MWAKYEMBE, SITTA , TIBAIJUKA, etc KUWENI WAJASIRI, WAZAELENDO NA MFANO KWA HILI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MWAKYEMBE, SITTA , TIBAIJUKA, etc KUWENI WAJASIRI, WAZAELENDO NA MFANO KWA HILI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zing, Mar 8, 2011.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kama mwakyembe aliweza kuvaa magwanda na kusimamia ukweli na haki kwenye ile tume hawezi kushindwa hili.

  Sitta naye Alijipatia sifa kem kem kwa bunge lake kwa msemo wa speed and standard.

  Sasa ninawawahsuri hawa tunaowaita wapiganaji na watu wao w akribu.

  • Waagize/ waamrishe kuwa watafutiwe Vitara au Mark II za kutumia kiofisi na si GX an VX kama ilivyo sasa
  Naamini ni kama kweli ni wazelendo kutumia vitara au Mark II haiwezi kuathiri utendaji wao wala sio kwamba ni demotion.

  Kwa kufanya hivi wataonyesha wao kuwa wana tofauti na "wenzao" wengine. Na wengine wataona aibu na kuanza kuiga..

  Hapa nimemuongelea sitta na mwakyembe lakini na majina tunimeyatumia kufikisha ujumbe kwa baraza lote la mawaziri.

  Nashangaa hata mtu kama Prof Tibaijuka naye anasubiri kumabiwa kuwa sasa mawaziri wasitumie VX wakiwa dar. Kiongozi kama prof tibaijuka mwakeyembe watanzania tulitegemea wawe hatua moja mbele na kumshtua Rais JK.

  from masaki to posta why VX?

  Hivi maamuzi ya gari gani waziri atumie si ni maamuzi ya waziri.Au ni ni standard UWT na ikulu. kuwa waziri ni lazima atembelee VX hata anapokuwa Dar?
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu mama Tibaijuka nimemuona kama vile anatumia gari moja aina ya FORD; unless simfahamu vizuri lakini siku za kwanza za uteuzi wake alikuwa na gari la aina hiyo na sio shangingi LAND CRUISER V8 kama hao majasusi wengine!!
   
 3. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ahaaaaa ebu ngoja nimfuatilie it will be a good news
   
 4. F

  Fataki Senior Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama ulimwona mwanamke mmoja anatembelea FORD, basi hakuwa Tibaijuka maana gari yake ya ofisi ni VX. Tulishajadiliana huko nyuma kuwa magari hayo hata kama ni ya anasa yanavumilia kila aina ya barabara na vipindi virefu. Mpe Magufuli/Mwakyembe Suzuki, wapuyange toka Tunduma kwenda Laela, Sumbawanga, Kasanga (Lake Tanganyika), Kizi, Mpanda, Kigoma, Tunduru, Lindi n.k., utanunua Suziki mpya kila baada ya miezi sita na wanaume hao wataishia kunyooshwa migongo Muhimbili kila safari. Tuwe na mashangingi machache kwa kila wizara na kwa safari ndefu kama hizo ila Makatibu Wakuu wanaoshinda maofisini na Wakurugenzi wao, Wakurugenzi wa Halmashauri, Ma-DC n.k. wote tuwape Hardtop au Landrover, zinawatosha!
   
 5. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,534
  Likes Received: 2,115
  Trophy Points: 280
  Wana-JF
  Huko mikoani mawaziri wanafuata nini kila siku wakati kuna Ma-RC, Ma-DC, Ma-DED na mabaraza ya halmashauri(madiwani)??????

  • Mimi natoa pendekezo kuwa mawaziri wabaki ofisini wakitengeneza sera bora za kitaifa wakitumia saloon cars za bei nafuu kabisa na waende mikoani tu wakiongozana na Mh. Raisi au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu wakienda kukagua miradi mikubwa inayoratibiwa na wizara husika. Na hapa Rais lazima awe na ratiba maalumu ya kukagua miradi mikubwa tu mikoani, miradi mingine wakuu wa mikoa/wilaya/halmashauri waisimamie huko mikoani.
  • Hivyo kila safari ya Rais mikoani kufungua mradi mkubwa waziri atakuwa anapanda ndege pamoja na Raisi kama vile Raisi afanyavyo ziara za nje ya nchi (akiongozana na mawaziri husika) na kupunguza ununuzi wa mashangingi VX n.k
  • Kama kutatokea dharura ya kweli kabisa basi Waziri aende ktk 'pool ya magari machache ya VX n.k' kupatiwa gari aina ya shangingi kwenda safari ya mikoani/wilayani/kijijini na akirudi DSM gari linaenda kufungiwa gereji ya pool ya ma-VX hayo machache mpaka safari nyingine ikizuka.
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  land cruiser ni cheap halafu ni imara kwa maan zinatumika sana serikalini ia wanapewa maafisa wa chini,..yanamudu barabara za aina zote..ufisadi tu
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kazi ngumu hiyo ndugu yangu, nani asiyependa starehe? mtoto wa mkulima alilalama lakini wapi msafara wake migari zaidi ya 20.
   
Loading...