Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe amesisitiza kuwa itakapofika Desemba mwaka 2021 ndio mwisho wa waandishi wa habari wasiokua na elimu kuanzia ngazi ya stashahada kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya habari ya Mwaka 2016.
Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo jana Mkoani Singida alipokuwa anazungumza na wadau wa tasnia ya habari ambapo amewataka waandishi hao kutambua kuwa kuanzia mwaka 2022 wale ambao hawatakua na vigezo kulingana na Sheria ya Huduma za Habari hawatakua na nafasi wala sifa ya kuitwa Waandishi wa Habari.
“Uandishi wa habari ni taaluma kama taaluma nyingine na sio kimbilio la wale ambao wamefeli katika masomo au waliokosa kazi ya kufanya,hivyo naomba mtambue kuwa mwaka 2021 ndio mwisho wa waandishi wasiokua na elimu ya uandishi wa habari kuanzia ngazi ya stashahada”amesema Mwakyembe.
Aidha Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Ibara ya 18 d ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa kila mwananchi ana haki ya kupata taarifa sahihi hivyo ni jukumu la wanahabari kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa ambazo ni sahihi kutoka kwa watu sahihi na kuzifikisha kwa walengwa kwa usahihi.