Mwakyembe: Serikali kuanzisha chuo cha wahudumu wa ndege; warembo kupewa kipaumbele!

GIB

JF-Expert Member
Mar 2, 2012
336
92
Wakati wa kuwakilisha Makisio ya bajeti yake, Waziri Mwakyembe amesema wanatarajia kuanzisha chuo cha wahudumu wa ndege. Ila chuo hicho kitatoa upendeleo kwa warembo hasa wale walioshiriki u-miss.

Sasa kwa wale wenye sura za kutisha hata mtoto akikuona analia sijui watasaidiwaje kupata nafasi hizo? Au watumie mikorogo?

Nawasilisha

GIB
 
Alikuwa na sura nzuri ila walipotaka kumnanihii basi tena. hatasura yake haitambuliki vizuri
 
Wakati wa kuwakilisha Makisiyo ya bageti yake , amesema wanatarajia kuanzisha chuo cha wahudumu wa ndege. ila kitatoa upendeleo kwa warembo. hasa wale walioshiriki u miss. sasa kwa wale wenye sura za kutisha hata mtoto akikuona analia sijui watasaidwaje kupata nafasi hizo. au watumie mikorogo?

Nawasilisha

GIB

Wewe ni Mtanzania?? Kiswahili ni lugha ya ngapi kwako?? Ukiandika post isome kwanza halafu rejea matumizi ya nukta na koma maana inatulazimu kutumia nguvu nyingi sana kukuelewa.
 
Wakati wa kuwakilisha Makisio ya bajeti yake, Waziri Mwakyembe amesema wanatarajia kuanzisha chuo cha wahudumu wa ndege. Ila chuo hicho kitatoa upendeleo kwa warembo hasa wale walioshiriki u-miss.

Sasa kwa wale wenye sura za kutisha hata mtoto akikuona analia sijui watasaidiwaje kupata nafasi hizo? Au watumie mikorogo?

Nawasilisha

GIB

Kwa kuhudumia Precision Air au Qatar?
 
Wakishahitimu watafanya kazi wapi? Au ndo watahudumia Precision Air na 540?
 
Wewe ni Mtanzania?? Kiswahili ni lugha ya ngapi kwako?? Ukiandika post isome kwanza halafu rejea matumizi ya nukta na koma maana inatulazimu kutumia nguvu nyingi sana kukuelewa.

Mkirua usipate tabu mambo ya St,kayumba Secondary School hayo,
 
Wewe ni Mtanzania?? Kiswahili ni lugha ya ngapi kwako?? Ukiandika post isome kwanza halafu rejea matumizi ya nukta na koma maana inatulazimu kutumia nguvu nyingi sana kukuelewa.

Nenda kwenye point acha utoto wewe hayo yanahusu nini?
 
Point unaipataje kama alichokiandika hakieleweki??...wewe unaweza kuwakilisha makisio ya bajeti?? mimi sielewi kitu hapo wala sioni pointi hapo.
Hata hivyo kama wewe unaelewa (kwasababu ni kulugha chenu may be ) unaweza kuchangia pia au ndo umechangia hivyo??
 
Huu usanii huu!!! Sasa wakimaliza hizo kozi watafanya kazi wapi?
Ni mtu ngapi zitapata udahili kwa mkupuo mmoja wa hiyo kozi?

Huyu angesema serikali imeagiza ndege 5 mpya,Airbus au Boieng ili kuimarisha shughuli za ATC na hao warembo wao wangewapeleka Kenya au Ethiopia kupata hizo kozi. Kozi hizo ni fupi kama wiki tu.
 
Wakati wa kuwakilisha Makisio ya bajeti yake, Waziri Mwakyembe amesema wanatarajia kuanzisha chuo cha wahudumu wa ndege. Ila chuo hicho kitatoa upendeleo kwa warembo hasa wale walioshiriki u-miss.

Sasa kwa wale wenye sura za kutisha hata mtoto akikuona analia sijui watasaidiwaje kupata nafasi hizo? Au watumie mikorogo?

Nawasilisha

GIB

:biggrin1: afadhali aisee sio tu wawe vimodo bali wawe na vifiga wasituletee vischana havina hata tutako
 
Tanzania tuna ndege chache sana: Precision si zaidi ya 15; Air Tanzania 1; ya mukuu 1. Sasa sijui hao mamia ya wahudumu watafanya kazi wapi!! Labda wangekuwa na uwezo wangeajiriwa kwenye ndege nyingine e.g. Kenya Airways; lakini wahudumu wetu hawako competitive.
 
Point unaipataje kama alichokiandika hakieleweki??...wewe unaweza kuwakilisha makisio ya bajeti?? mimi sielewi kitu hapo wala sioni pointi hapo.
Hata hivyo kama wewe unaelewa (kwasababu ni kulugha chenu may be ) unaweza kuchangia pia au ndo umechangia hivyo??

pole sana.
 
Back
Top Bottom