TANZIA Mwalimu Alex Kashasha, mchambuzi nguli wa Soka afariki dunia

A ball in the space, a man in the space a ball in the net!

Style yake ya uchambuzi wa soka la ndani(Bongo) ilikua inaburudisha saana sana. Hakua mtu wa jazba wala hasira na alichangamana vizuri na vijana aliowapita umri kwa mbali sana kiasi cha kua kama ni watoto wake na wote akiwaheshimu

Poleni sana ndugu, familia, marafiki na TBC
 
Kuanzia 2019 nchi imepoteza vichwa vingi! Yani kuanzia kwa Ruge, Kibonde, Mengi,....... mpaka kwa Kashasha!

Mola awalaze mahali pema peponi ameen!
 

Mchambuzi nguli wa habari ya michezo maarufu kama mwalimu Kashasha amefariki dunia hivi punde alipokuwa amelazwa hospitali ya Kairuki.

Chanzo mimi mwenyewe niko eneo la tukio.

----
Mchambuzi nguli wa soka nchini Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha amefariki dunia leo Agosti 19, 2021 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki Jijini Dar es Salaam.

Mwalimu Kashasha alizaliwa mwaka 1957, mpaka umauti unamkuta alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC).

Mwalimu kashasha alikuwa mwalimu wa michezo katika vyuo mbalimbali na baadae akawa mchambuzi wa soka katika television ya taifa .

Mwalimu kashasha alikuwa anasikika katika kipindi cha michezo cha TBC FM.
R.I.P Mwalimu
 
Back
Top Bottom