Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano kuhusu hali ya Elimu nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano kuhusu hali ya Elimu nchini

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by neemarug, Nov 21, 2011.

 1. n

  neemarug New Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Katika kuadhimisha miaka hamsini (50) ya Uhuru wa Tanzania Bara, Umoja wa Wanafunzi Walimu (UDSTA) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la HakiElimu wameandaa kongamano kuhusu hali ya elimu nchini. Kongamano hili litajadili maendeleo na changamoto katika Sekta ya Elimu tangu nchi yetu ilipopata uhuru. Kongamano hili litafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 kuanzia saa 4.00 asubuhi katika Ukumbi wa Yombo 4, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wazungumzaji wakuu katika Kongamano hili watakuwa Ndugu Jackson Makweta, Waziri wa zamani wa Elimu, na Profesa Justinian Galabawa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Ukiwa mdau muhimu wa maendeleo ya elimu na ya kijamii hapa nchini, unaombwa kuhudhuria kongamano hili wewe mwenyewe pamoja na viongozi wenzako. Aidha, unaombwa kwa nafasi yako uhamasishe wadau wengine katika taasisi yako, taasisi zingine, pamoja na wananchi kwa ujumla kuhudhuria kongamano hili muhimu.Tafadhali wasiliana nasi kwa ufafanuzi zaidi.
  Simu ya mezani; 255 22 2151892/3, simu za mkononi: +255 655/784 283 163
  Barua pepe: media@hakielimu.orgTunatanguliza shukrani zetu kwa kukubali mwaliko huu.Wasalaam,
  Annastazia Rugaba
  Idara ya Habari
   
Loading...