Mwalimu akatwakatwa mapanga na kupoteza mkono wake mmoja. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu akatwakatwa mapanga na kupoteza mkono wake mmoja.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Skype, Jul 8, 2012.

 1. S

  Skype JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwalimu mmoja wa shule ya msingi digodigo jana alikatwakatwa mapanga akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake.

  Tukio hili limetokea jana majira ya saa 5 asubuhi ambapo mwalimu huyo wa kiume alivamiwa ghafla na kijana wa kimasai kisha kuanza kumshambulia kwa mapanga hadi kumfyeka mkono.

  Chanzo cha kijana huyo kufanya mashambulizi inasemekana ni mambo ya mapenzi, yaani inasemekana kua mwalimu huyo alikua akimchukua mke wa kijana huyo wa kimasai.

  Mara baada ya tukio, mwalimu huyo alipelekwa kituo cha afya kilichopo kijiji cha digodigo jirani na kijiji cha samunge.

  Kwa taarifa za uhakika ni kwamba matibabu yalishindikana ikabidi apelekwe hospitali ya wilaya ya Ngorongoro iliyopo eneo liitwalo Wasso jirani na Loliondo. Pamoja na juhudi zote za madaktari kuokoa maisha ya mwalimu imebidi leo mchana mnamo saa 8 apelekwe Arusha mjini ambapo anatarajia kufika saa5 usiku wa leo tarehe 8 July, 2012.

  Updates zaidi tusubiri walioko Arusha kuanzia kesho ila tukio ni la kusikitisha na mpaka sasa mtuhumiwa bado hajakamatwa.

  Nawasilisha hoja kwa masikitiko makubwa kwa maana mwalimu huyu kafanyiwa kitendo cha kikatili yaani kukatwa mapanga, kufyekwa mkono mpaka ukadondoka, kuumizwa vibaya, n.k.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Na ule mkono wa Simbawacheee je uko wapi? :redface: Mke wa mtu mtamu hana hata gharama siona ona wakina Nchemba na Simba wavyogombani wake za watu
   
 3. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  huyu c mmasai,nachojua wamasai hawana mawivu ya mapenzi,kushea wives hakunaga noma kbsaaa
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kumbe alikuwa mzinzi shauri yake
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,844
  Trophy Points: 280
  muke ya muntu ni sumu...........................
   
 6. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  Na mume ya mutu wanasema ni masiwa ati..ha haa haa,ni utani tu!
   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,844
  Trophy Points: 280
  ni masiwa kweli.................
   
Loading...