Mwakyembe na vijembe kwa mwanafunzi wake(Lissu)

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,053
4,596
Nimeiona hii video na kuiangalia mara kama tatu na nilichokigundua ni msimamo wa serikali ya Magufuli ya kupambana na Lissu na kutaka kumnyamazisha kuendelea kutumegea vipande vya sheria kwa kuwatumia wanasheria wakongwe na walimu wake kina Prof Mwakyembe na Prof Kabudi.

Kwa wiki kadhaa Mwanafunzi wao Lissu ameonekana katika vyombo mbalimbali hapa nchini akituhatarisha wananchi kuwa kuna mnyakyusa mmoja anaitwa MIGA huko majuu atakuja kutumaliza na kutufanya tulie na kusaga meno. Zaidi ya vijembe vingi kutoka kwa wale ndugu zetu wa Ndiyo Mzee kwa kumuita Lissu ni mamluki kulikua hakuna majibu rasmi kutoka serikalini. Ieleweke wazi kuwa mimi kama Mtanzania nimempenda sana Lissu kuwepo bungeni maana anatusaidia sana kuminya serikali ili ilete majibu ya kuridhisha maana kama si Lissu wengine tusingejua kama kuna huyu mnyakyusa anayeitwa MIGA.

Lakini pia pamoja na kumpenda na kumuunga sana mkono Lissu kwa jitihada zake na dhamira yake ya kuilinda nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi pia ningemshauri sana anapotaka kutuelewesha watanzania kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria asipende sana kutumia vitisho.

Kutumia vitisho tu pamoja na nia yake njema itaonekana kua ana kitu anakificha. Ilikua vizuri kututahadharisha na pia kutuambia kuwa pamoja na taadhari hiyo lakini bado tunaweza kutumia vipengele kadhaa kujaribu kushinda kesi hizo na hivyo kuweza kusamamia vizuri rasilimali zetu.

Lakini kwasababu anazozijua mwenyewe aliamua tu kuwa upende moja(ACACIA) na kututahadharisha kuwa hatutaweza kushinda hii vita. Binafsi kwakua ni Lay man katika masuala ya sheria niliamini hivyo, lakini pia kama mtu mwenye kumbukumbu nilijaribu kuangalia clip za huko nyuma na kumuona huyu huyu Lissu aliunga mkono mapendekezo ya tume za huko nyuma ambazo kwa kiasi Fulani zilifanana na mapendekezo ya hizi tume za rais.

Swali likawa nimuamini Lissu na masuala ya MIGA ama nimuamini Lisu kwa masuala ya report ya Boman na ESCROW? Nikabaki katika njia panda mpaka nilipoiona hii clip nikaamua labda nnilete mada hapa jamvini maana natambua sana japo kuna mannzi wa kijani na wale nyumbu wa ufipa lakini pia kuna watu waaminifu wa nchi yao ambao kwao vyama ni kama timu za mpira ila mapenzi yao yapo zaidi kwa nchi yao na hao ndiyo dhamira kuu ya hili jamvi la JF hao watu wanaitwa Ma Great Thinker.

Na hapo ndipo ninapokuja kwa walimu wake waandamizi waliomfundisha pale Mlimani. Katika video nitakayoiweka hapo chini kuanzia 10:0 Mwakyembe kachukua muda aliopewa wa kuchangia hotuba ya wizara ya fedha kwa kumpatia vijembe Lissu bila kutaja jina lake na kutuonjesha kidogo vipengele vya MIGA, na kwabahati mbaya muda ulikua mdogo hakuweza kumalizia maana kama tujuavyo wabunge wetu hutumia zaidi jazba na hivyo kupoteza muda mwingi katika vijembe zaidi ya kutueleza maana kamili ya mada.Mada: Je ni huu ni muda wa kupeana vijembe bungeni ama kueleweshana na kutuelewesha watanzania?

Maoni yenu
Mbase1970 ni mwanachi aliyekatishwa tamaa na mageuzi tangu mwaka 1992 na kubaki kuwa Mtanzania bila ushabiki wa vyama akiwa na mategemeo kuwa kizazi kipya kitakuja na mageuzi ya kweli na siyo wana CCM, NCCR, CHADEMA wala CUF maana hao wote ni kizazi cha nyoka hakiwezi kuwa binadamu ( maoni yangu binafsi)
 
Hivi wakati wa Kuchangia hotuba ya wizara ya Nishati na madini Mwakiyembe hakwepo Bungeni? Azungumzie makinikia na ishu za MIGA? Anakuja kuibuka leo kwny mjadala wa wizara ya fedha kuongelea miga, hii inaonesha mambo 2:
1: Inawezekana ana digest mambo taratibu kiasi kwamba after 2 weeks ndy amejua kwamba alitakiwa kuchallenge hoja za Huyo anaye muita msaliti, na imemchukua PhD holder wiki 2 kujua MIGA convention inasema mini? Slow learner!!
2: Huenda ni mtu asiyejua ni wakati gani wa kusema nini ili iwe na impact.lkn time management ni tatizo kwake. Umeambiwa una dakika 7 tu unaongea vijembe badala ya hoja , muda unaisha hujaongea point.
 
Kwa sasa Mwakyembe akimbizane na kina Steven Nyerere, Lissu hamuwezi tena.Miaka 18 iliyopita Lissu alisema hayo wakati akina Mwakyembe wakipiga Makofi kuashiria kwamba wanaunga mkono kwa 100% wawekezaji kuchuma raslimali zetu bure,tujiandae Miaka mwingine 18 kwa watu kama akina Mwakyembe kumuelewa Lissu.
 
Unafiki kitu kibaya sana katika nchi hii, Mwakyembe hayo unayoyaongea ungeyaongea kipindi kileeeeeeeee kutetea hii nchi wakati wenzio wanasign 4% ya mrahaba... Mwakyembe leo hii unakuwa shujaa wakati mikataba ya hovyo inasigniwa ulikuwepo humo kwenye mjengo..

Mwakyembe zaidi nayeye anapotosha umma, Tanzania ina migodi sita mikubwa na mmoja wa saba umefungwa baada ya kumaliza uzalishaji, katika hiyo migodi sita active ni miwili tu inayosafirisha makinikia. Je Mh Mwakyembe kwenye hiyo migodi minne ambayo haisafirisha makinikia Tanzania inapata nini? nalo mbona haliongelewi?. Tuache unafiki tuwaambie watanzania ukweli ili tatizo litatuliwe..

Leo tunalia kwa ACACIA kutuibia kwenye makinikia na tunasahau kuwaambia Watanzania ACACIA hao hao wanamiliki migodi 3 Tanzania na katika migodi miwili wanazalisha pure gold na makanikia, mgodi mmoja wa north mara hauzalishi makanikia zaidi ya pure gold.. kwenye hii pure Gold ambayo kimsingi ndio dhahabu yenye gharama na isiyo na longolongo watanzania tumesign 4% mrahaba. Nani amesign 4% mrahaba? mbona hili halizungumziwi kabisa??

Mbona 4% mrahaba hauzungumziwa na hawa watu wanaojiona wana akili leo hii, tumezuia makanikia lakini uzalishaji kwenye migodi unaendelea, Je Tanzania kama taifa linanufaikaje na huo uzalishaji wa dhahabu unaoendelea? mbona kwenye hili hatuongeai??..

ANGLO PALE GEITA, ACACIA (NORTH MARA, BULYANHULU, na BUZWAGI), SHANTA KULE CHUNYA, PETRA PALE MWADUI BADO WANAENDELEA NA UZALISHAJI, SERIKALI ITUAMBIE TAIFA LINANUFAIKA NA NINI, NA JE TUNACHOPEWA NI HAKI AU SIO HAKI..KWENYE ILE MICHE INAYOONDOKA NA NDEGE TANZANIA INAPATA NINI?..
 
Kwa sasa Mwakyembe akimbizane na kina Steven Nyerere, Lissu hamuwezi tena.Miaka 18 iliyopita Lissu alisema hayo wakati akina Mwakyembe wakipiga Makofi kuashiria kwamba wanaunga mkono kwa 100% wawekezaji kuchuma raslimali zetu bure,tujiandae Miaka mwingine 18 kwa watu kama akina Mwakyembe kumuelewa Lissu.
Mkuu upo sahihi lakini pia unatakiwa kumshauri Lissu pia maneno kama hayo. Tatizo kubwa hapa kwetu na ninavyoangalia comments nyingi naona watu wanachangia zaidi kwa emotions ama kumchukia mtu. Kila siku ukichangia kwa kujikita katika mada iliyoletwa unawezaukaonekana neutral hata kama umeegemea upande Fulani.
 
Upeo wa Mwakyembe unalitia aibu taifa.

Kwanza kuingiza hoja ya kuwaogopa wazungu ni yake binafsi hakuna aliyeibua. Hoja ni kutoheshimu mikataba na wawekezaji.

Pili, katumia muda mwingi kumkuza Nyerere na kusahau Nyerere ndiye aliyedidimiza uchumi mno na alipondoka 1985 tulikuwa mufilisi kabisa leo anamvika kilemba cha ukoka kuwa ati naye ni shujaa

Kwa mitazamo hii ya akina Mwakyembe na wenzie kutoka hapa tulipo ni kwa maombi tu!
 
Ccm kamwe haiwezi kusimamia ukweli nasiku iki simamia ukweli chama kitateketea.
Ata hivyo huwa nafikiria sana juu ya wa tanzania wanao waunga mkono ccm.
Jamani hii ikowazi kabisa haihitaji elimu ata ya phd.
 
Hivi wakati wa Kuchangia hotuba ya wizara ya Nishati na madini Mwakiyembe hakwepo Bungeni? Azungumzie makinikia na ishu za MIGA? Anakuja kuibuka leo kwny mjadala wa wizara ya fedha kuongelea miga, hii inaonesha mambo 2:
1: Inawezekana ana digest mambo taratibu kiasi kwamba after 2 weeks ndy amejua kwamba alitakiwa kuchallenge hoja za Huyo anaye muita msaliti, na imemchukua PhD holder wiki 2 kujua MIGA convention inasema mini? Slow learner!!
2: Huenda ni mtu asiyejua ni wakati gani wa kusema nini ili iwe na impact.lkn time management ni tatizo kwake. Umeambiwa una dakika 7 tu unaongea vijembe badala ya hoja , muda unaisha hujaongea point.
Huyu Mwakyembe ambaye hajamaliza tiba India azitoe wapi hoja za maana zaidi ya vijembe.

MIGA haijasema ukiuke mikataba bali uiheshimu.

Migogoro hupelekwa kwenye tume huru ya usuluhishi na siyo Mlalamikaji kujizolea mamlaka ya uchunguzi ambayo hana!
 
Haiwezekani ata kama umechizi vipi eti shamba Bilali umpe mtu alime apate junia mia afu mwenye shamba uchukue tatu. kama watanzania ata hii iko wazi hawaielewi basi tusubiri miujiza hamna namna.
 
Unafiki ni sehemu ya maisha ya watanzania hasa wana CCM..

siku unafiki ukiachwa na wana CCM ndio siku Taifa la Tanzania litakombolewa..

InshaAllah tuliombee taifa letu na watu wake waache unafiki na ubinafsi ili nasi tusonge mbele tuwe moja ya taifa lenye maguvu ya kiuchumi duniani...
 
Upeo wa Mwakyembe unalitia aibu taifa.

Kwanza kuingiza hoja ya kuwaogopa wazungu ni yake binafsi hakuna aliyeibua. Hoja ni kutoheshimu mikataba na wawekezaji.

Pili, katumia muda mwingi kumkuza Nyerere na kusahau Nyerere ndiye aliyedidimiza uchumi mno na alipondoka 1985 tulikuwa mufilisi kabisa leo anamvika kilemba cha ukoka kuwa ati naye ni shujaa

Kwa mitazamo hii ya akina Mwakyembe na wenzie kutoka hapa tulipo ni kwa maombi tu!
Tufanyeje? Maana mimi binafsi kama nilivyosema katika hitimisho sioni mtu yeyote wa upande wowote wa kutukomboa kutoka hapa tulipo na mapendekezo yangu ni kwamba tunahitaji uwanaharakati mpya wa kizazi cha millennium maana huwezi kufika kokote na kina Lowasa maana na wao kama kina Nyerere ndiyo waliotufikisha hapo tulipo. Nathubutu pia kusema hatuwezi kufika kwa kuwategemea kina Lissu, Mnyika, Bashe na Zitto hao wameshaonjeshwa utamu wa ufisadi na wakubwa zao ambao wengi ni zao la CCM. Sumaye hawezi kutufikisha Canaan maana na yeye ni walewale.

Baada ya kila kukicha kuwashambulia CCM na kuwatukuza CCM waliohamia upinzani bila kutafuta njia na mbinu mpya za kututoa hapa tulipo tukitegemea mtu kama Lowasa ama Seif ambao ni mazao ya CCM na bado wanakula keki ya Taifa kama viongozi wastaafu basi ni sawa na kujitekenya na kucheka wenyewe.

Lissu ana kila sifa anayopewa na wengi hapa lakini Lissu hana msimamo. Nilipenda sana angekua anaonyesha msimamo huo huo anaouonyesha anapowasema CCM na serikali yake angeuonyesha na upande alipo hasa pale walipobadilisha agenda yao kuacha kupigania maslahi ya watanzania badala yake kupigania maslahi yao binafsi na kuanza kuwachukua watu walioliharibu hili Taifa.

Unaposema kashfa zote tulizoziona huko nyuma na tunazoendelea kuziona hawa watu wawili ambao CDM wanatuaminisha kuwa ni malaika kwa asilimia zaidi ya 60 wanahusika. Na wao wanahusika zaidi maana walikua ni watendaji wakuu serikalini na wawakilishi wakuu wa serikali bungeni kwa nafasi walizokua nazo za u waziri mkuu. sielewi kwanini tunawaweka pembeni hawa watu kwasababu tu wamehamia upande tunaoushabikia. Kusema ukweli zaidi kutatutoa hapa tulipo hata kama utauma.

Magufuli alihusika na huu uchafu nitashangaa kama kuna mtu yeyote atakaye tetea kwa hili labda awe ana akili kama za nyumbu, lakini unapomshutum Magufuli kwa hili wewe kama mpinzani angalia na upande wako una mtu ambaye alikua ni boss wa Magufuli na huyu naye utamsemaje???? Magufuli aliuza Nyumba za serikali lakini baraza lile la mawaziri lilikua na Sumaye na ninyi mmempokea Sumaye utawezaje kumsema Magufuli wakati una Sumaye?

Tulikua na nafasi nzuri sana Taifa hili mwaka 2015 kuleta mabadiliko ya kweli kwa maendeleo ya watanzania na watanzania wengi waliwaamini kina Mbowe, Lissu, Lema na wengine wengi bila kumsahau Dr Slaa lakini imani yao ilikufa pale mwaka 2015 July walianza kuyakaribisha majoka kuu kuingia katika kambi ya watu angalau walikua wasafi kidogo. Kama dhana ya upinzani ilikua kuondoa ufisadi Tanzania wakubwa hawakuliona hili kuwa kwa kuwakaribisha watu mliowaita wezi ni kujiharibia nafasi yenu na imani kwa wananchi?

Ndiyo maana nasema wanasiasa wa kambi ya upinzani wakitaka kujirudishia sifa walioipata mwaka 2010 mpaka 2015 wajiangalie sana na makapi wanayoyapokea kutoka chujio la maji taka ya CCM. Huwezi kuvuna kitu kizuri kilichochujwa kutoka katika maji taka lazima kitakua na uchafu tu.

Napenda sana mabadiliko lakini siamini kama kuna mabadiliko kwasasa, hata huyu Rais wetu ajitahidi vipi sioni kabisa kama atafanikiwa. Ningependa sana afanikiwe lakini ukweli unaonyesha kua haiwezekani na itaendelea kuwa maigizo tu. Ukiwachukulia hatua kina Muhongo ukawaacha waliowatuma na kutukataza tusiwajadili sioni kama kiapo chako cha kila siku kujifanya unawapenda wanyonge kama ni cha kweli ama kurubuni watu wakupigie kura mwaka 2020. hataweza kutufikisha pale tunapopataka kwasababu anaongoza nchi kama ya chama kimoja kwa kutuhadaa kama vile wote ni walevi wa viroba. magufuli halipendi kabisa hili Taifa kwanini nasema hivyo, mtu anayelipenda Taifa lake kitu muhimu cha kwanza atashirikiana na wapinzani wake kuweka misingi bora ya kiutawala maana sharia nyingi zikipitishwa kama by partisan badala partisan zinakua na nafasi kubwa kwa jamii. Unapozuia mikutano ya siasa ya wapinzani wako watu wenye akili timamu tunajiuliza unaogopa nini kama kweli unapendwa na wananchi ama unafanya kitu wananchi wanachokipenda?

Asante tujikite katika kuchangia mada positively.
 
Nimeiona hii video na kuiangalia mara kama tatu na nilichokigundua ni msimamo wa serikali ya Magufuli ya kupambana na Lissu na kutaka kumnyamazisha kuendelea kutumegea vipande vya sheria kwa kuwatumia wanasheria wakongwe na walimu wake kina Prof Mwakyembe na Prof Kabudi.

Kwa wiki kadhaa Mwanafunzi wao Lissu ameonekana katika vyombo mbalimbali hapa nchini akituhatarisha wananchi kuwa kuna mnyakyusa mmoja anaitwa MIGA huko majuu atakuja kutumaliza na kutufanya tulie na kusaga meno. Zaidi ya vijembe vingi kutoka kwa wale ndugu zetu wa Ndiyo Mzee kwa kumuita Lissu ni mamluki kulikua hakuna majibu rasmi kutoka serikalini. Ieleweke wazi kuwa mimi kama Mtanzania nimempenda sana Lissu kuwepo bungeni maana anatusaidia sana kuminya serikali ili ilete majibu ya kuridhisha maana kama si Lissu wengine tusingejua kama kuna huyu mnyakyusa anayeitwa MIGA.

Lakini pia pamoja na kumpenda na kumuunga sana mkono Lissu kwa jitihada zake na dhamira yake ya kuilinda nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi pia ningemshauri sana anapotaka kutuelewesha watanzania kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria asipende sana kutumia vitisho.

Kutumia vitisho tu pamoja na nia yake njema itaonekana kua ana kitu anakificha. Ilikua vizuri kututahadharisha na pia kutuambia kuwa pamoja na taadhari hiyo lakini bado tunaweza kutumia vipengele kadhaa kujaribu kushinda kesi hizo na hivyo kuweza kusamamia vizuri rasilimali zetu.

Lakini kwasababu anazozijua mwenyewe aliamua tu kuwa upende moja(ACACIA) na kututahadharisha kuwa hatutaweza kushinda hii vita. Binafsi kwakua ni Lay man katika masuala ya sheria niliamini hivyo, lakini pia kama mtu mwenye kumbukumbu nilijaribu kuangalia clip za huko nyuma na kumuona huyu huyu Lissu aliunga mkono mapendekezo ya tume za huko nyuma ambazo kwa kiasi Fulani zilifanana na mapendekezo ya hizi tume za rais.

Swali likawa nimuamini Lissu na masuala ya MIGA ama nimuamini Lisu kwa masuala ya report ya Boman na ESCROW? Nikabaki katika njia panda mpaka nilipoiona hii clip nikaamua labda nnilete mada hapa jamvini maana natambua sana japo kuna mannzi wa kijani na wale nyumbu wa ufipa lakini pia kuna watu waaminifu wa nchi yao ambao kwao vyama ni kama timu za mpira ila mapenzi yao yapo zaidi kwa nchi yao na hao ndiyo dhamira kuu ya hili jamvi la JF hao watu wanaitwa Ma Great Thinker.

Na hapo ndipo ninapokuja kwa walimu wake waandamizi waliomfundisha pale Mlimani. Katika video nitakayoiweka hapo chini kuanzia 10:0 Mwakyembe kachukua muda aliopewa wa kuchangia hotuba ya wizara ya fedha kwa kumpatia vijembe Lissu bila kutaja jina lake na kutuonjesha kidogo vipengele vya MIGA, na kwabahati mbaya muda ulikua mdogo hakuweza kumalizia maana kama tujuavyo wabunge wetu hutumia zaidi jazba na hivyo kupoteza muda mwingi katika vijembe zaidi ya kutueleza maana kamili ya mada.Mada: Je ni huu ni muda wa kupeana vijembe bungeni ama kueleweshana na kutuelewesha watanzania?

Maoni yenu
Mbase1970 ni mwanachi aliyekatishwa tamaa na mageuzi tangu mwaka 1992 na kubaki kuwa Mtanzania bila ushabiki wa vyama akiwa na mategemeo kuwa kizazi kipya kitakuja na mageuzi ya kweli na siyo wana CCM, NCCR, CHADEMA wala CUF maana hao wote ni kizazi cha nyoka hakiwezi kuwa binadamu ( maoni yangu binafsi)

Inaonekana ni kwa kiasi gani ulivyo Nyumbu, Lisu ni kibaraka wa Wazungu, kwa vile wewe ni Lichadema huwezi kuona ubaya wa Lisu kwa jicho la pili. Lisu ni tapeli mwizi mjinga na kila mara amekuwa akizua mambo mengi yasiyokuwa na maana, mfano; Kwenye Bunge maalumu la Katiba ambapo UKAWA feki ulizaliwa, Tundu Lisu alizua jambo la aibu kuwa "Eti Tanzania haina Hati ya Muungano ktkt Umoja wa Mataifa UN" madai haya ya Ovyo ya Mh.Lisu yalithibitishwa kwa Hati kuletwa hadharani, Lakini pia ni Lisu huyo huyo alifikia hatua ya kumtukana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kuwa eti alizoea vya Kunyanga vya kuchinja haviwezi, Ni Tundu Lisu huyo huyo aliwahi kumtukana Lowasa kuwa ni Mwizi na Fisadi hatari, lakini ni Lisu huyo huyo ndiye leo anamsafisha Lowasa. Na anadiriki kusema mchana kweupe kuwa Lowasa siyo Fisadi !!! . Hivyo ni Mwendawazimu pekee anayeweza kumkubalia Lisu kuwa ayasemayo ni sahihi.
 
Back
Top Bottom