Kwa muda mrefu sasa tokea Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, abadili uongozi mzima wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), huduma za bandari zimekua zikizidi kuzorota kwa kasi na yeye na wenzake kukanusha kuhusu kuzorota huko.
Siku zilivyozidi kwenda Dk. Mwakyembe na wenzake wakaanza kudai sasa wanahujumiwa. Swali la kujiuliza wanahujumiwa na nani wakati watu wanaoona hawafai wote wameondoka na walimo kazini ndio wanaowaamini.
Mbali ya watendaji wameondoa hata bodi yote na kuunda mpya, sasa kama kuna mtumishi anayewahujumu kwanini wasimchukulie hatua?
Mwakyembe akiwa makini atabaini kwamba tatizo sio hujuma bali ni uwezo mdogo na usio na tija wa watu aliowakabidhi LANGO KUU LA UCHUMI yaani bandari yetu ambayo pia ni lango kuu la USALAMA na kuna ushahidi mwingi kuhusu hillo.
Mwakyembe asiogope kugeuka jiwe maana amefanikiwa kusafisha na kuboresha sekta nyingi ndani ya wizara yake na kila mpenda maendeleo anaamini waziri hana nia mbaya bali anaangushwa na watu alioamini kuwa wana uwezo na watamsaidia kwa hiyo si kosa lake hata kidogo. Tumewahi kuona maamuzi ya bodi ya NBC kumuondoa CEO wake Mr. Mafuru na baada ya kubaini hana tatizo na kama lipo halifanani na uwezo wake walimrudisha kazini na Mwakyembe ajue hata kama kuna mapungufu kwa uongozi aliouondoa, bado uwezo wao na mema yao yanameza hayo mapungufu yao na vyema akawarudisha kuokoa bandari yetu.
Hebu sasa fikirieni, CEO anayekaimu TPA, Madeni Kipande anavyoshindwa hata kuwasiliana na gazeti la serikali kwa kutoa majibu ya kitoto na hata alipokutana na wenye meli, badala ya kuongea lugha ya kibiashara na mwenye mali na mteja, yeye aliwatisha na kuonyesha ubabe uso maana na sasa ameandika barua ya kuomba kazi bila hata kuonyesha umakini wowote.
Kipande akawaelekeza wasaidizi wake kuandika barua kwa Kiswahili kwenda kwa makampuni ya meli duniani kabla ya kulalamikia ndio akaandika nyingine ya Kiingereza, na zote zikiwa hazikidhi kuwango cha barua ya mtu mwenye kuwasiliana na wateja wa Kimataifa (naambatanisha musome).
Naambatanisha pia barua na mawasiliano ya wenye meli na TPA na wenzao wa Kenya muone jinsi wenzake wanavyochukua hatua si kufanya siasa katika uchumi.
Tuliwahi kutahadharisha humu ndani kwamba issue hapa siyo idadi ya vifaa *ulivyo navyo TPA ila ni management makini ya kupanga na kusimamia hivyo vifaa vifanye kazi vizuri na kufanya turn round ya meli iwe ya kuridhisha kuliko ilivyo sasa.
Hatua ya Waziri Mwakyembe kuuondoa uongozi wote wa Bandari imewasikitisha wadau na watumiaji wakubwa wa Bandari kwa kile kinachoonekana ni kutotilia maanani athari zinazoweza kutokea kutokana na maamuzi hayo.
Kwa sasa bandarini hakuna anayefanya maamuzi ya kiutendaji kutokana na nafasi ninakaimiwa na walioshika nafasi za waliondolewa kutokuwa na sifa stahili za kuongoza bandari. Wadau walianza kumshangaa Waziri Mwakyembe pale alipoanza kukosoa ufanisi kwenye Mamlaka ya bandari alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani mara tu alipoteuliwa kuwa Waziri.
Kwenye mkutano huo aliuambia umma kuwa anajua kuna madudu na malalamiko mengi ya wizi huko TPA na angevamia huko kuondoa. Hapa wadau waliona kama vile alikuwa anawafurahisha waliokuwa wanamsikiliza kwa sababu alikuwa mno mgeni kwa jinsi bandari invyofanya kazi na process nzima ya utoaji mzigo bandarini ilivyo ikiwa ni pamoja na kuwafahamu wadau halisi wanaohusika katika process hiyo.
Wadau walifurahia sana kwa kuteuliwa kwake wakiamini kwamba angekuwa na tofauti na mtangulizi wake Mh Nundu ambaye kwa kipindi chote cha mwaka mmoja na nusu alichokaa hakuwahi kukutana na wadau wowote wa bandari zaidi ya kuwaita wachache offissini kwake aliowaona pengine wangemsaidia kumbe wengi wao walikuwa ni kwa maslahi yao na siyo kwa port&shipping industry nzima.
Mfano halisi ni ule wa wadau kushauri TPA kujenga a "car terminal facility" kama ilivyo kwenye bandari nyingine . Hii ilitokana na shehena ya magari kuonekana kukua mwaka hadi mwaka toka mwaka 2008 na sehemu za uegeshaji wa magari hayo bandarini kuonekana kuwa finyu kutokana na shehena ya macontainers kuongezeka kwa kiasi cha asilimia 12-15 kila mwaka kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano iliyopita.
Pamoja na wadau kushauri kuwa kuwe na private icds nje ya bandari zinazomilikiwa na watu binafsi, bado Tpa kuwa na terminal yake ya kupokelea na kuhifadhi magari kabla hayajachukuliwa kwenda kwenye icds za watu binafsi au moja kwa moja kwa wateja ilikuwa ni muhimu kwa sababu si rahisi magari yaondolewe moja kwa moja baada ya kushushwa kwenye meli kutokana na "logistics" za kutolea. Magari kutolewa usiku tu kutokana na folleni ya magari barabarani mpaka kwenye maeneo ya private icds za kupokelea magari hayo.
Cha kushangaza pamoja na ushauri wa muda mrefu wa wadau, Waziri Nundu aliuzikiliza upande mmoja wa mdau aliyekwenda kwake kumshauri asitishe mradi wa " multistorey car terminal"kwa kuwa ana ICD yake na hatimaye akamshauri mh Rais na mradi ukasitishwa. Leo hii private icds zinachukuwa 50% tu ya magari yanayoshuka kwenye meli kitu ambacho kinafanya maeneo mengi muhimu bandarini ambayo yangetumika kwa kuweka containers yawekwe magari yayozagaa kila pembe.
Wadau wanasema kitendo cha Waziri Mwakyembe kuweka hadharani mbele ya wanahabari kwamba kuna matatizo makubwa ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na wizi wa mali za wateja hakikuwa makini na kwa kiasi kikubwa kimetoa signal mbaya kwa wateja wa ndani na nje wanaotumia bandari ya Dar es salaam. Waziri kwa kuweka matatizo lukuki yasiyothibitishwa hadharani kibiashara ni kauli isiyojenga na badala yake inaweza kukimbiza wateja na kuwapa faida bandari zunazoshindana na sisi Kama Mombasa, Nacala, Beira, Maputo , Durban nk. Taarifa zile zilikuwa zitolewe kwenye vikao vya ndani kwa wahusika na wanahabari wapewe taarifa zinazotoa matumaini ya kutumia bandari zetu pamoja na changamoto zilizoko ambazo sisi kama wadau tunaona zimeshashughulikiwa kwa kiasi cha kutia matumaini.
Wadau wanamkumbuka Waziri Shukuru Kawambwa ambaye kwenye miaka ile ya 2008/9 wakati kulikuwa na msongamano mkubwa wa meli na mizigo bandarini ambao haukuwahi kutokea , alishirikisha wadau na kwa pamoja wadau pamoja na wizara husika wakikwenda kuonana na Mh Rais ambapo kwa pamoja tuliyaainisha matatizo yaliyokuwa yanakabili bandari ikiwa ni pamoja na kipengele kilichokuwa kwenye mkataba wa Ticts na Serikali kilichokuwa kinakipa Ticts ukiritimba wa kuhudumia meli zote za macontainers zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam hata kama kwa wakati huo watakuwa wamezidiwa!! Huu ulikuwa mkataba wa ajabu na wa kifisadi uliosababisha hasara kubwa na wateja wengi wa nchi za jirani walikimbia bandari hii.
Mh. Rais kwa maneno yake mwenyewe baada ya kusikiliza hoja za wadau wote waliokuwepo kwenye kiako hicho alisema matatizo mengi ya bandari mnaweza kuyatatua nyie wadau wenyewe kwa pamoja. Tokea hapo ndipo ikaundwa kamati ya kushughulikia msongamano huo mkubwa iliyoitwa " port congestion committee" iliyojumuisha Wajumbe kutoka kwenye taasisi zote zinazohusika katika utoaji na upakiaji wa mizigo bandarini ambao ni TPA,TICTS,TASAA,TAFFA,TAZARA,TRL,TRA,SUMATRA, OIL MARTETING ASSOCIATION,PORT IMMIGRATION OFFICIALS, PORT HEALTH OFFICIALS, TBS,MARINE POLICE, ICD OPERATORS, EMPTY CONTAINER DEPOT OPERATORS, REPRESENTATIVE FROM MINISTRY OF TRANSPORT,NK.
Kila taasisi ilitakiwa kuwa na Wajumbe at least wawili na mwenyekiti wa kamati alikuwa Katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi na wakati hayupo ni Mkurugenzi mkuu wa bandari. Kamati hii ilifanya kazi kubwa na msongamano ule ukapata jawabu na matatizo kupungua kwa kiasi kikubwa. Baada ya lile tatizo kubwa kupungua kamati iliona ni vema tukabadilisha jina badala ya kuwa port congestion committee tukaona iitwe PORT IMPROVEMENT COMMITTEE ili badala ya kushughulikia swala la congestion ya meli na mizigo peke yake iwe inaangalia maswala ya ufanisi katika bandari kwa kina na kitaalam zaidi.
Wadau wanaona tusipoangalia tutarudi kule kule tulipokuwa tena kwa speed ya ajabu kutokana na wanasiasa wanavyoparamia swala la uendeshaji wa bandari. Mwakyembe ajaribu kufuata nyayo kama za *mwenzake Shukuru Kawambwa ambaye alihakikisha hata Bodi ya wakurugenzi ya bandari iliyoingia mwaka 2010 anaweka mchanganyiko wa wadau wenye utalaam na mambo ya bandari ili matatizo kama yaliyojitokeza huko nyuma yasijitokeze tena.
Kwa upande mwingine wadau wanaona Waziri Mwakyembe hangekuwa na haja ya kwenda bandarini kukumbizana na uondoaji wa mafuta machafu yanayobaki bandarini kwenye mabomba baada ya meli za mafuta kushusha mafuta yake badala yake kama kuna mteja amepeleka malalamiko offisini kwake angetakiwa alete swala hilo kwenye "port improvement committee" ili lipate ufumbuzi wa kitaalaam zaidi.
Wadau wa mafuta kwa kutumia chama chao cha " Tanzania oil importers marketing Association bado wanasisitiza kuwa mafuta Waziri Mwakyembe anayodai kuyakamata yeye na driver wake ni mafuta machafu ambayo kihalali ni mali ya waagizaji wa mafuta na huwa wanayaacha bandarini ili yachukuliwe kwa utaratibu maalum pasipo kuharibu mazingira. Kwa sheria za kimataifa za maritime safety and security hayatakiwi kumwagwa baharini .
Pia wadau wanashangaa kumsikia Waziri kuueleza umma kuwa kuna ufanisi mmbovu na uozo bandarini wakati ni mwaka jana tu Rais Kikwete alipotembelea bandarini alisifu juhudi zilizofanywa na wadau mbali mbali wa bandari wa kuhakikisha hali ya ufanisi inarudi kwa kiasi cha kuridhisha. Matatizo ya meli za mafuta zilizokuwa zinazagaa nje yaliisha, bandari ikaongeza uwezo wa kupakuwa na kupakia meli nyingi za containers baada ya Ticts kuondolewa ukiritimba wa kuhudumia meli zote za containers kiasi kwamba hivi sasa karibu asilimia 40%ya meli za containers zinahudumiwa upande wa Tpa na kuiacha Ticts na asilimia 60 tu. Yote haya ni juhudi za Wadau wote *chini ya " Port Improvement Committee".
Wadau wanaona tatizo kubwa lililopo kwenye " Maritime Transport Logistic network" kwa kiasi kikubwa yako kwenye upande wa Reli yaani TAZARA na TRL. Hapa Waziri kama anataka kufanikiwa hapaswi kulala usingizi kwa sababu hivi ndivyo viungo muhimu vinavyoongeza ufanisi kwenye bandari yoyote duniani.
Waziri akae na wadau na wataalam mbalimbali wanaifahamu vizuri sector hii muhimu kwenye uchumi wa nchi yoyote iliyojaliwa kuwa na bandari ili wamshauri priorities zake za kuanzia kazi katika wizara hii la sivyo atakuwa anakimbizana na vitu vidogo vidogo ambavyo havileti tija zaidi ya kuchafua taswira nzima ya bandari na wadau wake wanaoitegemea.
Sasa matatizo yanatokea Mwakyembe anasema anahujumiwa, nani anayemhjumu? Asiwe kama mbuni kutia kichwa kwenye mchanga na kusahau mwili nje unaungua na moto.