Mambo muhimu yatakayokufanya udumu kwenye ajira
1. Kamwe usile miwa ya shule (usitembee na wanafunzi). Miwa ya shule ni mitamu ila nakuasa usijaribu kwa usalama wako.
2. Usihoji kila kitu kwa mkuu wa shule hasa MAPATO na MATUMIZI. Wakuu hawapendi watu wanaohoji.
3. Kopa kwa kiasi. Baada ya mwaka kuanza kazi mtaruhusiwa kukopa benki. Kopa benki epuka taasisi kama FAIDIKA, FANIKIWA,RICHMOND,ATLASMARA na nyinginezo.
4. Kazi ya ualimu haina posho yeyote wala over time hata ukeshe hadi SAA nane usiku unafundisha. Posho pekee anayopata mwalimu ni usimamizi wa mitihani ya NECTA kwa mwaka mara moja.Hivyo tafuta kipato nje ya ajira.
5. Fundisha kwa kiasi usijitese sana maana ukifaulisha sifa ni za mkuu wa shule na sio za kwako ila ukifelisha lawama ni za kwako.
6. Usiingie kwenye makundi ofisini wala usipeleke umbea kwa mkuu wako epuka kutumika
7. Kumbuka kujiendeleza elimu haina mwisho.
8.Mwisho lakini sio kwa umuhimu acha siasa ofisini hasa kama wewe ni mpinzani. Tunasema hakuna ubaguzi kwa nje ila kwa ndani fursa nyingi zitakupita kuna ubaguzi mkubwa sana.
KAZI NJEMA