Mwalimu asakwa kwa kumtia mimba bintiye

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi nchini, linamsaka mwalimu wa Shule ya Msingi Ziwani, Haule Karudijina, kwa kosa la kumbaka na kumtia mimba binti yake wa miaka 15.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Steven Buyuya, alisema kuwa taarifa za mimba ya binti huyo aliyemaliza darasa la saba mwaka huu shuleni hapo ziligundulika baada ya kuchukuliwa vipimo mbalimbali kutokana na homa za mara kwa mara zilizokuwa zikimwandama.

Hata hivyo Kamanda Buyuya alisema, katika vipimo hivyo, ilibainika kwamba mwanafunzi huyo alitiwa mimba na baba yake mzazi.

Alisema, mama wa kambo wa mwanafunzi huyo alisaidia kumbana binti huyo ambaye alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba yake mzazi ingawa ilichukua muda kwa mwanafunzi huyo kusema ukweli hadi alipoelezwa kwamba angepelekwa polisi.

Kwa mujibu wa binti huyo, baba yake alitengana na mama yake mzazi kisha kumwoa mwanamke mwingine na kwamba uhusiano na baba yake ulianza Julai, mwaka huu, wakati mama yake wa kambo alipokuwa safarini.

“Huyu mwanafunzi alitueleza kwamba baba yake alikuwa akirudi kutoka kilabuni akiwa amelewa anaingia chumbani kwa binti yake huyo sasa… alisema wakati wanafanya hivyo, mama yake wa kambo alikuwa safarini,” alisema kamanda huyo na kuongeza kwamba baba yake alitishia kumuua endapo angepiga kelele.
 
Huyo mwalimu ana njaa gani??? ngale gani unamalizia kwa mwanao?????? Dunia ipo mwishoni hii....
 
quote, " vipimo vinaonyesha kuwa amepewa mimba na baba yake mzazi" jamani ni vipimo gani hivyo? naona mwandishi kaongeza chumvi hapo
 
Kwa kweli inasikitisha! Ni tamaa, pepo au ni mambo ya kishirikina? Mbona vilabuni wanawake ni wengi mno? We mwalimu ulaaniwe!
 
Dunia inahitaji maombezi... Ni ngumu kuamini hii. Yaani baba unamfunua nguo bintiyo, afu unamfanyia foreplay, then unammega? kweliiii
 
Back
Top Bottom