Mwakyembe: Kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi kwa kupiga magoti kwa Mungu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1469107461484.jpg


Kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi kwa kupiga magoti kwa Mungu na tuliifanya haki kwa kila mtu, tulichoamua hata uniambie kesho asubuhi nirudie tena hata kama haitabadilika itakuwa vilevile, na mimi nitafurahi sana.

Chini ya kanuni tunaruhusiwa kuifufua tena Richmond ili ichunguzwe upya na nina apa wanaweza wote wakahama wakaniacha peke yangu na uhakika mimi mwenyewe nilichonacho nitajenga hoja, sidhani kama kuna mtu hata mmoja atasalimika kwenda jela" alisema Dk. Harrison Mwakyembe.
 
Mimi naomba kama Mungu huyu huyu anayemsema mwakyembe ni Mungu tunaye mwabudu airudie watu wakasimame mahakamani tuone Yale aliyoficha aliyosema anailinda serikali yote ayo aliyoficha kwa nini alificha kama anamwamini Mungu huyu mpenda haki
 
Nani atamwamini Mwakyembe tena? Wakati ule anapukutika nywele na ngozi inatoa magamba kama ya kenge na huku akijua siku ni za kuhesabika akaandika waraka kuwa anawindwa kuuwawa na serikali inajua pia akamueleza rafiki yake Sitta kuwa kalishwa sumu.
Kutoka India na kuahidiwa cheo akamkana rafiki yake kuwa hajasema hivyo hata kule kanisani alipotoa ushuhuda napo akapaasi.
Ndio Mwakyembe huyo! Aliyekana hata andiko lake la Phd
 
Hivi kuna mtu mwenye akili zake timamu atamwamini Dr Mwakyembe aliyekana andiko la PhD yake mwenye mchana kweupe.Kwa hakika tangu Dr Mwakyembe alipokana andiko la PhD yake si imani naye tena.
 
Back
Top Bottom