Mwalimu atimuliwa kazi kwa kuongea Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu atimuliwa kazi kwa kuongea Kiswahili

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MCHONGANISHI, Aug 3, 2012.

 1. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="align: center"]Mwalimu Daniel Urioh.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.


  Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya kazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na sheria.

  Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.

  Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania?

  Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika.

  Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.

  Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumia viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea kishahili na wanafunzi.

  Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
  Kwanza kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya waajiri.
  Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.

  Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza kuzifanya.

  Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania.

  Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.

  Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.

  Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737
  Chanzo: www.kajunason.blogspot.com
   
 2. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kulingana na Employment and Labour Relation Act No. 6 2004, inapinga manyanyaso ya aina yoyote. so kwa ushauri wangu, hebu awaone wanasheria ili suala hilo lifikishwe kwa CMA then haki itendeke.

  Hata kama hutarudishwa kazini, lakini kwa ushauri wa kisheria unaweza kulipwa pesa ya kutosha tu.

  Ni bora kutekeleza hili mapema usijekuambiwa muda wa kufuatilia haki yako umepita.

  Jikaze kaka, upo ktk kipindi cha mpito.
   
 3. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  watz ni wavivu sana, sherehe za kitaifa zinasaidia nini kwenye ufanisi wa kazi? Ndo maana kila siku zinapendekezwa sherehe mpya ili kutegea kazi. Inabidi uanzishwe utaratibu wa kulipwa kwa masaa unayofanya kazi, hii italeta discipline ya muda. Aafu kama ni english medium kwa nini uongee kiswahili? Kwani sheria za nchi zinalazimisha kuongea kiswahili? Mambo ya kupigana picha siwezi ulizia, this is new to me. Shule inajitangaza kwa kuuza picha za weusi!!
   
 4. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kaka usitetee kile usichokijua,inamaana hauelewi wala kuamini kuhusu huu uonevu? Kuna mambo mengi ya ajabu yanayotendeka kwenye sekta binafsi,kama hujui tembea uone. Hata kama ni english medium,kuongea kiswahili sio dhambi.
   
 5. WENYELE

  WENYELE JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,172
  Likes Received: 757
  Trophy Points: 280
  Kumbe hii shule nayo ni hamna? Ila nasikia kikwete alienda pale akatimuatimua watu...
   
 6. allan clement

  allan clement JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2014
  Joined: Aug 14, 2013
  Messages: 1,622
  Likes Received: 1,136
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kujaza mkataba si umekubali "terms and condition" kila shule imeweka sheria zake...ni kweli lugha ya kingereza ni tatizo...kajifunzeni lugha acheni uchonganishi.
   
 7. Hoshea

  Hoshea JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2014
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 3,837
  Likes Received: 1,541
  Trophy Points: 280
  Pole teacher, hao wanaimba hata wimbo wa taifa kweli? Tanzania Tanzania?
  Me naona peleka hayo maandishi kwenye mashirika yanotetea haki za wafanyakazi watakusaidia, haipaswi kuwa hivyo.
   
 8. Slim5

  Slim5 JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2014
  Joined: Jan 7, 2014
  Messages: 15,639
  Likes Received: 12,625
  Trophy Points: 280
  Made in Tanzania
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2014
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Hayo ni baada ya kufukuzwa kazi? kabla alikuwa wapi hajayaleta?

  Hivi picha za Waafrika zinauzika nje? hebu tupe maujanja. Hii ni sababu bogus kabisa ambayo sijapata kusikia ila leo.

  Sasa na hicho kicheko kwenye picha huwa sauti inatoka? au uliambiwa "smile" ukaona unaambiwa ucheke?

  Huu ni usogo wa kufukuzwa kazi, hakuna zaidi.

  Katafute kazi shule ambazo, hazipigi picha, zinakwenda kwenye sikukuu zote za Kitaifa na ambazo haziongei Kiingereza, huko hapakufai.

  Huu ni ufataani usio na mfano.
   
 10. m

  mahalathetz Member

  #10
  Dec 3, 2014
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 36
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama lugha unawaonea kabisaaaaaa,hata huku kwetu shuleni kila darasa linakibao kimeandukwa " speak english"
  Na kila ofisi imeandikwa" no english no service"
  Sasa hao wamekosea nini? Kuhusu kupigwa picha sasa unataka serikali ije imwambie asipige na wakati muhusika ni wewe?
  Hafu wa tz tunaingoza kwa ujinga hata tusome vip!!!!!

  Huwezi niambia et mwl mwenye sifa kabisa anavunja sheria za shule na za inch makusudi hafu anabwabwaja et ni uzalendo mfano :- unatumia kiswahili kama lugha ya mawsiliano na mwanafunzi huku ukijua kabisaaa ni kosa kubwa kuanzia shuleni mpaka serikalini

  Wewe unashindwa kuelewa mitiahani yenyewe haipimi uzalendo wa mtanzania bali hupimwa amesoma nini? Na tena kwa kiingereza mdau
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2014
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Hii ID ya mleta mada MCHONGANISHI inanifanya niamini kuwa huu ni uchonganishi na ufataani.
   
 12. M

  Mapya Yaja JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2014
  Joined: Feb 8, 2013
  Messages: 546
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 80
  Sera mbovu ya lugha Tanzania itaendelea kutufanya takataka mbele ya mataifa mengi. Kwakweli watanzania hatuuziki katika soko la ajira kwa sababu ya English.
   
 13. K

  KVM JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2014
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Eti wanauza picha za Waafrika na wanapata pesa nyingi sana. Mambo ya ajabu haya. Kwa nini wakuu wetu wa nchi hawajachangamkia biashara kama hiyo? Tanzania ingekuwa nchi tajiti sana!

  Kila shule ina masharti yake jinsi ya kuwafanya wanafunzi wafahamu lugha, iwe kiswahili au kiingereza. Sioni tatizo kabisa. Kama kuna mwalimu hajui kiingereza na sharti ni kujua kiingereza aachie ngazi.
   
 14. P

  Princely Member

  #14
  Dec 5, 2014
  Joined: Oct 30, 2014
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu naona tatizo lipo kwako unavuja sheria za shule makusudi then unakuja kulalamika hapa,kwaizo shule utafukuzwa sana ushauri wangu huku kwa kinass unaeza ukamalza mwez hujaingia darasan na hakuna wa kukuulza!
   
 15. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2014
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,211
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280

  Ili kulindaa imani ya wazazi wenye watoto kwenye shule hii dhidi ya tuhuma hizi. Mods ninaombi kama kuna namna shule hii ikapata taarifa ya uwepo wa hii tuhuma nao wakaleta utetezi /maelezo itawasaidia wazazi na hata jamii kutokujenga taswira hatarishi . Maana vyombo vyetu vya usimamizi Nchi hii vingine viko likizo siku nyingi.

  Cc. Invisible
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Madam Mwajuma

  Madam Mwajuma Verified User

  #16
  Dec 6, 2014
  Joined: Sep 13, 2014
  Messages: 6,238
  Likes Received: 4,281
  Trophy Points: 280

  nafikiri hamjamuelewa mleta mada. kuna sehemu kaandika shule ilianzishwa kusaidia wasiojiweza kama ilivyo kwa shule nyingi za private. ndio maana huchukua picha za wazazi na wanafunzi wanazipeleka ughaibuni kuwaonyesha wafadhili watu wanaowasaidia kumbe sivyo.

  unakuta watoto wanalipa ada lakini wanalazimishwa kuleta picha za wazazi ziwekwe kama wanasaidiwa
   
 17. K

  KVM JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2014
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Mleta mada anaonyesha kabisa kuwa hizo picha ndizo zinazoleta pesa hapo shuleni. Shule yeyote inayofadhiliwa ni lazima ionyeshe ni nini kinaendelea hapo shuleni. Sidhani kuwa kinachopelekwa kwa wafadhili ni picha za watoto na familia zao tu bali ripoti ya maendeleo ya shule ikiwemo ufaulu, majengo, michezo, n.k. Hata hivyo hajasema hao wanafunzi wanalipa karo kiasi gani katika hiyo shule.
   
 18. K

  KING 2GB Member

  #18
  Dec 7, 2014
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  noma sanaaa
   
 19. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2014
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Ni kweli yametokea na mwalimu ashaanza maisha kwingine, ila huu uzi umesaidia kumekuwa na changes kibao ktk policy na utawala.
   
 20. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2014
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Hii Ilikuwa back 2012 na lilishafanyiwa kazi, nenda kaone changes... Sasa wamebaki wanafunzi wanao deserve tu YAANI watoto maskini wenye akili.... Na management mpya ipo
   
Loading...