Mwakyembe: Mbunge unakwenda kwenye mkutano nje umevaa suti na raba kwanini usidharaulike?

Hapa Mwakyembe anataka tuamini kuvaa suti na raba tu ndio kunakotufanya tudhaurike na mataifa mengine. Japo ana point kuhusu presentation lakini ni hoja dhaifu kusema mavazi tu......
 
Si bora wavae raba waongee vya maana? Kuliko mukulu aliesema we are manufacturing teachers huku kavaa suti ya kuhongwa na viatu vya complimentary! In the end ur brain is supposed to sell u. When u got brains, very few will care about looks and dressings!

Mkuu umenichekesha hasa hapo uliposema suti za 'kuhongwa' hii si imewahi kumkuta mkuu wa kaya iliibuliwa na week leak?
 
Nahisi hiyo ni imani yetu tu kuwa tunadharaulika kwa sababu ya kivazi - Watanzania kwa sasa tunadharaulika kama nchi. Katika watu ambao hawajali umevaa nini ni wazungu. Hata katika protokoli ikiwa umeamua kuepuka kwa sababu zako za kiitikadi au kiimani, hakulazimishi mtu, kwa mfano, kuna watu kwa itikadi zao za kisiasa hawataki kuvaa tai na hawavai.

Tatizo sio aina ya kivazi bali namna ya uvaaji. Hivi unaingia mahali rasmi, chini unaning'iniza suruali ya michezo juu umetundika koti la suti unataka uonekane vipi kama sio mshamba. Ikiwa unataka kufanya comedy, chagua mazingira na hakuna atakayekudharau, kinyume chake utashangiliwa.
 
:biggrin1: hapo mwakyembe kampiga mtu dongo....eti suti na raba hivi kweli kuna mtanzania alikua akiwa kwenye mikutano huko nje anavaa suti na raba? na sio hiyo tu pia wakiwa huko kwenye mikutano nina uhakika hata kiingereza walikua hawakijui kwa hiyo walikua wakiongea wenzao wanawacheka tu.. juzi wakati wa kuchagua wabunge wa bunge la afrika mashariki ndio nilipojua kua kweli watanzania hatujui kiingereza, nna uhakika hata wakenya na waganda wanatuchekaga sana wakiwa kwenye hilo bunge la EA

Katika ule uchaguzi wa wabunge wa EA, ni wateule wengi wa ccm [ akiwemo la Mutz @ Ny] na mmoja wa cuf ndio walionekana kutokujua kiingereza na kwa bahati mbaya kati yao ndio wabunge wetu hivi sasa kutokana na uwingi wa ccm bungeni!! Nchi yetu inaabika kwa sababu ya ccm kwani majirani zetu wanajua kuwa nchini kuna watu wengi mahili lakini hawapewi nafasi kutokana na mizengwe ya chama cha magamba!!
 
Kwani ina tatizo gani? Mbona Will Smith anapigaga sana hizo tu?

Mwakyembe ni limbukeni mno.Nje ya Nchi mikutano kadhaa wazungu mnao wafuata huwa wamevaa kawaida tu na pia wakija hapa mara nyingi wanavaa kawaida sasa ubaya uko wapi .Kuvaa suti kunasaidia nini

Nyie hapo juu......hamjamuelewa Dr Mwakyembe.....lol
 
Mwakyembe ni limbukeni mno.Nje ya Nchi mikutano kadhaa wazungu mnao wafuata huwa wamevaa kawaida tu na pia wakija hapa mara nyingi wanavaa kawaida sasa ubaya uko wapi .Kuvaa suti kunasaidia nini

Hot air! kwani kigezo chako wewe cha "Viwango" ni wazungu, you dont have your own standards za represent personality yako kama mtu; hivi unajua "the first impression is the last impression"?! au unabomoka tu mradi umkashifu mtu! Man learn to put your mind into gear before you go ballistic; civility is a virtue!!
 
'Upumbavu ni kipaji kama urefu na ufupi' J. K. Nyerere

Mwakyembe ni MFUPI....
 
waafrika bwana, wengine mavazi, wengine raba, wengine kiingereza .ha ha ha ha

Mbona George W Bush alikuwa anavaa kajizi kamepaukaa. Na pia sidhani kama Putin wa urusi anafahamu kuongea kiingereza. Mwakyembe naye nafikiri bado ana colonial mentality.

Kinachowafanya kudharaurika ni kuomba omba na kusema sisi ni masikini wakati kila kitu kimejaa bongo madini mpaka mnyama kakakuona. Wabunge wakitaka kutodharaulika watunge sheria za kulinda hadhi kwa taifa, sheria zikulinda umoja wa kitaifa, sheria za kulinda maliasili na malaghafi kwa taifa, sheria za kuwapendelea watanzania. Na wakati huo huo wasizisimamie sheria na kuziheshimu.

Vingenevyo hata ukipiga suti kali na kiatu chako kikali na kuongea lugha ya mkoloni kwa madaha yote bado utadharaulika tu, tena watakuonyesha kwenye tv zao ulivyopiga viwalo vyako na hapo hapo wanaonyesha watu wanavyoishi kwenye vinyumba vya msonge inzi wakiwatapakaa machoni na mdomoni na watu hao hao hawana chakula. Tena ni bora ukienda umevaa kimasai utaheshimika zaidi.
 
Sidhani kama wabunge walivyodai kudharauliwa nje ni kwa sababu moja tu ya uvaaji (wala si sababu mojawapo, wapo wanaovaa kawaida tu na heshima tele). kwanini sababu kubwa isiwe ufisadi uliofumbiwa macho TZ. leo hii Kagame akivaa suti na makobazi anaweza kabisa kupewa heshima yake vile vile.
Mwakyembe dharau zimemzidi. Toka apate full uwaziri naona confidence imekuwa over.
tutayasikia mengi.
 
ccm hawakomi kuongea kwa mafumbo,sasa si angemtaja kwa jina huyo aliyevaa suti na raba?lukuvi hakuomba mwongozo athibitishe kauli yake?mbona jk anavaaga koti na jeans kumuiga Bush?..hivi nchemba kafia wapi?
 
angalieni hiii tabia ya kuweka mbele mambo ya kuvaa suti ndo ilipelekea mwenzenu tena mkuu wa nchi akauza mahakama kuu kwa pair tano za suti. ohooooo
 
Leo Mwakyembe ametoa kali bungeni wakati akijibu hoja za wabunge kuwa waache kulalamika kuwa wanapokuwa nje ya nchi kama watanzania wanadharaulika na badala yake akawaambia kuwa kama mtu unaenda nje ya nchi kwenye mkutano huku umevaa suti na raba kwanini usidharaulike.

Sasa hapa sijui alikuwa anamlenga nani ila kauli hii iliibua zogo bungeni na ilibidi mwenyekiti wa bunge Jenister Mhagama afanye jitihada kumaliza kelele zilizoibuka baada ya kauli hiyo.

Mtu haeshimiwi kwa mavazi peke yake ila kilichomo kichwani mwake... Ukiwa pompompo utadharauliwa tu hata kama ungevaa suti za thamani kubwa kiasi gani.
 
Muacheni Mnyakyusa wa watu avae kadiri awezavyo.
Je ni nani kati yenu alizaliwa na nguo?
Nguo is nothing but utumwa mpya.
Thats why l hate suites na ties
 
Naona ndugu yangu hujamuelewa, hapa ni kuvaa suti na raba! si kuvaa kawaida
Ni kweli , tunahitaji dress code kwa viongozi wetu.
Hawamuoni JK anavyomwaga pamba za uhakika?
Na ikija kuvaa kanzu na kibarghashia bado anapendeza kwa sehemu yake na mahali pake.

Utakuta mtu kapiga suti, kibarghashia halafu makubadhi, hapo ni funga kazi kwa clash of dress codes!!!
 
Kunatakiwa semina elekezi Ngurdoto kwa viongozi wa ngazi fulani wakiwemo wabunge na mawaziri kuhusu dress codes, casual, official, dinner na table manners! bila kusahau crash programe kama ya wiki 4 hivi ili wapolish kiingereza chao; wagombea wa ubunge wa afrika mashariki walinitia kichefuchefu walipokuwa wakijieleza kabla ya uchaguzi!, teh teh teh.

naunga mkono hoja nakumbuka wakati nasoma chuo flan hukooo nje tulikuwa tunatembea kwenye makampun mbali mbali makubwa kabla ya kufanya hivyo siku mbili kwanza tulikuwa tunapewa semina elekezi ya kuvaa, jinsi ya kuongea, kuuliza maswali na vitu vingine kibao kwa mtu ambae sio muelewa unaweza ukahisi unapoteza muda ila ukweli dress code ni muhimu sana kutokana na sehemu husika. kuna vitu vidogo vidogo tu ambavyo vinaweza kukufanya udharaulike
 
Hivi huyu Will Smith ni mbunge wa jimbo gani? Au hakuna tofauti kati ya mavazi ya msanii na mbunge?
 
Back
Top Bottom