Mwalimu awaficha wanafunzi kichakani baada ya kufumaniwa na Naibu waziri Mwanri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu awaficha wanafunzi kichakani baada ya kufumaniwa na Naibu waziri Mwanri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Jan 20, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Picha Kushoto:
  Msafara wa naibu waziri wa tamisemi Aggrey Mwanri ukipita eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima

  Picha Kulia:
  Mwalimu wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa mwalimu Mgaya akipita katika eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima na kuacha majembe na kukimbia kujificha


  [​IMG] ​[​IMG]
  Picha Kushoto:
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa wakiwa wamejificha katika kichaka pamoja na walimu wao kumkwepa naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri leo

  Picha Kulia:
  Wanafunzi wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa wakilima shamba la shule mida ya masomo majira ya saa 3 asubuhi leo baada ya kufanya ziara ya ghafla eneo hilo


  [​IMG] [​IMG]
  Picha Kulia:
  Naibu waziri wa Tamisemi akiwahoji walimu na wanafunzi waliokuwa wakiwatumikisha watoto wa shule mida ya masomo leo

  Picha Kushoto:
  Mwanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa akiwa amebeba majembe baada ya naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kuagiza warudi madarasani leo asubuhi

  BAADA ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Aggrey Mwanri kuukataa mradi wa umwagiliaji katika kata ya Lifua wilayani Ludewa uliojengwa kwa zaidi ya shilingi milinio 500 bila kufanya kazi kutoka na kubomoka kabla ya muda na ule wa ukarabati wa nyumba ya mganga kata ya Lupanga iliyokarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni 7 ,mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibu waziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.

  Mbunge Filikunjombe aliwakataa wahandisi hao wawili Christopher Nyandiga wa maji na mhandisi wa ujenzi Rashid Mtamila leo katika ukumbi wa Halmashauri yawilaya ya Ludewa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya naibu wazirihuyo katika kutembelea miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Ludewa. Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewaimegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambaowamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuhujumu miradi ya kimaendeleoinayoibuliwa katika wilaya hiyo.

  Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewakufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyeshauaminifu katika utendaji wa kazi yao. “Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasema heri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadiunaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu “ Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwa miradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumia fedha nyingi zaidi .

  Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi . Akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji. Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenyedaraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2.

  Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu yakulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huohivyo hawezi kujibia swali hilo. Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upande wake hajapendezewa na ufisadi mkubwauliofanyika katika miradi hiyo.

   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe walikuwa wanalima shamba la shule? Ratiba ilikuwa inaonesha vipindi gani wakati huo?
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  ratiba ilikuwa inaonyesha wana kipindi gani? au ilikua siku ya kulima?
  kwa tuliosoma vijijini ni kawaida kuna siku lazima mkatumike shamba, ila sijui kizazi hiki cha dot.com vipi hakitaki mafunzo kwa vitendo?
   
 4. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  hizi picha zinanikumbusha enzi zetu wakati tukisoma huko kijijini. Ila kwasasa kijijini kwetu haya mambo hayapo tena. Kumbe sehemu nyengine kama kawaida?
   
 5. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  serikali wameyataka wenyewe
   
 6. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Hii naona Haina Shida ndio Elimu Ya Kujitegemea!! Sasa mnaosomesha Watoto wenu Kwenye English medium Mnashangaa? Kwani na nyie Hamjui Kwa nini Tanzania ni Maskini!! Alijisemea fulani!!!
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Jimbo hilo kama lingekuwa la yule mgombea Ubunge wa UPDP kule Igunga angewanunulia "Power Tiller" na kuachana kulimia majembe kama Baba Ubaya!
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  shule za vijijini wanafunzi hufanya kazi ya kujitolea kulima mashamba ya walimu na wenyeviti wa vijiji wakati zamani wanafunzi walikuwa wakilima mashamba ya shule na kuiletea uchumi shule na kujizoesha elimu ya kujitegemea. Mwlalimu kuwaficha watoto kichakani maana yake walikuwa wanafanya kitu kilichokinyume cha ratiba na taratibu za shule
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,925
  Trophy Points: 280
  Duh!

  Hao ni wanafunzi ama misukule?

  Bongo kazi kweli kweli.

  Hivi tatizo ni nani hapo?
   
 10. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mbona baba wa Taifa alikuwa analia,je watotot wa Taifa wasilime?
   
 11. M Mahona

  M Mahona Senior Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni walime tu! Wakati mwingine wanalipwa kidogo na ndio maisha yao hayo
   
 12. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Shule zote zilibidi ziwe na mashamba kama hayo kusudi wanafunzi wasome kwa vitendo somo la kilimo ,isitoshe Kilimo ndo Uti wa Mgongo wa Uchumi wa Taifa.KILIMO KWANZA.
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hivi mbunge na madiwani wanafanya kazi gani,yaani uozo huo kaja ugundua Mwanri ambaye amepita mara moja tu ilihali mbunge na madiwani wapo hapo muda wote au ndio wako bize na vikao ili wapate allowance ya kuhudhuria vikao,eti sasa mbunge ndio anatema cheche ,alikwina?
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ati nchi masikini wakati viongozi wanavinjari na magari lukuki bila tija yoyote.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  hawa leo hawakuandamana/?
   
Loading...