Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Aug 4, 2012.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini nawawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwawatoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfanoninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio chawafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwana kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.

  Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedhakuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara nakulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwamfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani chafedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu patona matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyopicha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihalifamilia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidini pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanyakazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizokuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume nasheria.

  Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wamuafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedhazisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendovisivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa pichailihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwakazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalishakiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwakufukuzwa.

  Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchibila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume nasheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenyenafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungubasi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shuleimekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima nakutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maishakujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia sikuza mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuzasheria za nchi yetu Tanzania?

  Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumiziya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibukwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hatakufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa nikuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchiusiovumilika.

  Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimilimkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kamaawa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenyeshida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.

  Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu waowa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumiaviongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharauna kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyeshauzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kuteteasheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lughaya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa lakuongea kishahili na wanafunzi.

  Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
  Kwanza kupandisha mshahara na mazingira yakazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwani manyanyaso ya waajiri.
  Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali piamfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwabinafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.

  Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wamapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shidaza watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watuwasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendowanaweza kuzifanya.

  Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchinikuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu zakitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwamanufaa ya Tanzania.

  Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi yakufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.

  Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kuteteanchi yangu Tanzania.

  Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga:+255 755 379 737

  Chanzo:HABARI NA MATUKIO: MWALIMU AFUKUZWA KAZI KWA KUONGEA "KISWAHILI" - ARUSHA
   
 2. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Kama mkataba na Mwajiri wake ni kuongea Ung'eng'e maeneo ya shule akiuvunja anategemea nini?
   
 3. kiagata

  kiagata Senior Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duah,pole sana kwa yaliyokupata.
  Kazi ni ajira,chakula,heshima na msaada kwa anayeifanya.Kuipoteza kwa vyovyote inauma na kupteza hayo hapo juu na zaidi.
  Sasa kwa ushauri,nenda Mahakamani kwenye mahakama ya kazi na utapata msaada kwa watu waliokerwa na tabia ya kufukuzwa watu hovyo hovyo bila kufuata taratibu.Ingawa shule za Internatinal,English mediam na hizi zote za st.st......... lugha(english) ndio msingi unaotofautisha shule za kina Kayumba na zao.
  Pole sana.
   
 4. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mnaabudu wazungu halafu mnakuja kulalamika hapa tuwasaidie nini? Endeleeni kuwaabudu!
   
 5. M

  MI6 Senior Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  pole sana...

  Usisahau kudai chako mapemaaaa....
   
 6. D

  DR. RICHARD Senior Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama kunamkataba wa kazi unaosema mwl. atafukuzwa kazi akiongea kiswahili na wanafunzi (siyokufundisha) ndani ya tanzania lazima tu utakuwa batili kwani kiswahili ni lugha ya taifa na kama kakosea kuna kutoa onyo, hao wawekezaji kama elimu ni liingereza basi wakaweke huko kwa waingeleza, haliwezi likawa taifa linalopuuza lugha yake ya taifa.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Very sad ila sasa huyu kaanza kuongea lugha hii kuanzia lini hadi afukuzwe mara hii ? Na mikataba ya aina hii ndani ya Tanzania inakuwaje ?
   
 8. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  jaman 2msaidie huyu jamaa kisheria
   
 9. r

  rwazi JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ymimi sioni sababu ya kujua wafafhili wanatoa kiasi gani kwani eakati unaingia hapo ulirnda kuomba kaxi sasa unataka kujua eafadhili wanatoa kiasi gani hiyosiyo kazi yako wewe dai kilicho chako qtu
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  wewe umenena vyema.....hawa wazungu wanataka kutushika nyeti sasa.....
   
 11. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Pole sana kweli ni kituko.Mikasa kama hii inatoka Afrika tuu.Ila ndio hivyo waafrika tumezidi kudharau lugha zetu this in cludes nyinyi waalimu.Natumaini hilo ni fundisho.
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  pole ndugu,mahakama zinamlinda mwenye nacho sijui utapataje haki yako
   
 13. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  duu inategemea na makubaliano anaonekana alionywa sana akawa anajisahau! ila vp kuhusu st kayumba kakosa kabisaa!
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kama mkataba alioingia nao unamkataza kuzungumza kiswahili maeneo ya kazini shughuli ipo!
  Labda pa kuanzia ni kumfukuza mzungu aliye implement kanuni ya kukataza kuzungumza kiswahili!
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..wa-Tz tuhakikishe tunajifunza Kiingereza kwa juhudi zote.

  ..Kiswahili hakiwezi kutufikisha mbali, that is the reality.
   
 16. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  shule nyingi, after lol wewe unavyeti vyako, huyo hakupi kiinua mgongo wewe, jiajiri na safari hii fungua biashara zako
   
 17. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Yani acha tu! Halafu Mi hawa wasungu wananitia kichefuchefu sasa!

  Lakini haya yote ni ccm ndio wametusababishia!
   
 18. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  hembu iandike hiyo kwa ung'eng'e tukuone
   
 19. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  wanataka watushike sehemu za siri tuendelee? wew vipi bana
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Issue siyo kutokujua kuzungumza kiingereza. Issue ni kuzungumza kiswahili kwenye eneo la kazi!
   
Loading...