Mwakyembe kuanika yanayomsibu ACHOSHWA NA MASWALI YA AFYA YAKE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe kuanika yanayomsibu ACHOSHWA NA MASWALI YA AFYA YAKE

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jan 27, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  HATIMAYE Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameamua kuzungumzia ugonjwa unaomsumbua kwa muda mrefu sasa.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Dk. Mwakyembe alisema wiki ijayo anatarajia kuzungumzia ugonjwa huo ambao baadhi ya watu wamekuwa wakiuhusisha na kulishwa sumu.

  Miongoni mwa watu wanaodai kuwa Dk. Mwakyembe kalishwa sumu ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye mara kwa mara amekuwa akiwatuhumu watu anaowaita mafisadi kushiriki katika uovu huo.

  Sitta amenukuliwa akisema pamoja na kutoa madai hayo jeshi la polisi halijayatilia uzito zaidi ya kumhoji yeye na Dk. Mwakyembe.

  Katika mazungumzo yake jana na gazeti hili, Dk. Mwakyembe ambaye alirejea nchini mwishoni mwaka jana akitokea India kwa matibabu, alisema kwa siku mbili hizi hawezi kuzungumzia hali yake na kilichomsibu.


  "Kwa sasa waulize madaktari kuhusu hali ya ugonjwa wangu, mimi nitafute wiki ijayo tuzungumze," alisema Mwakyembe bila kubainisha ni siku gani hasa.


  Juzi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipozungumza na waandishi wa habari alisema kuwa serikali haiko tayari kuzungumzia ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe, kwani ni kinyume cha maadili ya utabibu.


  Pinda alisema hata kama anafahamu ugonjwa unaomsumbua hawezi kuuzungumzia na badala yake mwenye wajibu wa kufanya hivyo ni Dk. Mwakyembe mwenyewe.


  Wakati Pinda akitoa kauli hiyo, serikali ilishawahi kutoa taarifa ya magonjwa yaliyowasumbua baadhi ya viongozi waliopata kutibiwa nje ya nchi, akiwamo Rais Jakaya Kikwete.


  Kwa muda mrefu Dk. Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao hadi sasa haujawekwa wazi jambo linalowafanya baadhi ya wananchi wapate wasiwasi kuhusu usalama wa viongozi wa serikali.


  Tanzania Daima lilidokezwa kuwa madaktari waliomtibu katika Hospitali ya Apollo nchini India waliandika ripoti inayohusu ugonjwa wake ambayo inasemekana imekabidhiwa serikalini.


  Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kuandikwa na gazeti hili kutoka kwa baadhi ya watu walio karibu na kiongozi huyo ni kuwa hali yake si nzuri na hatoweza kurejea katika shughuli zake za kawaida katika kipindi kifupi kijacho.


  Watu hao walidokeza kuwa Naibu Waziri huyo amenyonyoka nywele, kope na vinyweleo huku ngozi ikiwa imeharibika.

  Kabla ya Dk. Mwakyembe kuanza kuugua na hatimaye kupelekwa India alitoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya njama za baadhi ya watu kutaka kumuua.

  Baada ya madai hayo Dk. Mwakyembe aliitwa polisi kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo lakini mpaka sasa jeshi hilo halijaeleza hatua ilizozichukua dhidi ya watu waliotajwa kuhusika na njama hizo

  Tanzania daima
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  amekawia sana na hata akiongea hatakuwa na jipya zaidi ya kusema tu kuwa ni kaugonjwa ka kawaida
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe weka wazi kabla hawajakulisha sumu ya kuharibu kumbukumbu yako.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  the chapter has been closed to this man since last year in August.......
   
 5. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  you see.
   
 6. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Go in details my brother, how the chapter has been closed, just for the sake of curiosity
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  aaaaagrrrrrrrr....!i am out of curiosity,....uoga wake ndio ujinga wake,......sijui anaogopa nini....ngoja nisubiri week ijayo.
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mi hata nimeshasahau kama Dr atapona, au ndiyo basi. Kafanya kazi kuubwa weee sasa anashindwa kumalizia conclusion ambayo inareflect kazi yote. He has to standstill until his last moment, kama alikuwa anapigania maslahi ya watanzania basi let him do that until his last moment. By the way! kila mmoja tunapita tu hapa duniani, sioni haja ya yeye kuendelea kukalia hizo siri wakati maadui wake walimfanyia timing.
   
 9. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  siasa za bongo bwana.sanaa tupo!.haujui msema kweli ni upi? Na mwigizaji ni yupo.wenyewe wanasema ni political syndicate
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  subiri wiki ijayo ndio tutaelewa uongo na uzushi na ukweli,ila tu awe makini kwa kipindi hiki tunachosubiri aseme siri yake la sivyo wanaweza piga penati hata kabla hajasema siri yenyewe
   
 11. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kachelewa sana sijui alikuwa anasubiri nini?
   
 12. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama kuna kamlio ka bomu kulipuka hivi ....................................
   
 13. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nani kamwambia Wiki Ijayo atakuwa Hai

  Au anamkataba na Mungu...aache upumbavu wameshamlisha Sumu kwa ajili ya Ujinga wake wa kuficha mambo kwenye report yake.
   
 14. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Muda wote alikuwa wapi kusema?Ukweli wa taarifa yake una mashaka.
   
 15. A

  ADAMSON Senior Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namsubiri kwa hamu kubwa lakini asithubutu kuishia katikati ka ripot ya Rich Mond
   
Loading...