Mwalimu akutwa kalala uchi kwenye kibao cha shule

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
345
100
Mwalimu mmoja katika shule ya msingi katika kijiji cha Lukukwe huko Lindi, amekutwa asubuhi akiwa amelala kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama. Katika kuhojiwa amesema aliingia ndani kwake vizuri na kufunga mlango, ameshangaa sana asubuhi mlinzi wa shule anamuamsha na yeye kujikuta yupo nje na akiwa uchi wa mnyama. Hii imeleta hofu kubwa kwa walimu wenzake na inaonekana amani shuleni hapo imetoweka.
Wadau hii imekaaje?

Source: TBC1
 
hii isije ikawa kama story za huko Ukerewe......ukitandika mtoto wa watu unashangaa wakati unaoga mamba anakuibukia kwenye beseni.....eti nyie wakerewe....ni kweli haya.....?
 
Ngoja Mkandara aje hapa akujibu. Siyo kwenye beseni tu. Usiku wa manane unajisikia kutokwa jasho la ajabu na unajisikia lazima ya kwenda ziwani kuoga. Kumbe mamba anakusubiria pale. Lakini si Ukerewe tu. Tanga je? Nasikia ukipiga kifuu cha nazi teke kinakusemesha: nimekukosea ni?
 
Wewe Preta Beseni mbona kubwa hivyo, hadi kwenye glasi ya maji unashangaa mamba huyo na wewe kiulaini unabebwa.
 
hii isije ikawa kama story za huko Ukerewe......ukitandika mtoto wa watu unashangaa wakati unaoga mamba anakuibukia kwenye beseni.....eti nyie wakerewe....ni kweli haya.....?
Duh!..hii hadithi imesimama!..lol!

Haya mambo yapo jamani kwa walimu ulizeni watu Mbozi na Sumbawanga kuna visa kama hivi kibao tu kwa walimu,kwa hyo mi natoa pole kwa mwalimu na wala si usanii kama wengine wanavyodai hapa
 
Ngoja Mkandara aje hapa akujibu. Siyo kwenye beseni tu. Usiku wa manane unajisikia kutokwa jasho la ajabu na unajisikia lazima ya kwenda ziwani kuoga. Kumbe mamba anakusubiria pale. Lakini si Ukerewe tu. Tanga je? Nasikia ukipiga kifuu cha nazi teke kinakusemesha: nimekukosea ni?

hiyo ya Tanga hata mimi nimewahi kusikia....tena kifuu kikikuuliza ukijifanya mkaidi.....basi mbele unakuta umezungukwa na bahari huna pa kutokea....duh.....Mkandara hebu kuja sawazisha mambo hapa.....
 
Mwalimu mmoja katika shule ya msingi katika kijiji cha Lukukwe huko Lindi, amekutwa asubuhi akiwa amelala kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama. Katika kuhojiwa amesema aliingia ndani kwake vizuri na kufunga mlango, ameshangaa sana asubuhi mlinzi wa shule anamuamsha na yeye kujikuta yupo nje na akiwa uchi wa mnyama. Hii imeleta hofu kubwa kwa walimu wenzake na inaonekana amani shuleni hapo imetoweka.
Wadau hii imekaaje?

Source: TBC1

Mambo yao kusini ndiyo haya , kisha wanlalama walimu awaendi. Ni vizuri kweli wanafunzi waone nyeti zako. Heshima itatoka wapi. Pambafu. Heri mie mkulima
 
huyu ni msanii anataka kuhama kwa urahisi
Ndugu yangu Tanzania ni kubwa sana na si hiyo unayoifahamu wewe ya kuishi mijini tu. mkielezwa yanayowatokea wenzenu mnabisha lakini hampo tayari kwenda kuvaa uhusika katika eneo husika ili kuhakikisha kama yapo au la
 
Natamani hao wanga wamfanyie jk wa pili, anamka asubuhi anajikuta yupo feri.
 
Natamani hao wanga wamfanyie jk wa pili, anamka asubuhi anajikuta yupo feri.[/QUO

Askari aliowaacha sheikh Yahya bado wapo imara!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom