri mkuu! Mleta thread hajasifia mvua ila ametoa onyo.
Wewe ndiyo soma vizuri... Mtoa mada ameisifia mvua iliyoharibu miundombinu ili kumkwamisha Rais Magufuli kutekeleza majukumu.

Mtoa mada yeye anafurahi sana kwa mvua hii maana unamlilia Rais Dr Magufuli
 
Sasa wewe mtoa mada mtu wa ajabu kabisa unasifia mvua wakati imeleta madhara makubwa sana kwa wananchi nyumba nyingi zimebomoka na kutengeneza nyufa.
Kwani bomoa bomoa haikuwasababishia madhara wahanga? Wapo waliopoteza maisha kwa mshtuko, familia zinalala nje na kuharibiwa kwa njia za kujitafutia riziki.
Mungu amekasirishwa Na Jamii ya kinafiki inayoshindwa kukemea uonevu ndio maana kashusha gharika (tingatinga kuu) ili liwe funzo kwa viongozi wanaowaonea watu wanaowaongoza.
 
Back
Top Bottom