Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemvamia na kuumua kwa kumpiga risasi na kisha kutokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu chochote Fredrick Richald mwalimu wa shule ya sekondari Kihenya iliyopo katika kijiji cha Herushingo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati akiwa amekaa na familia yake nyumbani.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi wa Polisi James Manyama amesema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo jeshi hilo limefanya uchunguzi na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye hakutajwa jina lake anayedaiwa kuhusika na tukio hilo huku wengine wakiendelea kutafutwa.
Aidha Kamanda Manyama amesema tayari mwili wa mwalimu huyo umefanyiwa vipimo na umesafirishwa kwenda mkoani Shinyanga kwa hatua za mazishi.
ITV