Mwalimu ajinyonga mpaka kufa...hatari!!

mind ur business

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
416
414
MWALIMU wa Shule ya Msingi Ikongolo Kata ya Ikongolo Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kitenge cha mkewe. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Barnabas Mwakalukwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alitaja jina la mwalimu aliyejinyonga kuwa ni Basil Sungu (38). Alieleza kuwa tukio hilo ni la Desemba 31 mwaka jana katika Shule ya Msingi Ikongolo. Mwili wa mtu huyo ulikutwa katika chumba chake anacholala na mkewe, Theresia Ali (35) ukiwa umening’inia kwenye dari.

Alisema upelelezi wa chanzo cha tukio hilo unaendelea, lakini uchunguzi wa awali unaonesha kulikuwa na mgogoro wa kifamilia kati yake na mkewe huyo, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mbiti.

Katika tukio jingine, Mwakalukwa alisema kuwa mjasiriamali, James Albert (22), mkazi wa Kata ya Chemchem katika Manispaa ya Tabora, amekutwa amejinyonga kwa kujitundika kwenye kenchi sebuleni kwake kwa kutumia mkanda wa begi.

Alisema tukio hilo ni la Desemba 31, mwaka jana Mtaa wa Juhudi Kata ya Chemchem. Chanzo cha tukio hilo hakijafahamika na upelelezi unaendelea. Kamanda Mwakalukwa alibainisha kuwa vitendo vya watu kujinyonga, havifurahishi na vinaleta simanzi, hasa ikizingatiwa kuwa mhusika ni mwanandoa. Kwamba hali hiyo huwapa shida sana watoto, mke au mume anayebaki.

“Kuanza sasa tutaanza kuwasaka wale wote wanaosababisha wenzao kujinyonga ili sheria ichukue mkondo wake, hatuwezi kuwaacha hivi hivi, wanasababisha simanzi kubwa kwa familia zao,” alisema.

Aliongeza kuwa kuanza sasa wakipata taarifa yoyote, kwamba mtu fulani anataka kujinyonga, atakamatwa kabla hajatekeleza azma yake. Alishauri wanaotaka kujinyonga, waende kwenye madawati ya jinsia, watoe taarifa za wanaowasumbua ili wakamatwe.

Alitoa mwito kwa viongozi wa dini, kukemea tabia za namna hiyo kwenye nyumba za ibada, ili kuepusha usumbufu kwa watoto na familia, pale wanandoa wanapojinyonga.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao viongozi wa dini wanaotarajiwa kutoa mafundisho ya kiroho kuepusha haya ndio hao ambao sasa hawajali tena na wanachokiangalia sana na sadaka,, michango ya harambee na kuwauzia waumini tu vitu twa hovyo wakiwaambia kuwa vina upako,,
 
Back
Top Bottom