Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,316
- 33,125
19th November 2009
Wamwaga mamilioni kwa yatima
Pia wamo Selelii, Mpendazoe na Lembeli
Wengine ni Laiser, Nape na Porokwa
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojipambanua kupambana na vitendo vya ufisadi nchini, juzi waliibukia katika jimbo la aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kuchanga mamilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto yatima.
Wabunge hao machachari katika vita dhidi ya ufisadi walikichangia kituo hicho cha FPCT-Ereto kilichopo katika kijiji cha Monduli Juu, ambako ndiko alikozaliwa na kuzikwa Waziri Mkuu wa zamani, aliyefariki kwa ajali mkoani Morogoro mwaka 1984, Hayati Edward Moringe Sokoine.
Ingawa wabunge hao hawakuhudhuria wenyewe katika harambee hiyo, michango yao iliwakilishwa kupitia kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Daniel Porokwa, ambaye aliongoza harambee hiyo.
Wabunge waliotoa michango yao ni pamoja na mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka aliyechangia Sh. milioni 1, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (milioni 1), Mbunge wa Longido, Lekule Michael Laizer (milioni 1), Mbunge wa Nzenga, Lucas Selelii (milioni 1), Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (Sh. 500,000) na Mbunge wa Kahama, James Lembeli (Sh. 500,000).
Wabunge wengine waliochangia ni pamoja na Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (Sh. 500,000), Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya (Sh. 500,000) na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (Sh. 500,000).
Mbali na wabunge hao, wengine waliochangia ujenzi huo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye (Sh. 500,000) wakati Porokwa mwenyewe alichangia Sh. milioni 2.5 ikiwa mchango wake na marafiki zake, ambao hakuwataja.
Akizungumza katika harambee hiyo iliyofanikisha kukusanywa Sh. milioni 9.5, Porokwa alitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuwa na moyo wa huruma kwa ajili ya kuyasadia makundi ya watu wasio na uwezo katika jamii kama, wazee, wajane na watoto yatima.
Jukumu la kuwasadia watu wasio na uwezo katika jamii yetu ni la kila mtu hivyo tujitolee kadiri tunavyoweza kuwasadia watu hao hasa watoto yatima ambao wamepoteza wazazi wao kwa sababu mbalimbali, alisema na kuongeza kuwa: Kutoa ni moyo na wala si utajiri wa mali tunazomiliki.
Porokwa aliutaka uongozi wa kituo hicho kutumia vizuri fedha zilizochangwa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kutowavunja moyo wafadhili wanaojitolea kusadia kituo hicho, na pia msaada huo ulete manufaa kwa watoto yatima wanaotunzwa katika kituo hicho.
Awali, mlezi wa kituo hicho, Mchungaji Zablon ole Sima, alisema kwa sasa kituo chake kinahudumia jumla ya watoto 160, wenye umri wa kuanzia miaka miwili hadi 12 na mradi huo ulianzishwa mwaka 2006 lengo likiwa ni kuwasadia watoto waliofiwa na wazazi na walezi wao kutokana na sababu mbalimbali.
Mchungaji Sima alisema kituo chake pia kinawahudumia watoto hao kwa kuwapatia malazi na chakula, sare, madaftari na vitabu vya kiada.
Lengo letu ni kutumia fedha tulizopata hapa kuongeza idadi ya mabweni ya kulala watoto hawa kwani tuna uhaba mkubwa wa mabweni na mahitaji mengine muhimu hasa kwa wale watoto ambao wanasoma shule za msingi, alisema.
Mchungaji Sima aliongeza kuwa baada ya kukamilisha ujenzi wa mabweni ya kuwalaza watoto, wataongeza idadi ya watoto kadiri ya mahitaji yatakavyojitokeza na kuwaomba wafadhili wengine zaidi kujitokeza kukisaidia kituo hicho.
Selelii na Mwakyembe walikuwa katika Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa mkataba tete wa Kampuni ya Richmond LLC ya Marekani wa kufua umeme wa dharura wa megawati 100. Mkataba huo ulifungwa kati ya Tanesco na Richmond Juni 23, mwaka 2006, lakini haukutekelezwa matokeo yake ukachukuliwa na Dowans.
Kutokana na ripoti ya kamati hiyo, Lowassa aliwajibika kwa kujiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa hiyo na kufuatiwa na mawaziri walioiongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.
Wabunge wengine kama Kilango, Lembeli, Kimaro, Sendeka na Mpendazoe ni miongoni mwa kundi la wabunge ambalo limekuwa likiibana serikali kutekeleza maazimio 23 ya Bunge, hususani la kutaka watendaji waandamizi wa serikali waliohusika kuipa zabuni Richmond ya kuzalisha megawati 100 za umeme kuwajibishwa.
Kutokana na msimamo wa wabunge hao kushupalia Richmond na tuhuma nyingine za ufisadi, kimezuka kikundi cha watu wachache wakiwemo mawaziri, wabunge na baadhi ya makada wa CCM kuwakejeli kwa lengo la kuwasafisha watuhumiwa wa kashfa hizo.
Wakati wa hafla ya harambee hiyo, Lowassa hakuwepo, na haikujulikana mara moja kama alikuwa amealikwa au la.
CHANZO: NIPASHE
0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni