MWALE WA DEMOKRASIA/ The Flame of Democracy!

LENGEJU BOB

Member
Nov 1, 2010
53
29
The Flame of Democracy
MWALE WA DEMOKRASIA: Ndani ya Raia Tanzania
Na. Robert Victor Lengeju

Mwale wa Demokrasia ni Jukwaa Maalumu katika Gazeti la Raia Tanzania (Gazeti dada la Raia Mwema), linazoletwa kwenu na Mchambuzi na Rafiki yako, Rai wa Tanzania, Robert Victor Lengeju.Jina la jukwaa limechaguliwa na mwandishi kwa sababu mahsusi kabisa. Ni mfululizo wa makala zenye falsafa moja, yenye kuibua, kutafsiri na kuchokoza maswali na hoja zinazogusa maisha ya watu katika dhana pana ya Demokrasia. Ni katika MWALE WA DEMOKRASIA pekee, ambako ukweli unazungumzwa kwa rangi yake! Propaganda zinakemewa mchana kweupe na Elimu ya uraia inatolewa bure juu ya haki na wajibu, wa watu na viongozi. Tunahimiza uwajibikaji wa watumishi wa umma, tunahamasisha wananchi kuamka na kudai uwajibikaji huo, huku na wao pia wakitimiza wajibu wao, kwa nafasi zao.

Falsafa kuu ya mwandishi ni Dhana ya Demokrasia kama Rasilimali. Kwamba Demokrasia ndiyo rasilimali mama katika kubadilisha maisha ya watu kutoka katika ujinga, umaskini na maradhi; na wala hakuna njia ya mkato kuelekea huko, Kama tunahitaji maendeleo, ni lazima tuheshimu na kuhimiza ukuaji wa demokrasia.Ungana nami katika MWALE WA DEMOKRASIA, kila Alhamisi, Ndani ya Raia Tanzania Pekee.

Kwa kuanzia, Soma Toleo la leo, tarehe 5/12/2013...ukurasa wa 19 Mkala iliyoboreshwa "HATUA ZABA MUHIMU KWA UPONYAJI WA CHADEMA"....
 
Back
Top Bottom