Mwalimu avamiwa akiwa na familia yake Kasulu, auawa kwa risasi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,556
2,000
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemvamia na kuumua kwa kumpiga risasi na kisha kutokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu chochote Fredrick Richald mwalimu wa shule ya sekondari Kihenya iliyopo katika kijiji cha Herushingo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati akiwa amekaa na familia yake nyumbani.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi wa Polisi James Manyama amesema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo jeshi hilo limefanya uchunguzi na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye hakutajwa jina lake anayedaiwa kuhusika na tukio hilo huku wengine wakiendelea kutafutwa.

Aidha Kamanda Manyama amesema tayari mwili wa mwalimu huyo umefanyiwa vipimo na umesafirishwa kwenda mkoani Shinyanga kwa hatua za mazishi.

ITV
 

Abuu abdurahman

JF-Expert Member
May 9, 2017
970
1,000
Nadhani sio sahihi kuwaita hao wavamizi kuwa ni "MAJAMBAZI" wakati hawakuchukua/hawakuiba chochote baada ya kusababisha mauwaji..

HONGERA KWA MAKAMANDA WA POLISI KWA KUWA MAKINI NA KAZI YAO

MUNGU AIPE MAPUMZIKO MEMA ROHO YA MAREHEMU


Siro anatakiwa ahakikishe USALAMA wa raia na mali zao, Sio kirahisi rahisi roho zinatolewa kama hivyo na wauwaji kuońdoka kilaini namna hiyo.. Badala yake yeye anakodolea macho wapinzani tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom