Mwakyembe, Magufuli, Muhongo walipuliwa bungeni - Kufanya siasa za Vyombo vya Habari

KISHOMBO

Senior Member
Jul 19, 2012
198
170
Ndugu wana JF

Sasa hivi naangalia bunge kupitia TBC1 kuna mbunge mwanamke sikumpata jina lake amesema mawaziri Mwakyembe, Magufuli na Muhongo wanafanya kazi na vyombo vya habari kwamba ni mabomu kuliko mawaziri wengine wanaotajwa kuwa mizigo. Inawezekana maneno ya huyu mama yakawa na ukweli. Tujadili
 
bona

JF-Expert Member
Nov 6, 2009
3,800
1,250
yaan hata huyo mbunge humjui ila unawajua aliowataja? ok kilichomfanya achanganye mada ni nini kuwataja hawa dhidi ya waliotajwa kua ni mizigo? alafu koma kabisa kumuweka muhongo kapu moja na kina mwakyembe na magufuli........unatia shaka na credibility yako!!!
 
Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
0

sababu hakuna wanchofanya zaidi ya kucheza na media, kila siku ni upembuzi yakinifu, reli ya kati bado dhoofu, ndege hiyo moja na ipo icu inavuja kama nyumba ya manyasi, hawaendi kwy kamati kuchukua mawazo ya wabunge. huyo muhongo ndio kabisa hana kitu alitutangazia umeme wa mgao basi wakati sasa ivi nchi ipo kwy mgao. muhongo ni muhongo tu.
 
nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,898
2,000
Katika ccm sijaona asiye mzigo....wote ni tatizo kea mustakabali wa taifa
 
bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,175
2,000
HASA MAGUFULI. Utasikia " na pesa za mradi huu tayari zipo."especially alipozungumzia flyovers za Dar es salaam mwaka jana bungeni, wakati akijua serikali imefilisika kama kipindi flani Zitto alipoweka issue hii hadharani. Hizi ni siasa za kizamani ( medieval politics) BOMU KWELIKWELI
 
East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,761
1,195
anaitwa maryam msabaha mbunge viti maalum (cdm) znz. yaani kapiga makavu live.

Ya ngoswe mwachie ngoswe.Hao mawaziri aliowachachafya hizo wizara sio wizara zinazohusu mambo ya muungano.Ni wizara za Tanzania bara tu.Angechangia ya mambo ya ndani,ulinzi,mambo ya nje ningemwelewa.Huyo mzanzibari asigusie hizo kabisa hazimhusu.Mwakyembe au Muhongo wawe wanaweza au hawawezi hayamhusu aachie wabunge wa bara waseme.Wabunge wa Zanzibar wakome kabisa kuongelee mambo ya wizara zisizokuwa za muungano.Wakome.

Wabunge wetu huwa hawaongelei za mawaziri wao wa wizara za Zanzibar.Akome.Treni ya mwakyembe iko bara na hawezi ijenga kisiwandui yeye si waziri wa uchukuzi wa Zanzibar.Pia mafuta ya zanzibar mlishasema bara hayatuhusu sababu hayako ndani ya Muungano sasa kwa nini huyu mzanzibari amparamie waziri wetu wa madini wakati madini si sehemu ya muungano?

Aliyemtuma akamwambie hivi wameniambia nikome.

Napendekeza wabunge wa Zanzibar wawe wanahudhuria vikao vya bunge vile tu vinavyohusu mambo ya wizara za muungano.Vingine out wanalipwa posho za vikao visivyowahusu bure tu.
 
made

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
814
500

Usipanic..........!kwanza elewa hili ni bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ana haki ya kuongelea jambo lolote linalohusu nchi hii pande zote pili hata ukimsikiliza vizuri mheshimiwa Msabaha hana hata chembe ya Uzanzibar yeye ni mtu wa bara hata kwa lafudhi tu ukimsikiliza na katiba inamruhusu kuwa mbunge toka sehemu yoyote ya Muungano.......na inawezekana alichoongea kina mantiki.......
 
MOSSAD II

JF-Expert Member
Apr 14, 2013
3,972
1,195
yaan hata huyo mbunge humjui ila unawajua aliowataja? ok kilichomfanya achanganye mada ni nini kuwataja hawa dhidi ya waliotajwa kua ni mizigo? alafu koma kabisa kumuweka muhongo kapu moja na kina mwakyembe na magufuli........unatia shaka na credibility yako!!!

what is so special kwa huyo professor wa makaratasi asiyejua mitaji ya kuwekeza inapatikana wapi?
 
East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,761
1,195
kwanza elewa hili ni bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ana haki ya kuongelea jambo lolote linalohusu nchi hii pande zote

Bunge ni la muungano lakini lina mambo mengine ya bara peke yake yeye ni wa muungano akiwakilisha Zanzibar kwa ajili ya mambo ya Zanzibar na yale ya muungano tu.Ninachotaka kusema ni kuwa pale yale ya bara pekee yanaongelewa wale wa Zanzibar wakae kimya au watoke nje.

Pia sioni uhalali wa wao kulipwa posho wakati mambo ya mawaziri wa wizara za bara tu wanapowakilisha au kujadili hoja zao kuna haja gani mbunge wa Zanzibar kuwemo ndani ya bunge? Anaongeza gharama bure za matumizi ya hela za walipa kodi.

Napendekeza mijadala ya bunge ianze na wizara za muungano zikiisha wabunge wa zanzibar wapande boat za Azam waende Zanzibar kwao waache wabunge wa Tanzania bara waendelee na wizara zao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom