Mwakyembe: Mbunge unakwenda kwenye mkutano nje umevaa suti na raba kwanini usidharaulike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe: Mbunge unakwenda kwenye mkutano nje umevaa suti na raba kwanini usidharaulike?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Aug 2, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,707
  Trophy Points: 280
  Leo Mwakyembe ametoa kali bungeni wakati akijibu hoja za wabunge kuwa waache kulalamika kuwa wanapokuwa nje ya nchi kama watanzania wanadharaulika na badala yake akawaambia kuwa kama mtu unaenda nje ya nchi kwenye mkutano huku umevaa suti na raba kwanini usidharaulike.

  Sasa hapa sijui alikuwa anamlenga nani ila kauli hii iliibua zogo bungeni na ilibidi mwenyekiti wa bunge Jenister Mhagama afanye jitihada kumaliza kelele zilizoibuka baada ya kauli hiyo.
   
 2. M

  MTK JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280

  Kunatakiwa semina elekezi Ngurdoto kwa viongozi wa ngazi fulani wakiwemo wabunge na mawaziri kuhusu dress codes, casual, official, dinner na table manners! bila kusahau crash programe kama ya wiki 4 hivi ili wapolish kiingereza chao; wagombea wa ubunge wa afrika mashariki walinitia kichefuchefu walipokuwa wakijieleza kabla ya uchaguzi!, teh teh teh.
   
 3. A

  Awo JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Kwani ina tatizo gani? Mbona Will Smith anapigaga sana hizo tu?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwakyembe yuko sahihi kabisa kwenye hili. Na wabunge wetu wasione aibu hata kidogo ya kufanya semina ili wajifunze namna ya kuvaa, maana wengi wao wakiwa nje ya nchi wanaleta fedheha.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 4,999
  Trophy Points: 280
  Salary slip,

  ..tatizo la Mwakyembe ni lugha yake ya dharau.

  ..nimeshamsikia, siyo mara moja, akitoa kauli za kudharau elimu za wenzake.

  ..sasa naona ameongeza na ujivuni kwamba yeye anajua kuvaa kuliko wenzake.
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Heri uvae hivyo umwage nondo za maana,sasa wengi wao kaputi kabisa. Tanzania ya Nyerere alikufa nayo!
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Watu wanaojifanya vipanga aka wenye tabia ya ujivuni wanaboa sana tulikua nao sana CoET lakn wengi sasa wanaemea pua moja tu!
   
 8. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu msamiati huu ni mgeni kwangu, ebu nisaidie maana
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mwakyembe ni limbukeni mno.Nje ya Nchi mikutano kadhaa wazungu mnao wafuata huwa wamevaa kawaida tu na pia wakija hapa mara nyingi wanavaa kawaida sasa ubaya uko wapi .Kuvaa suti kunasaidia nini
   
 10. kai

  kai Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naona ndugu yangu hujamuelewa, hapa ni kuvaa suti na raba! si kuvaa kawaida

   
 11. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mimi nakerwa na wabunge wanaovaa suti za kaunda mikono mifupi na ndani wanaweka vibrauzi vya kike,
  Unaona mbunge amevaa ki t-shirt kina shingo ndefu imeacha kifua wazi. Hizo ni brauzi, zinatia kichefu chefu.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 4,999
  Trophy Points: 280
  Makene,

  ..U made my day!!

  ..mimi kaunda yangu huwa sivai t-shirt ndani.

  ..naachia kifua wazi ili watu waone nywele zangu zenye mvi!!

  ..just kidding!
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ikazaliwa ya ipi Mkuu? Kikwerete?
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Si bora wavae raba waongee vya maana? Kuliko mukulu aliesema we are manufacturing teachers huku kavaa suti ya kuhongwa na viatu vya complimentary! In the end ur brain is supposed to sell u. When u got brains, very few will care about looks and dressings!
   
 15. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa udaku niliopata toka kwa mtu wa karibu kabisa na bunge la URT, nasikia hilo dongo kapigwa Mh Kafulira
   
 16. m

  massai JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzazi umemaliza yote,kweli julius aliondoka na baraka zake
   
 17. D

  Deofm JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama ni mwanamke ulitaka avae ya kiume?
   
 18. 911

  911 Platinum Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Alishawahi kwenda kwenye press conference akiwa kavaa tshirt...kipindi kile cha conflict of interest kule kisasida!!!nakumbuka akina kiranga walimsema kwelikweli...nadhani somo lile lilimuingia hivyo nae kaona awanange wenzake!!!
   
 19. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mbona yeye alishafanya press conference akawa anajiita msomi, wakati alikuwa amevaa tisheti......
   
 20. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :biggrin1: hapo mwakyembe kampiga mtu dongo....eti suti na raba hivi kweli kuna mtanzania alikua akiwa kwenye mikutano huko nje anavaa suti na raba? na sio hiyo tu pia wakiwa huko kwenye mikutano nina uhakika hata kiingereza walikua hawakijui kwa hiyo walikua wakiongea wenzao wanawacheka tu.. juzi wakati wa kuchagua wabunge wa bunge la afrika mashariki ndio nilipojua kua kweli watanzania hatujui kiingereza, nna uhakika hata wakenya na waganda wanatuchekaga sana wakiwa kwenye hilo bunge la EA
   
Loading...