Mwakyembe katibu mkuu wa wizara yako ndio atakuharibia kazi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe katibu mkuu wa wizara yako ndio atakuharibia kazi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwigo, Jun 6, 2012.

 1. m

  mwigo Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh wewe ni waziri ambaye umeteuliwa juzi tu, inawezekana haujui nini kinaendelea ndani ya wizara yako. Sisi kama watanzania ni muda mrefu sana tumeilalamikia serikali yetu kuwa tunahitaji ndege kwa ajili ya safari za anga.

  Ni juzi tu Katibu mkuu wako alitamka maneno kuwa ndege hiyo isiruke mpaka itemize mashart yote.hali ya kuwa ndege imetimiza masharti yanayotakiwa kuruka. Je katibu mkuu alikuwa na dhamira gani kuizuia ndege isiruke? Kama mdau wa usafiri wa anga ilitustua sana kuona katibu mkuu ambaye ndie mtendaji wizarani na mtegemewa na wananchi ndio anakuwa mtu wa kwanza kuikwamisha ndege ya watanzania isifanye kazi.

  Wiki mbili baadae baada ya ndege ile aina ya B 737 – 500 kuanza safari zake DAR- JRO- MWZ-DAR tukasikia ndege ile imepokea vitisho kuwa itafanyiwa hujuma. Ni wiki moja sasa tangu vitisho hivo vitolewe, na leo tunaona DIRECT MR. CHIZI ambaye ndio ameisimamia ndege ile mpaka kuileta hapa nchini amesimamishwa kazi.

  Kuna haja gani ya kumuondoa MR CHIZI katika nafasi ambaye tumeona matunda yake? Au ni kwa vile alikaidi amri ya katibu mkuu wake ya kutoiondoa ndege kwa visingizio kuwa haijatimiza mashart? Hali ya kuwa imetimiza? Au kosa lake ni kuisimamia hii ndege mpaka ikapatikana? Au ni kwa vile yeye katibu mkuu hakushirikishwa ipasavyo katika kuileta ndege hii?? Nina maswali mengi ya kujiuliza kuhusu huyu katibu mkuu na namna alivyo mfukuzisha kazi mr chizi.Kiukweli katibu mkuu anakitu kimejificha nyuma yake kuhusu hii ndege na ATCL kwa ujumla.

  Mh Mwakyembe hujuma kwa ndege zina fanyika katika mazingira tofauti, katika kile katibu mkuu alidai kuwa "tutaona itafika wapi" sasa ndio ameanza kwa kukushawisi wewe ili kumsafisha DIRECTOR CHIZI ambaye ameileta kisha na ndege hiyo kurudi kwao ili yeye KATIBU MKUU anufaike anavyonufaika katika makampuni mengine ya NDEGE ambayo yanamtumia kuisambaratisha ndege hii.

  Tuna wasi wasi na katibu mkuu huyu ambaye inaonekakana yupo nyuma ya kikundi Fulani ambacho kina mtumia ili kuiua ndege hii ambayo inatumika kufanya safari za ndani ya nchi.

  Sisi kwetu hii ni hujuma kubwa ambayo imefanywa na kiongozi wetu wa serikalini bila kuangalia maslahi ya taifa na badala yake anaangalia maslahi yake binafsi.

  Kama waziri wa wizara husika tunaomba ukae na wadau mbali mbali wa secta ya anga ikiwemo AIR TANZANIA ili upate maoni yao.Hatuja pendezwa na hatujafurahia maamuzi ya katibu mkuu huyo kukushawishi kumsimamisha kazi DIRECTOR CHIZI.


  Ahsaante sana
  Madau.
   
 2. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aiseeee! Tanzania si mahala pa kuaminika tena - hakuna msema ukweli!!
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inamaana mwakyembe kaambiwa tu na kuchukua maamuzi bila ya ushahidi,sidhani kama mwakyembe ni mtu wa sampuli hiyo.Halafu isitoshe hata kama alikuwa mtendaji mzuri lakini utaratibu wa kumpa madaraka kama haukufuatwa anastahili aondoke.
   
 4. t

  tara Senior Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwezi tu majugu yashaanza.....hapa kuna kitu.
   
 5. m

  mwigo Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inavosemakana alitoa kauli kuwa tutaona hiyo ATCL yenu itafika wapi, si mnajidai??? tutaona. wao wana hisa kwenye kampuni moja ya ndege ambayo ilichukua abiria waote wa ATCL ya mwanzoni kabla haijafa, sasa wanataka kuiua ili atcl ya sasa ishindwe kazi. hujiulizi kwanini waondolewe hadi wanasheria na mhasibu??? mhasibu aliidhinisha fedha zikatoka za kuikodi ndege ile na mwanasheria alihusika ktk kuhakikisha ile ndege inafanya kazi, sasa kwanini huyo KATIBU MKUU atoe kauli za namna hiyo?? hujiuli???
   
 6. B

  Bosili Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera juhudi za mwakyembe tumeziona bado DK Mwinyi na wizara yako ya Afya MSD wanangoja nini ofisini na sasa kila mtu kaamua kuchukua chake mapema DODOMA vifaa vya mamilioni vimechomolewa toka bohari na jamaa kwa kulindana utasikia wahusika wamehamishiwa mkoa mwingine angalia Mwinyi kaa na mwakyembe waulize wenzio ujasiri wameupata hadi wakachukua hatua Big Up Kyusa wembe ule ule hadi kieleweke
   
 7. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kama CHIZI ana tatizo lingine ni vizuri tuambiwe ukweli na Serikali.Vinginevyo mimi nina mawazo yafuatayo:
  Kwanza Chizi aliteuliwa kukaimu nafasi iliyoachwa wazi na hili la kukaimu halihitaji nafasi kujazwa kwa ushindani yaani uitishe tangazo la nafasi ya Kaimu Director General.Chizi hajajiteua na huyu Chambo Omari anaelewa kuwa Katibu Mkuu ndiye mshauri wa Waziri.Hivyo WAZIRI ALIYEKUWEPO na KATIBU MKUU wake wangewajibishwa baada ya uteuzi kusitishwa.
  Pili ni jambo baya kwa Waziri kufanya kazi kwa kutumia Magazeti. Yaani kila faili utakalosaini au kukataa kusaini kama kiongozi liwe NEWS kama vile umefanya muujiza usiokuwa wajibu wako ni utamaduni wa Serikali ya CCM wa kujaribu kujiosha ili wale wasiofiiiikiri wanaomeza kila hadithi washawishike.Katabia haka kana Mh Mwakyembe, Mh. Magufuli, Mh. Naibu Waziri(au Waziri Mdogo?) wa Elimu,na watu wengine wanaopenda umaarufu wa rejareja.
  Tatu naamini kuwa njia nzuri kwa kuwa Chizi alikuwa Kaimu, nafasi lie ingetangazwa na Chizi na Watanzania wengine wangeomba nnafasi hiyo na ATCL ingepata DG wa kudumu ama wa mkataba apewe terms of reference ikiwepo time frames za kufufua shirika,kuongeza safari za ndani na nje na hata kujitegemea na kujiendesha kibiashara.
  Nne kusitisha ajira ya Acting DG na kumweka ACTING mwingine pia bila kutumia njia za ushindani kama sheria na kanuni za utumishi wa umma zinavyosema ni kuanza safari kwa wrong footing kwa rafiki yetu MWAKYEMBE
   
 8. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hivyo kukaimu kuna mishiko kweli - si unaweza pisha na nafasi ikitangazwa ya full na sio kukaimu hakuna atakaekuzuia kuiomba na kuipigania - katika ile simple logic. malalamiko yote chimbuko lake ni nini.
   
 9. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Safi sana Kombe Sana.
  Tatizo lipo kati ya masalia ya Nundu na Katibu Mkuu Ndugu Chambo na Mwakyembe ameingia kichwa kichwa bila tathimini ya kina.Tatizo bado linaonekana katika kupata CEO wa ATCL ,hivi Eng Chizi alijiteua kukaimu nafasi hiyo ?,na kama aliteuliwa na Nundu ,Chambo kama Katibu Mkuu alifanya nini na Bodi ya ATCL pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu Utumishi.?.Uzembe na jeuri ya Chambo ndiyo kifo na udhaifu mashirika mengi yaliyo katika wizara ya uchukuzi,siyo reli,ATCL yenye unafuu japo ni mashirka muhimu katika ustawi wa uchumi wa nchi.Kipindi cha nyuma vyombo vya habri zilinadika tishio la Chambo kumweka ndani Chizi kama angeendelea na kazi ya kuleta na kurusha ndege iliyokodiwa ya ATCL.Kama kuna matatizo ya kiufindi mamlaka kama TCAA ndiyo ingetoa sababu za kina juu ya ubora na usalama wa ndege hiyo lakini mpaka sasa inaonyesha ndege hiyo ina ubora.Mwakyembe asipoangalia atajikuta anatumika kama mpira wa kiume kwa Chambo na kuvuruga shirika badala ya kujenga.
   
 10. m

  mwigo Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua kinachotufanya tumtilie mashaka huyu katibu mkuu ni kuwa kauli zake za kuikwamisha atcl ilionekana tangu mwanzo, na akaapa kuwa tutaiona, Kiukweli mr chizi ndio alioisimamia mpaka ikafika hapa, na yeye katibu mkuu aligoma mapema kwa hivo akaonekana kuwa haihitaji ndege hii itue na ikaruka kimagushi tu.Kama kuna kingine watuambie tu. lakini sio
   
 11. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huyo chambo yuko hapo toka lini maana anonekana hajui anachokifanya .anaongoza wizara ambayo imesimama huku taasis hata moja iliyoko chini yake yenye ufanisi wa kuamini labda TAA na TCAA. Huyu jamaa atakuwa mzigo
   
 12. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Duh, hata sijui niamini lipi sasa?
  Mungu ibariki Tanzania...
   
 13. T

  Turbulence Senior Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tukiunganisha dots, nina hili swali apa: Ivi kwa nini Precision wanapandisha nauli za ndege hovyo, as they wish, hakuna connection hapo?? Isije ikawa kuna watu serikalini wanahujumu ATCL ili precision iendelee kutawala. Sidhani kama kuna justification yoyote ya kupandisha nauli kwa zaidi ya asilimia 80 ndani ya miezi 6. dar-kilimanjaro return sasa ni sh 450,000; miezi sita iliyopita illikuwa 320,000. One year ago ilikuwa 270,000. Hii nchi ina wenyewe jamani??? Makampuni yanafanya yanavyotaka: tanesco, kampuni za sim, airlines, swissport, etc. Aghhhhhhhhh.
   
 14. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Nionavo mimi, ni kuwa kuna makusudi yalifanya ili ATC IFILIE MBALI, hili lilifanywa na kina Mramba na ndio maana naona leo wamewajibishwa, na tumeona jinsi Precision air ilivokuja juu mpaka basi, ilivoletwa ndege ile juzi juzi ikahujumiwa ndege ikaanguka, sasa hivi inaonekana ATCL inakuja juu watu wamerudhisha imani nayo sasa sijui nini kimetokea mara huyo Acting amesimamishwa kazi, kweli hatujui undani lakini pia TUTAPENDA TUONE ATC INAENDELEA KUPAA KAMA ILIVOANZA VINGINEVYO TUTAKUWA HATUNA IMANI NA WEWE MWAKYEMBE !
   
 15. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Hilo shirika ni la watu fulani ambao wapo hapo kutumia kila wanaloweza ili shirika lingine la ndege lisiguse, kama unakumbuka Diallo alikuja na Cummunity Airline likafa kifo kibaya hata halikuwahi kuoperate, hawa watu wanatumia kila wanaloweza hata ikiwezekana ATC isiweze kuishi, ile ndege iloangusha siku ile ile Presicion ikaongeza bei pale pale ! nadhani serikali iangalie hili kwa kina! tumechoka tumechoka kuhujumiwa nchi yetu na mashirika yetu na watu wachache wabinfsi, tunaomba Rais alianglie hili kwa kina kipana kabisa.
   
 16. m

  mwigo Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siku ya ya uzinduzi wa hiyo ndege KATIBU MKUU aliigomea isiondoke mpaka waziri mkuu alipoingilia kati ndipo ndege ile ikaruka na akasababisha delay kubwa. Je kwann yy katibu mkuu aiwekee vikwazo atcl?? lazima katibu mkuu anamatatizo. na lazima katibu mkuu achunguzwe ili kijulikane.
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe hiyo wizara wamekupakazia.!
   
 18. m

  mwigo Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa hawa wanahisa katika precission air ndio maana wanaitaka ife hii ndege, kama mnakumbuka waliwahi kumtumia MRAMBA aiponde hii ndege ya ATCL hatimaye watu waichukie kwa kauli za kejeli, ni kweli viongozi wetu serikalini ndio wenye hisa huko PW ndio maana wanaikwamisha.na hao PW wanapandisha nauli kwa kuona hakuna kampuni ya kushindana nao, sasa wakisikia NZENGO inarudi wanaifanyia fitna. LAKINI WABAYA NI VIONGOZI WA SERIKALI YETU KWANI WAO NDIO WANAHISA HUKO KTK MAKAMPUNI BINAFSI.
   
 19. m

  mwigo Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WEWE UMELONGA HASA YALIYO MOYONI MWANGU,maana hii ni hujuma kali sana,Tumepata ndege nzuri sana na pia ACTING WETU alikubalika kwa wafanyakazi wa atcl wote na hata wadau wengine, hatukusikia minongono bali tukasikia katibu mkuu anaikwamisha ndege hii.MWAKYEMBE FANYIA KAZI HAYA YOTE nenda kamuulize WAZIRI MKUU PIA atakueleza kuwa yeye ndio aliotoa amri iruke.LAKINI huyo KATIBU MKUU WAKO atakufukuzisha kazi kwani anamaslahi yake binafsi kwenye kampuni binafsi.
   
 20. m

  mamajack JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mwakyembe acha kufanyiwa maamuzi na wezi,huyo katibu mkuu wako atakuponza maana tunahisi wewe bado unachembe ya uzalendo lakini naamini kuwa huwezi ishi na mwizi ndani ya nyumba yako mkaelewana nae labda akushawishi uwe mwizi,au umshawishi asiwe mwizi.naamini unaweza fanya kazi kama wewe,bula kuhusisha chuku za watu ambao wakati wanachukizana hukuwepo,huui chanzo wala mwisho,fanya kazi dhamana ulopewa,
   
Loading...