Mwakyembe je wajua? Watu wanapanda ATCL kwa 50,000Tsh.DAR/MWZ,DAR/JRO

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
GreatThinkers,
Hii nayo ni habari ya kweli hutaki unaacha.
ukifika counter unaambiwa nafasi hakuna, waliokata kihalali ni watu kama 15,wakati watu hamsini au zaidi waliobaki wanapitia njia ya panya kwa kulipia 50,000 tu.

Napendekeza wanyongwe ili adabu na uzalendo uwepo. Hii ni dharau!!!!
 
Umetuhumu, kisha ukatoa na mapendekezo!

Mkuu pia kuna tetesi kuna watu wamekosa nafasi za kazi ndio wapika majungu sana ATCL , je umeshawahi kusikia hizi taarifa mkuu?
 
GreatThinkers,
Hii nayo ni habari ya kweli hutaki unaacha.
ukifika counter unaambiwa nafasi hakuna, waliokata kihalali ni watu kama 15,wakati watu hamsini au zaidi waliobaki wanapitia njia ya panya kwa kulipia 50,000 tu.

Napendekeza wanyongwe ili adabu na uzalendo uwepo. Hii ni dharau!!!!

Ina maana watu wengi wanaopanda ndege za ATCL hawalipi nauli? Nasikia TRC nayo ilikwenda kaburini kwa style hiyo hiyo
 
Nimeshasikia hiyo kitu. Mtu mzima anakata ticket ya mtoto wa miaka 2? Hihihiiii.............

Ila hiyo ipo zaidi Precision Air na mashirika mengine ya Kiswahili.

Waswahili kwa madeal huwawezi.
 
Ina maana watu wengi wanaopanda ndege za ATCL hawalipi nauli? Nasikia TRC nayo ilikwenda kaburini kwa style hiyo hiyo

ekzaktly,,,,,mi mwenyewe nimepanda sana kwa styl hiyo,,,,unaongea na mhudumu wa BEHEWA,CLEANER,AU TT(SIJUI KIREFU CHAKE)
 
GreatThinkers,
Hii nayo ni habari ya kweli hutaki unaacha.
ukifika counter unaambiwa nafasi hakuna, waliokata kihalali ni watu kama 15,wakati watu hamsini au zaidi waliobaki wanapitia njia ya panya kwa kulipia 50,000 tu.

Napendekeza wanyongwe ili adabu na uzalendo uwepo. Hii ni dharau!!!!
Uongo wa mchana huu!! Sasa utacheck in vipi? Unapoenda Nairobi lazima upitie kule International departures ambako passport inakuwa linked na ticket. Ticket za ndege ni online na zinadhibitiwa kwa ajili ya usalama wa ndege kwa maghaidi. Ingekuwa ni bus ningesema waliolipa 50elfu watapandia Mbezi but kwenye ndege labda kama itatua sehem kwa ajili ya kuwapakia. Ukileta justification za hii tuhuma zitawasaidia sana wana usalama kuboresha usalama wa ndege. Kumbuka wanaokagua ticket na vitambulisho sio Airline ni watu wa usalama ambao hawahusiani na shirika la ndege
 
uchafu huo wa ATCL umesisikika sana - watu wanasimamishwa kazi au wanastaafu hawalipi nauli wao pamoja na familia zao na nyumba za pembeni - utafanya biashara kweli hapo. Na hiyo ni safari za masafa marefu sio Tz au EAC
 
ekzaktly,,,,,mi mwenyewe nimepanda sana kwa styl hiyo,,,,unaongea na mhudumu wa BEHEWA,CLEANER,AU TT(SIJUI KIREFU CHAKE)

Halafu akija muwekezaji inakuwaje? Maana muwekezaji anachokuja kufanya ni kuongeza walinzi na kupunguza wakata ticket. that is it!!
 
GreatThinkers,
Hii nayo ni habari ya kweli hutaki unaacha.
ukifika counter unaambiwa nafasi hakuna, waliokata kihalali ni watu kama 15,wakati watu hamsini au zaidi waliobaki wanapitia njia ya panya kwa kulipia 50,000 tu.

Napendekeza wanyongwe ili adabu na uzalendo uwepo. Hii ni dharau!!!!

Wanaingiaje kwenye ndege bila boarding pass? Maana kuna sehemu mbili za kucheck boarding pass; kwenyegate, ambako boarding pass itachanwa na abiria aachiwe stub, na mlangoni kwenye ndege, ambako abiria anatakiwa aonyeshe stub ili waone kama yuko kwenye flight sawa.

Ina maana ATCL abiria wanapanda kwa free seating bila kupewa seat number?
 
Uongo wa mchana huu!! Sasa utacheck in vipi? Unapoenda Nairobi lazima upitie kule International departures ambako passport inakuwa linked na ticket. Ticket za ndege ni online na zinadhibitiwa kwa ajili ya usalama wa ndege kwa maghaidi. Ingekuwa ni bus ningesema waliolipa 50elfu watapandia Mbezi but kwenye ndege labda kama itatua sehem kwa ajili ya kuwapakia. Ukileta justification za hii tuhuma zitawasaidia sana wana usalama kuboresha usalama wa ndege. Kumbuka wanaokagua ticket na vitambulisho sio Airline ni watu wa usalama ambao hawahusiani na shirika la ndege

We na wewe.. Nway mradi umepost.. Sasa kama wanaokagua tikiti ni usalama wa taifa na kwamba hawana uhusiano au linjage yoyote na ATCL, sasa ulichomsahihisha mwenye thread ni nini?? Kama wanakagua TISS ina maana takwimu za tikiti wanazo wao na si ATCL.. Kwa maana nyingine hata kama kuna tikiti 20 za dili chini ya ATCL menejment kuihujumu serikali hakuna wa kuzisemea, hata kama TISS watakuwa wameona si jukumu lao, na inawezekana hawafanyi ”book-reconcilliation na ATCL, as u said no direct linkage in-between..

Kwa maneno mengne unakubali kwamba ufisadi wa kulipa nauli tofauti unafanyika sana pale ATCL.. Hakuna wa kumshika mwenzake. Hzo taratibu za usalama wa taifa hazihusiani na bei ya tikiti, labda useme mtu hapewi tikiti na usalama wa taifa wanataka kukagua validity ya mtu kupitia tikiti hapo ndo pana point.

Mbumbumbu intelligent.
 
Mh ! hebu tujuzeni zaidi hii picha inavyochezwa maana mpaka sasa sijaelewe na security zote za airport hili linafanyikaje? naona kama ni kimajungu zaidi hebu tujuzeni zaidi.
 
GreatThinkers,
Hii nayo ni habari ya kweli hutaki unaacha.
ukifika counter unaambiwa nafasi hakuna, waliokata kihalali ni watu kama 15,wakati watu hamsini au zaidi waliobaki wanapitia njia ya panya kwa kulipia 50,000 tu.

Napendekeza wanyongwe ili adabu na uzalendo uwepo. Hii ni dharau!!!!

Mkuu nakubaliana na wewe kwa 100%. Katika sehemu ambazo Mwakyembe anatakiwa kuwamulika wale watu wa counter pia. Yaani kama kuua shirika ni wale. Nilifika kutaka ticket ya kwenda mkoa mmoja wa magharibi. Nilikuta wadada wawili na mama mmoja amevaa hijab(huyu alikuwa kimya sana) na kujifanya yupo busy kwenye mtandao.

Nikaambiwa return ticket ni laki mbili na themanini. Nikaenda CRDB PPF Tower kuchukua hela ili nije kulipa maana walikuwa hawana facility za kulipia online. Nilipofika tu dada mmoja akaniambia samahani kaka nimepata msg nafasi hakuna kwa tarehe unayotaka, nikamwambia zipo za lini?, akanitajia tarehe ya mbele a week after nikamwambia Okay nikatie hiyo akaniambia ngojea ni confirm kwanza, mara akasema mtandao upo down. Akachukua simu na kuanza kuongea kwa coding language, 'H1 H1 upo, kuna mtu hapa wa tarehe...,' baada ya sekunde ishirini za kujifanya anasikiliza simu akaniambie tena samahani kumbe nayo imeishajaa. Akaniambia ila kuna watu huwa wana cancel hivyo niachie namba yako ntakupigia ikitokea, nikamwachia nilipokuwa njiani narudi home simu ikaita, nikapaki na kupokea akaniambia kuna mtu ame-cancel ile tarehe niliyoitaka mwanzo ila bei yake itaongeza alfu 50,000 kwenye bei ya kawaida nikamwambia nimeahirisha safari. Tokeo siku hiyo sikuwahi kuwaza su kufikiria kusafiri na ATC tena.

Matendo kama haya ya mpaka watu wa counter kutaka kutengeneza pesa ndiyo yameifikisha ATC hapo ilipo. Mimi ningekuwa Mwakyembe ningeagiza hata ukataji wa ticket uwe electronised na ofisi ya GM ndiyo iwe inashughulika na ticket moja kwa moja wale wa pale chini wote ni redundant. Kama una ndege moja haihitaji complex workforces kabisa, halafu wawe wanaajiri kulingana na demand ya wateja na ongezeko la huduma za ndege. Demand for local flight in Tanzania is very high but we don't have serious people who can it into profitable venture. Kila mtu akiingia anawaza kuchuma aondoke. Serikali inatakiwa kutafuta watu watatu makini sana na kuingia nao mkataba wa management for ten years, na kama watawafukuza wawalipe bilioni tano kila mmoja ila kwa masharti kuwa kwa muda wa miaka mitano ATCL iwe na ndege zisizopungua saba, na waruhusiwe kuajiri na kuachisha yeyote yule.

ATCL haitaweza kuwa profitable katika mazingira ya wafanyakazi wa sasa wote ninasema wote pale Makao makuu hawafai ni wezi wala rushwa wanahujumu shirika kwa ajili ya kupata cha juu.
 
Mkuu,nadhani hii ni zamani au?
Huyo anaye risk ni wa wapi? wakati kwenda MWZ na kurudi kwa ATCL na sasa Precision ni 190,000 au 130,000 kwenda tu, unaweza kuingia deal ya hivyo huku unachungulia jela?labda wasubiri zikipanda tena ndio wazee wazima wajiite watoto,so sad halafu hawa ndio wanamzomea Mh.Rais wakiwa mbele.Hii nchi inahitajika adhabu za papo kwa papo, umeshikwa kifo au unapotea.
 
We na wewe.. Nway mradi umepost.. Sasa kama wanaokagua tikiti ni usalama wa taifa na kwamba hawana uhusiano au linjage yoyote na ATCL, sasa ulichomsahihisha mwenye thread ni nini?? Kama wanakagua TISS ina maana takwimu za tikiti wanazo wao na si ATCL.. Kwa maana nyingine hata kama kuna tikiti 20 za dili chini ya ATCL menejment kuihujumu serikali hakuna wa kuzisemea, hata kama TISS watakuwa wameona si jukumu lao, na inawezekana hawafanyi ”book-reconcilliation na ATCL, as u said no direct linkage in-between..

Kwa maneno mengne unakubali kwamba ufisadi wa kulipa nauli tofauti unafanyika sana pale ATCL.. Hakuna wa kumshika mwenzake. Hzo taratibu za usalama wa taifa hazihusiani na bei ya tikiti, labda useme mtu hapewi tikiti na usalama wa taifa wanataka kukagua validity ya mtu kupitia tikiti hapo ndo pana point.

Mbumbumbu intelligent.
Hakuna TISS mbumbumbu, wanaokagua ticket pale airport ni watu wa SWISSPORT na kwa kuwa ticket za ndege zinapatikana online sio rahisi kuiba ticket. Kama unasafiri kwa dili ina maana hautakuwa na ticket, na pale kwenye foleni utakutana na abiria wa KQ, Emirates, SAA nk which means kama hauna ticket haupiti. Labda ipigwe dili kati ya abiria, mkagua ticket wa swissport, anayefanya check in wa ATC na flight attendant anayechek boaring passs. Mimi binafsi siamini kama kuna dili la watu wengi. Tunaopandaga ndege za dili huwa ni katika ndege za jeshi au za serikali kwa misafara ya viongozi. Kwa commercial flight haiwezekani kuforge ticket kwa kuwa mfumo ni mmoja tu wa kukata ticket
 
Si wapande mabasi. Tamaa ya ndege ya nini . Nchi ndivyo ilivyoishi kufoji kila kona sasa deni la taifa trilion 14 kwa sababu ya ukosefu wa uzalendo .kila mwaka ruzuku haziishi
nimeshasikia hiyo kitu. Mtu mzima anakata ticket ya mtoto wa miaka 2? Hihihiiii.............

Ila hiyo ipo zaidi precision air na mashirika mengine ya kiswahili.

Waswahili kwa madeal huwawezi.
 
ekzaktly,,,,,mi mwenyewe nimepanda sana kwa styl hiyo,,,,unaongea na mhudumu wa BEHEWA,CLEANER,AU TT(SIJUI KIREFU CHAKE)

Mimi nadhani mabadiliko ya aina au kitu chochote yanatakiwa kuanzia kwa mtu mmoja mmoja, sasa kiongozi wewe unasema umepanda kwa njia hiyo mara nyingi na unasikia ni ufahari lakini wakati huo huo unalaumu kuwa watendaji hawafanyi vizuri wakati wewe ndiye unayewashauwishi kufanya hivyo. Ni vizuri utkabadilika tupende vitu halali, tuache kununua magendo vitu vya wizi n.k, wenzetu wameendelea kwa kuweka maslahi ya nchi mbele, unanunua kitu lazima upewe risiti na ionyeshe bei halisi na kiasi cha kodi, bila hivyo mteja na kupeleka mbele ya sheria. Sisi tunafurahi kupata vya dezo halafu tunataka maendeleo, haiwezekani hata kidogo.

Ukikuta mtu anakupata ticket ya ndege kwa 50,000 huyo ni adui toa taarifa ili iwe fundisho siyo kufurahi unaua maendeleo ya shirika na nchi pia. So tubadilike please, mabadiliko hayaji kwa kulipiza baya kwa baya, bali kwa kufanya what is right and just.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom