Mwalimu Chaula: Mambo manne yanayofelisha viongozi - Part 2; Kushindwa kukuza uwezo wa watu

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
484
541
MAMBO MANNE YANAYOFELISHA VIONGOZI-PART 2-Kushindwa kukuza Uwezo wa watu. (FAILURE IN TALENTS DEVELOPMENT)

Mtu mmoja aliwahi kusema, "good leaders have many followers but great leaders produce many leaders." Akimaanisha kwamba, "viongozi wazuri wana wafuasi wengi sana wanaowashabikia lakini viongozi bora zaidi wanazalisha viongozi wengine."
.
John Maxwell mtaalamu wa mambo ya uongozi aliweka Level 5 za uongozi:

~ Level 1 - positional leadership:Watu wanakufuata kwa sababu ya nafasi yako,ukiondoka kwenya nafasi hauna ushawishi tena.

~ Level 2 - permission leadership: watu wanakufuata kwa sababu wameanza kukupenda na umejenga mahusiano nao.

~ Level 3 - production:Kuna vitu umefanya/Matokea umepata yanayokupa mamlaka ya kiuongozi.

~ Level 4 - people development:Kuwekeza katika kuwafanya watu wawe bora zaidi.
.
Viongozi wengi sana wanasumbuliwa na “Leadership Insecurity “-Hofu ya kuogopa kuwa wakiruhusu watu wengine wakue zaidi au wawe bora zaidi watachukua nafasi yao.Matokeo yake kila wanayemuona ana mbegu ya ukubwa wanamkandamiza asiinuke.
.
Viongozi wazuri ni wale wanaoweza kuwafanya wafuasi wao wa leo wawe viongozi wa kesho.Usijivunie pale ambapo mambo yanaharibika unapoondoka bali furahia pale ambapo unaondoka na unaacha mtu uliyemkuza ili aendeleze yale uliyoanzisha.
.
See You AT The Top

#TIMIZAMALENGOYAKO
 
Back
Top Bottom