Mwalimu adaiwa kumpa mimba mtoto wa mwalimu mwenzake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Mwalimu wa shule ya Sekondari Lugulu iliyopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu, mwenye umri wa miaka 17 na kisha kutokomea kusikojulikana.

Mei 27 mwaka huu shule hiyo iliwapima wanafunzi wote wa kike ujauzito na mwanafunzi huyo alibainika kuwa na ujauzito wa miezi wa sita.

Akizungumza na Mwananchi juzi, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Nduga Makenji alisema baada ya mwanafunzi huyo kubainika kuwa na ujauzito walimhoji na alimtaja mwalimu kuhusika na ujauzito huo.

“Mei 27 kama ilivyo kawaida ya kupima wanafunzi ujauzito wakati wa kufunga shule, mwanafunzi huyu alibainika kuwa na ujauzito wa miezi sita, tulimhoji aliyehusika na ujauzito wake ambapo alimtaja mwalimu (jina linahifadhiwa) kuhusika na ujauzito huo.

“Tulimweleza mzazi wake ambaye tulikuwa tukishirikiana naye, baada ya mwalimu anayetajwa kuhusika na ujauzito kupata taarifa hizi alikimbia na mpaka sasa hatujampata.

Nimeripoti suala hili katika mamlaka husika ili washughulike na jambo hili,” alisema mwalimu Makenji.

Alisema tukio hilo lililofanywa na mwalimu huyo ni tukio baya na kwamba halipaswi kutokea kwenye jamii na kufanywa na watu ambao wameaminiwa na jamii.

Akizungumzia tukio hilo, mzazi wa mwanafunzi huyo ambaye ni mwalimu katika shule hiyo, Charles Elimsaada alisema taarifa za mwanawe kupewa ujauzito na mwalimu mwenzake zimemshtua na kumuumiza, kwani hakutarajia kusikia taarifa kama hizo.

“Mei 27 nilipigiwa simu na Makamu Mkuu wa shule akiniambia wametoka kuwapima wanafunzi ujauzito, lakini mwanangu ambaye yuko kidato cha tatu amekutwa na ujauzito wa miezi sita.

Kwa kweli niliumia, ilibidi nimhoji tena mwenyewe akanieleza aliyempa ujauzito ni mwalimu,” alisema Elimsaada Mwalimu Elimsaada alisema kuwa aliamua kujiridhisha kwa kwenda kumpima tena mwanawe na kubaini kuwa ni kweli alikuwa na ujauzito.

“Ili kujiridhisha na taarifa hizi nilimpeleka mtoto kituo cha afya Ndungu, amepimwa na kweli akaonekana ana ujauzito wa miezi sita, baada ya hapo ikabidi niondoke na mwanangu maana nipo masomoni kwa sasa, tumefanya jitihada za kumkamata mwalimu huyo lakini hatujafanikiwa. Naziomba mamlaka husika zichukue hatua dhidi ya mwalimu huyu maana tayari ameshaharibu ndoto za mwanangu,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Same, Annastazia Tutuba alisema amezipata taarifa hizo na endapo mwalimu huyo akibainika kuhusika na jambo hiloatachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Tutamtafuta na kufuata taratibu za kiutumishi, tutamfungulia mashtaka ya kinidhamu baada ya kupata ushahidi kutoka vyombo husika,” alisema Tutuba. M,B

Chanzo: Mwananchi
 
Pale kati bwana utam wake ni adimu..

Ukiwa unaupata au kuutafuta akili huwa inaruka

Side effects huja baadae
 
Nimecheka ingawa kwa kweli nimeumia mno kwa maelezo ya baba mzazi. Virtually he was totally frastrated. Anaonekana alikuwa ana marajio makubwa na moto wake, masikini!

Hivi jamani nini dawa ya kadhia hii? Mbona miaka 30 jela ni mingi mno lakini inaonekana sio solution?
 
Back
Top Bottom