Mwalimu adaiwa kuua akimgombea 'Baa Medi'

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWALIMU wa shule ya Msingi Mtwivilla mjini Iringa, Alexander Kapolesya, anadaiwa kumuua mwalimu mwenzake, Ernest Komba (48), wa shule hiyo hiyo wakati wakimgombea mhudumu wa baa (Bar Maid).

Walimu hao walikuwa wakigombea penzi la mwanamke huyo aliyekuwa akiwahudumia kwenye moja ya sehemu zinazouza vinywaji katika eneo hilo la Mtwivilla.

Inadaiwa kwamba, mwalimu Komba alikufa baada ya Kapolesya kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa na jirani na eneo la tukio, walimu hao waligombana jana saa 2.30 usiku katika baa hiyo.

Habari kutoka katika eneo la tukio zinadai kuwa, wakati walimu hao wakinywa pombe kila mmoja kwa wakati wake alikuwa akiongea na mwanamke huyo ili aondoke naye kwa ajili ya kwenda kufanya ngono.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, amemtaja mwalimu Komba kuwa ndiye aliyempiga mwenzake hadi kufa.

Mangalla amesema, baada ya tukio hilo, Mwalimu Kapolesya alijaribu kukimbilia mafichoni lakini polisi walibaini alipokuwa wakamkamata.

“Alidhani angeweza kutoroka, lakini hakufanikiwa kwani alikamatwa muda mfupi baadaye katika maficho yake aliyoyafanya huko huko Mtwivilla,” amesema Kamanda Mangalla.

Amesema, wakati uchunguzi unaendelea, mwalimu huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.

Kamanda Mangalla amesema,jina la mwanamke aliyesababisha walimu hao wagombane halijapatikana, hajulikani alipo, polisi wanamtafuta.
 
Wanamtafutia nini? yeye anakosa gani? au na polisi wanataka kuona huyo bar maid ana utamu gani hadi walimu na elimu zao wanatoana roho? hivi huyo bar maid ni kbila gani vile wataalamu kiasi hicho? Pole Marehemu na wafiwa wote ukifika mpe hi MC Lema na wengine waliokufa katika hali kama hio.
 
Asomaye na afahamu!
Na kwa mtini jifunzeni!
Bra PJ na Biblical verse, nzuri na mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie na mwenye kukaidi haya afungiwe jiwe kuu na kutoswa katikati ya kina cha bahari
 
Walimu wa siku ni tofauti kweli! Ona sasa na wanafunzi waweje? Hawa ndo wanaokula watoto wetu huko wakiwadanganyia kuwapa visheti
 
Kuna wale walimu walikamatwa wakisagana darasani marekani.....je hao? Hii ni issue ya kawaida ktk jamii.
 
MWALIMU wa shule ya Msingi Mtwivilla mjini Iringa, Alexander Kapolesya, anadaiwa kumuua mwalimu mwenzake, Ernest Komba (48), wa shule hiyo hiyo wakati wakimgombea mhudumu wa baa (Bar Maid).

Walimu hao walikuwa wakigombea penzi la mwanamke huyo aliyekuwa akiwahudumia kwenye moja ya sehemu zinazouza vinywaji katika eneo hilo la Mtwivilla.

Inadaiwa kwamba, mwalimu Komba alikufa baada ya Kapolesya kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa na jirani na eneo la tukio, walimu hao waligombana jana saa 2.30 usiku katika baa hiyo.

Habari kutoka katika eneo la tukio zinadai kuwa, wakati walimu hao wakinywa pombe kila mmoja kwa wakati wake alikuwa akiongea na mwanamke huyo ili aondoke naye kwa ajili ya kwenda kufanya ngono.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, amemtaja mwalimu Komba kuwa ndiye aliyempiga mwenzake hadi kufa.

Mangalla amesema, baada ya tukio hilo, Mwalimu Kapolesya alijaribu kukimbilia mafichoni lakini polisi walibaini alipokuwa wakamkamata.

“Alidhani angeweza kutoroka, lakini hakufanikiwa kwani alikamatwa muda mfupi baadaye katika maficho yake aliyoyafanya huko huko Mtwivilla,” amesema Kamanda Mangalla.

Amesema, wakati uchunguzi unaendelea, mwalimu huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.

Kamanda Mangalla amesema,jina la mwanamke aliyesababisha walimu hao wagombane halijapatikana, hajulikani alipo, polisi wanamtafuta.

Next level jamani na ninyi huko mupo!!
 
Back
Top Bottom