Mwalimu Aozeshwa Maiti ya Mkewe kabla ya Kuzikwa: hii imetokea Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Aozeshwa Maiti ya Mkewe kabla ya Kuzikwa: hii imetokea Iringa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gagurito, Jun 16, 2011.

 1. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ukistaajabu ya Mussa...ya firauni! Ni jambo la ajabu bt ndio ukweli wenyewe huo na imetokea Iringa, mpaka niandikapo thread hii nipo iringa na hili ndio gumzo la mtaani.. Mume, mwalimu wa shule ya msingi ya hapa iringa mjini amezuiwa kuzika, maiti ya mkewe ikafukuliwa na ndugu za mkewe wakiongezwa baba mkwe wake na kusababisha marehemu kuzikwa usiku kwa kutumia taa za chemli, karabai, tochi na mishumaa kisa mwalimu (mume wa marehemu) hakumalizia kulipa mahali. Hali hii ikasababisha wananchi waombolezaji kuchangia pesa kumlipa baba mkwe ili mwili wa marehemu uzikwe, baba mkwe kapokea na akaonekana akinywa pombe kwa furaha na rafiki zake. Kwa maoni ya mume (mwalimu) anasema mahali alilipa yote toka miaka ya 90 na ameishi ya marehemu kwa takriban miaka 20 pasipo matatizo yoyote ukweni! WanaJF hii stori niyakweli na imetokea hv karibuni hapa iringa.. Sijui unalichukuliaje swala hili? Hebu tujadili..
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  marehemu alizikwa saa 3 usiku. Je huu ni utu? Ubinadamu wetu ukoje?
   
Loading...