Mwaliko wa ubarikio

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
Familia ya Bwana na Bibi Tutor B wa jijini Mwanza wanayo furaha kuungana nawe Mwana JF katika sherehe ya mtoto wao mpendwa Akanganyila B kupata kipaimara.
Sherehe hizo zitafanyika siku ya Jumapili tarehe 16/12/2012 katika kanisa la KKT Igoma na baadaye kwenye tafrija fupi itakayofanyika ndani ya viwanja vya VATCAN VILLAGE Igoma Mwanza.
Wote mnakaribishwa. (Serrious)
Kwa maelekezo zaidi waweza kuni-PM ili tupeane maelekezo ya kina.
 
kwa sababu ni Tutor B.......naweza kwenda......weka savannah na Windhoek za kutosha.......

Umekuja vyema; bora umesema mapema utatumia nini; huku Mwanza tunapendelea bia inaitwa Senetor;
Vinywaji ni vya kutosha; karibuni sana!
 
Kwani Kipaimara ni graduation ya kuhitimu mafunzo ya ulevi??
Mi nilidhani unampelekea dogo ma Biblia na vitabu vya kiroho, kumbe we unataka ukaweke upako wa kipepo mchafu

Wenye upako watajulikana hapa! Duh! mbavu zangu! teh teh .....
 
Ndio hili daladala jipya? Nasikia watu wanapanda na kuku ndani kwenye passengers cabin.
Mwingine anavua viatu, miguuu inatema uvunde ile mbaya.

Kuku wapi wewe! mi naona mandoo ya samaki ndo mengi.
 
Kwani Kipaimara ni graduation ya kuhitimu mafunzo ya ulevi??
Mi nilidhani unampelekea dogo ma Biblia na vitabu vya kiroho, kumbe we unataka ukaweke upako wa kipepo mchafu

he he...hebu nipishe huko.....pepo ukikutana nae utamjua......?
 
Mmh, ubarikio nao unaandaa ukumbi??
Ukasherehekee na Biya?

Maono yangu ya sherehe za kiroho ni za kizee sana

Hongera!

Hata ndoa ni sherehe ya kiroho! bia ni kitu cha kawaida tu kwa watu wazima - kwa watoto ndo hairuhusiwi.

VATCAN VILLAGE sio ukumbi - ni uwanja wa wazi wenye vibanda vibanda na mziki wa mbali; hakuna vurugu wala fujo; msiogope kuja ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom