Mwalimu Awafundisha Wanafunzi Jinsi ya Kumuua Obama Rais wa Marekani, Barack Obama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Awafundisha Wanafunzi Jinsi ya Kumuua Obama Rais wa Marekani, Barack Obama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Marekani, Barack Obama Wednesday, May 19, 2010 4:39 AM
  Mwalimu wa somo la hisabati wa nchini Marekani anachunguzwa na shirika la ujasusi la Marekani baada ya kutumia mfano wa kumuua rais wa Marekani, Barack Obama kuwaelekeza hesabu wanafunzi wake. Mwalimu huyo wa mji wa Alabama, alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake somo la hisabati mada ya Jometri (Geometry) wakati alipotumia mfano wa kumuua Obama kuwaelekeza hisabati wanafunzi wake.

  Mwalimu huyo ambaye hakutajwa jina lake alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake mistari sambamba na pembe za maumbo mbali mbali wakati alipowaelekeza wanafunzi wake wasimame wapi ili kupata engo nzuri ya kumpiga risasi rais Obama.

  "Ukiwa kwenye jengo hili itakubidi ukae kwenye pembe hii ili kuweza kumtungua Obama", alisema mwalimu huyo.

  Mwalimu huyo alihojiwa na polisi baada ya mtu mmoja kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya tukio hilo.

  Taarifa zimesema kuwa mwalimu huyo hakutiwa mbaroni wala kufunguliwa mashtaka mahakamani lakini FBI wanamfanyia uchunguzi.

  Uongozi wa shule yake ya Corner High School umesema kuwa hauna mpango wa kumfukuza kazi mwalimu huyo na utamruhusu aendelee na kazi kama kawaida.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Loading...