Mwalimu aingia matatani baada ya kumwita mwanafunzi msichana wakati ni mvulana


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,092
Likes
4,037
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,092 4,037 280
male-teacher-cartoon.jpg

MWALIMU Joshua Sutcliffe wa Oxfordshire, Uingereza, ameingia matatani baada ya kusimamishwa kazi kwa kumwita kwa ‘bahati mbaya’ mwanafunzi wa kiume kuwa ni msichana.

“Nilimwita mvulana mwenye umbile la kike kuwa ni msichana, na sasa niko hatarini kufukuzwa kazi,” alisema mwalimu huyo wa hisabati.

Mwalimu huyo anadaiwa kusema “asanteni sana wasichana” kwa wavulana hao alipowaona wakiendelea kwa makini na masomo yao. Kumbe mmoja wa wanafunzi hao, ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu maalum, alikuwa ni mvulana mwenye sura na umbile la kike ambaye wakati wa kuzaliwa kwake sehemu zake za siri ziliwatatanisha wazazi na madaktari hadi kufikia kuamua kwamba alikuwa ni mvulana.

Inasemekana mwalimu huyo aliwaomba msamaha wavulana hao, lakini baada ya mvulana huyo kulifikisha kwa wazazi wake, wao waliamua kulivalia njunga na kulifikisha kwenye mamlaka maalum ambako mwalimu huyo aliitwa kwenda kujieleza kutokana na madai ya ‘kutusi kwa kutumia jinsia”.

Mwalimu huyo anayepata mshahara wa Paundi 30,000 kwa mwaka (sawa na Sh. milioni 90) hivi sasa amechanganyikiwa kwani ualimu ndiyo kazi yake kuu tangu zamani.

Wazazi wa mwanafunzi huyo wamesema mwalimu huyo alikuwa anamwonea mwanao kwani alibidi kukijua kitu hicho tangu zamani alipojiunga katika shule hiyo.

Muungwana
 
Maxmizer

Maxmizer

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2017
Messages
3,504
Likes
2,953
Points
280
Maxmizer

Maxmizer

JF-Expert Member
Joined May 22, 2017
3,504 2,953 280
Dunia hii haiishi vituko
 

Forum statistics

Threads 1,215,487
Members 463,205
Posts 28,550,339