Mwalimu afundisha peke yake la kwanza hadi la 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu afundisha peke yake la kwanza hadi la 7

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 19, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWALIMU wa Shule ya Msingi Pemba, Edmund Kadudu iliyopo katika Kijiji cha Pemba, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, ameelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi wapatao 1,000 anaolazimika kuwafundisha kwa zamu kuanzia darasa la kwanza hadi
  saba.

  Mwalimu huyo ameomba msaada kutoka Halmashauri ya Wilaya hiyo kuweza kuongezewa walimu wengine ili kukabiliana na tatizo hilo lililodumu kwa zaidi ya miaka minne, imeelezwa.

  Wilaya ya Mvomero kama zilivyo wilaya nyingine, inakabiliwa na changamoto kubwa ya
  uhaba wa walimu wa shule za Sekondari na wale wa Shule ya Msingi zilizopo maeneo ya pembezoni na mazingira duni ya kufanya kazi.

  Hali hiyo ya uhaba wa walimu imejitokeza kwenye Shule ya Msingi hiyo iliyopo katika Kijiji
  cha Pemba, Tarafa ya Turiani, Wilayani humo, kufuatia kuwa na walimu wawili pekee wanaolazimika kufundisha kwa zamu zaidi ya wanafunzi 1,000 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.

  Mbali na uhaba huo, alisema wanafunzi 42 wamefanikiwa kufaulu katika mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu, licha ya kujitokeza kwa hali hiyo kutokana na wanafunzi hao kuwa na vipaji vyao vya ziada katika masomo.

  Mwandishi wa habari hizi, aliyetembelea shule hiyo hivi karibuni alijionea mazingira
  duni yanayoikabili , ikiwa ni pamoja na baadhi ya majengo ya madarasa yaliyojengwa miaka
  mingi kutokamilishwa na hivyo kulazimika wanafunzi kubanana kwenye madarasa
  machache yaliyopo shuleni hapo.

  Kwa mujibu wa mwalimu huyo, kuwa shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 1,000 inakabiliwa
  na uhaba mkubwa wa walimu ambapo kwa muhula ujao wa masomo huenda akaendelea
  kufundisha pekee kutokana na mwalimu mkuu wa shule kuonyesha mazingira ya kutaka kuhama.

  Alisema hali hiyo itajitokeza kutokana na Mwalimu Mkuu (jina tunalo) kumweleza kuwa
  amepata uhamisho wa kwenda kufundisha shule moja ya msingi iliyopo mkoani Tanga.

  “Tunalo tatizo la uhaba wa walimu …na si uhaba tu , shule haina walimu , tulikuwa walimu
  wawili kwa maana Mwalimu Mkuu, lakini amesema kuwa amepata uhamisho wa kwenda
  Mkoa wa Tanga, hivyo muhula wa masomo utakapofunguliwa nitabakia pekee yangu,” alisema mwalimu huyo.Hata hivyo aliongeza kusema”

  …Mwalimu Mkuu alikuwa akifundisha mara moja moja na kuondoka, hivyo kwa muda wa
  miaka minne nipo pekee yangu kuwafundisha wanafunzi, “alisisitiza Mwalimu huyo.

  Akizungumza kwa huzuni na masikitiko makubwa, Mwalimu huyo alisema kuwa amekuwa
  akifundisha kwa zamu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kwamba kutokana na wingi wa wanafunzi kazi ya ufundishaji imekuwa ngumu kwake.

  Kwa mujibu wa Mwalimu huyo, kuwa darasa la pili lina wanafunzi 250 na wengine 600 ni
  wa madarasa ya tatu hadi sita, ambapo wataongezeka wengine wa darasa la kwanza mwakani
  na kufikisha idadi ya 950.

  “Tatizo hapa ni uhaba wa walimu , wanafunzi wanavyo vipaji na wa kupata walimu wa kutosha shule inatoa wanafunzi wengi wa kuingia kidato cha kwanza,“ alisema Mwalimu
  huyo.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Pemba, katika Kata hiyo, Mariam Kolowela, alikiri shule hiyo kubakiwa na mwalimu mmoja baada ya mwenzake ambaye ni Mwalimu Mkuu kudai kupata uhamisho.

  Hata hivyo alisema kutokana na uhaba wa walimu katika shule hiyo, Uongozi wa Serikali
  ya Kijiji katika maazimio yake uliamua kuandika barua rasmi kwenda kwa Ofisa Elimu wa
  Wilaya anayeshughulikia Shule za Msingi juu ya kuomba kupatiwa walimu zaidi.

  “Serikali ya Kijiji hiki inafahamu kuwa shule ina Mwalimu mmoja wa kudumu, anafundisha
  wanafunzi 700 …lakini kwa sasa wamefikia 1,000,” alisema Mwenyekiti wa Serikali
  ya Kijiji hicho.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, kuwa tatizo la upungufu wa walimu,
  wamelifikisha katika uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ili Shule hiyo ipatiwe walimu
  wengine zaidi kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora.

  Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Wilaya ya Mvomero (Msingi), Euphrasia Buchumu,
  akizungumzia suala hilo, alisema kuwa shule nyingi zilizopo pembezoni na maeneo yenye
  mazingira duni katika Wilaya hiyo zinakabiriwa na uhaba mkubwa wa walimu.

  Pamoja na hali hiyo, alisema kuwa tayari Ofisi yake imeomba Ikama ya kuwezesha ya kuweza
  kuwahamisha baadhi ya walimu kutoka shule nyingine na kuwapeleka kwenye shule hizo
  za pembezoni na zilizopo katika mazingira duni kabla ya kufunguliwa kwa shule hizo muhula
  ujao wa masomo.

  Akizungumzia vyumba vya madarasa, alisema kuwa tayari Ofisi yake ilifanya zoezi la ukaguzi
  katika shule zote za Msingi kuanzia mwaka 2003 hadi kufikia 2005 , ambapo ulibaini
  kuwa madarasa mengi yaliyoanzwa kujenga hayajamaliziwa.

  Kwa mujibu wa Ofisa Elimu huyo wa Wilaya, kuwa jambo hilo limechangiwa kwa kiasi
  kikubwa na wananchi kushindwa kuchangia nguvu kazi zao licha ya Serikali kutoa fedha za
  ujenzi katika baadhi ya Shule zilizopo vijijini.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yaani hawa ndiyo walitakiwa wape mishahara ya millions na siyo wanao sinzia bungeni tu lakini utakuta mshahara wake TZS 200,000
   
 3. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nampa pole mwalimu, naomba asichoke kuwasaidia watoto wa wanyonge. Pamoja na hayo serikali kushindwa kuboresha mazingira ya pembezoni ndo sababu kubwa ya kukosa walimu! unakuta sehemu zingine hata zile huduma za msingi hazipatikani kwa hiyo inakuwa ngumu kwa walimu kuishi,
  Mfano mzuri ni wenyewe serikali makao makuu ni Dodoma lakini utakuta viongozi wengi wanaishi Dar na pia ofisi nyingi za serikali ziko Dar!
   
 4. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ni pole kwake na kwa wazazi na wananchi wote wa shule hiyo
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Huyu asilipwe overtime bali alipwe na overdose!!! nipeni namba yake nikampige tafu
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Ahaa sisi tunajenga flyovers dar na airport,bandari mpya bagamoyo!watajijuu... elimu na afya bora sio kipaumbele chetu
   
 7. doup

  doup JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  kama ni mimi siku nyingi nimeenda kulima nyanya; taabu gani hiyo na hakuna hata mtu mmoja atakayetambua mchango wa huyo mwalimu kwa taifa hili; huyu anastahili kuitwa "Shujaa wa Taifa". Na usishangae kusikia hata wanakijiji wanamdharau kupita kiasi.
   
 8. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wee umenifanya nicheke pasipo stahili kucheka jamani.
  Mi naona aachane na kuwafundisha kutumia huo mtaala wa wizara. Ajiunge nna wanafunzi wafanye kilimo kwanza. Hakuna cha zamu, wote shamba at once wakimaliza waende home.

  Inasikitisha kwa kweli, na hili si tatizo unique kwa mvomero tu.
  Kweli hili ni taifa la wajinga!
   
Loading...