Mwakyembe,Selelii na Ole Sendeka:Tumeridhika na Hotuba Ya Pinda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe,Selelii na Ole Sendeka:Tumeridhika na Hotuba Ya Pinda!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kevo, Aug 29, 2008.

 1. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Of all the people in the world these great fighters against CORRUPTION had the guts to stand and say wameridhishwa na hatua zilizochukuliwa na SERIKALI maana yake ni kwamba zile BLAH BLAH za PINDA za jana zimewafurahisha sana.
  Nilipokuwa naangalia mahojiano ya ITV na hawa watu kidogo walinishangaza na maneno yao!Hizo hatua mpaka mwenzi wa kumi na moja nazo ni hatua and then mwenzi wa kumi na moja tutaambiwa wanapewa muda wa kufikiriwa adhabu gani wapewe mpaka kikao kingine cha Bunge and then itakuwa sasa mchezo!
  Dr Mwakyembe anasema hotuba ilikuwa makini na hatua za kisheria zimefuatwa ni zipi hizo?Za kuzidi kuwaficha hawa mafisadi?
  Lucas Selelii nao wakadai eti wamefurahishwa ila wakawa na ujasiri wa kuhoji kwa nini wapewe miezi sita?
  Nashindwa kuelewa kama ule moto wa hawa ma fighter umezimwa!
  Dr Slaa naye akajikanganya.kwanza anasema hatua zilizochukuliwa ni madhubuti na zinatia moyo then anasema huwezi kusema umeridhika ama hujaridhika mpaka hatua zitakapochukuliwa!Sasa hapo sijui kama Kiswahili kimenipiga chenga ama vipi?
  Hamad Rashid naye yupo kwenye mkumbo wa walioridhika!
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe ulitaka wasemeje?
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Misimamo yao dhabiti kama na jinsi gani ya kuharakisha hili jambo lipate utatuzi probably before November!November ni mbali sana na wataendelea kulipigia danadana na Politiki kibao!Sasa hivi CCM inafanya juu chini kuwasafisha hawa mafisadi wakubwa ilhali inapaswa wangekuwa wamefilisiwa tayari na kuswekwa ndani!
  JK juzi anasema mafisadi wa EPA wana hali mbaya siku hizi hapa TZ kuendesha 4Matic na Vogue Supercharger ni kuwa na hali mbaya?
  Ni porojo zimejaa ilhali watu wachache wanaponda raha na hamna lilofanywa ilhali ripoti ya Richmond inaonyesha washiriki na vitendo vyao vichafu!
  Pinda anasema eti tumewaconsult wanasheria wakubwa kama akina Mkono,Chenge na Mwanyika jamani hawa si ndio wameshindwa kuishauri serkali kuingia mikataba mizuri ilhali wametudidimiza kwenye umaskini mkubwa zaidi?
  Kuna lipi hapo la kuridhika?
  Ama na wewe upo kwenye hako ka list ka Richmond maana ulivyohoji kwa critique!
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndio gharama ya demokrasia na utawala bora hiyo, stahamili na kuwa mwingi wa subra, sound tayari una hukumu yako. Mambo haya hayaendeshwi kwa jazba na pupa
   
 5. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nakuunga mkono Kevo,

  Hamna jipya hapa,hata mimi nawashanga hawa wakubwa!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Uyu Mwakiyembe si ndio yule juzi mlimuona shujaa aliporopoka kuwatukana Viongozi wa Zanzibar sasa mkiambiwa msizarau mkunga na uzazi ungalipo ,natumai ninaposema huwa na uhakika kuwa mtu huyu ni wa aina ya watu wanaojipendekeza na si wa kweli wa kuweza kutenda haki au kuchagua ipi sawa na ipi ni batili ,hawa ni kama nilivyosema ni wale wanaoweza kuifanya kweli kuonekana uongo na uongo uonekane ni kweli.
  Jamaa anajipendekeza kwa raisi na vilevile anajipendekeza kwa Waziri Mkuu ,huyu si kiongozi shujaa bali ni goigoi anaeogopa kuwakosoa viongozi kwa kuona kufanya hivyo ni kuwadharau viongozi.

  Hivi mlitegemea aseme au akosoe aliyoyasema Pinda ? tatizo lake limewaambukiza wengine wote na kuonekana hakuna anaekwenda kinyume na hotuba ya Pinda.
  Tuchukulie Mheshimiwa Pinda aliyosema yote ni kweli na mazuri yanayofaa na kusubiriwa ,hayo yachukuliwe ni kwa upande wa Chama Tawala lakini upinzani usithubutu kusifu wala kushangilia ,ili uwe ni upinzani wa kweli basi itabidi waipinde hotuba ya PInda na kuifanya ni mbovu .jamani huo ndio upinzani ,sasa ikishakuwa mnaunga mkono fahamuni kuwa hamfai kuitwa upande wa upinzani bungeni wala chama pinzani ,imashakuwa mnaunga na kukubaliana ,sasa kutakuwa na upinzani tena ,na kama mkijidai ni wapinzani basi kwa mimi sitowakubali kuwaona nyinyi ni wapinzani bali mtakuwa mafisadi mnakula fedha ya wananchi na kupokea posho kumbe ni waunga mkono wakubwa wa Chama Tawala.
   
 7. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mi nilisema bongo usanii mwingi watu oooh, aah...

  Mnaona sasa, na bado kuna nyingine iko jikoni.
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana nilikwisga sema Mwakyembe hatufai Watanzania!Yaani kazi nzuri aliyofanya ya Richmond tukamwona ndiyo wetu kabisa kumbe tulikuwa tumepumbazwa tena hata wengine wakahoji kwa nini hakupewa uwaziri kumbe ni mlalahoi tuu hana lolote!
   
 9. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  watu ni wale wale ... ni majina tu ndiyo yanatofautiana .. usishangae kesho wote wakawa ccm damu damu
   
 10. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli sasa umekosa shabaha!Yaani akina Slaa na Hamad waende CCM sijui labda Makamba na Kingunge wakachanjie vijijini kwao kwa mababu zao la sivyo it will never happen ila I regret to say everything is possible under the sun!
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani hapa cha kushangaza ni kipi?
   
 12. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu cha kushangaza hapa ni pale umdhaniye kumbe siye!
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mnawalaumu akina Dr. Mwakyembe, je baada ya ile report ni wangapi tuliwaunga mkono kwa vitendo?

  Wao walishafanya kazi, mlitaka waendeleze haya mapambano peke yao mpaka wapi?

  Kama tunataka mapambano lazima tuwe tayari kuwa mbele kuwaunga mkono wale wenye
  ushujaa japo wa kukabiliana na hao mafisadi.

  Ukiachia watu wa Kyela, nani wengine ambao walionyesha kwa vitendo kuwaunga wajumbe wa kamati ya Mwakyembe?

  Hata wao ni binadamu, wanapoona mafisadi wanaachiwa na kupeta mitaani, tena wanaachiwa na rais na waziri mkuu wake, mlitaka wao waendelee kupigana peke yao mpaka lini?

  Imefika mahali hata wao wameona wacha yaishe na tuendelee mbele. Wa kulaumiwa hapa sio akina Mwakyembe na kamati yake bali sisi wote ambao hatukuwaunga mkono vya kutosha na pia hiyo serikali yetu pamoja na CCM ambao wanatumia vitisho kunyamazisha sauti huru.
   
 14. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tuliwaunga mkono kwa kuwapa moyo thru the media na kuwapongeza kwa kila aina!Ulitaka na tuandamane au?
  Naomba nikuulize Mkuu wewe uliwaungaje mkono?
  Na vilevile kama wataonyesha cheche zao zaidi tutawaunga mkono kwa Kuwarudisha Bungeni!
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa ni watu makini sana, hiyo tumeridhika tuosome vizuri wameridhika na nini? Kama kuna mtu analikuwa anafikiri hili saga la Richmond limekuwa swept under the carpet then is mistaken. Hii ni marathon na ina vigingi vingi vya kuruka tusiwa harakishe watu wafanye maamuzi ya pupa ili muradi kufurahisha nafsi zetu.

  Kweli ndio tulivyo yaani all over suddenly wale walikuwa wanaitwa mashujaa sasa washakkuwa villain. Watanzania tuwe makini katika masuala yanayo yanajiri. Wapo wanasiasa ambao ni one off show lakini sio Mwakyembe et al
   
 16. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kevo,

  Kama huwa unasoma kilichoandikwa utajua wazi mimi niko wapi kwenye hili na hivyo kuniuliza mimi niliwaungaje wakati jibu tayari limeandikwa huoni unauliza swali ambalo tayari una jibu lake? Rudia tena kusoma nilichoandika.

  Haitoshi kabisa kuandika JF na maoni kwenye magazeti. Inahitaji kwenda zaidi ya hapo.
   
Loading...