Mwakyembe azungumzia Kauli ya Kabudi kuwa Azory Gwanda amefariki

"".. Siri imefichuka, siri imefichuka..x 3 Profesaa kaleta balaaa, Profesaa kaleta mikosiii eeeh...... "🎺🎼
 
July 11, 2019
Bonn, Germany

Waziri Harrison Mwakyembe mwenye dhamana ya kusimamia habari Tanzania katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani DW, ametofautiana na kauli ya waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi.

Harrison Mwakyembe amesema hawezi kusema kwa uhakika kilichomtokea mwandishi wa habari aliyetoweka ktk mazingira ya utatanishi na kuongeza aliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili walichukulie kwa uzito suala hilo.

Mh. Harrison Mwakyembe akaongeza kuwa suala hilo kwa vile aliwasiliana na kuliwakilisha kwa vyombo vya usalama, anasubiri ripoti kamili toka vyombo hivyo.

Wakati huohuo wanaharakati wameanza kuichagiza serikali ya Tanzania kutoa ripoti kamili kuhusu yaliyomkuta mwanahabari huyo aliyetoweka baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi, kuthibitisha kifo cha mwandishi wa habari huyo Bw. Azory Gwanda.

mauaji tu. hakuna mwenye jibu wakati anahusika moja kwa moja. Mchawi hata siku moja hakubali kama anaroga.
 
Kabudi kazungumza kwa uhalisia wa Jambo air Malaysia iliipotea na watu zaidi ya 270.
ripoti ya mwisho ya serikali ya Malaysia inaamini watu wote waliokuamo katika ndege iyo wamepoteza maisha.
the same to Mr azory, Paramaganba Kama waziri Ana uhakika na serikali inajua Azori hayupo ndani wala nje ya mipaka ya Tanzanania kwa lugha laisi lazima utasema kafariki.
Kafariki au kauawawa? Maana mke wa marehemu anasema alichukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni wanausalama.
 
Kabudi inaonekana yupo karibu na ukweli. Alipoonopa ni kusema amekufa, usahihi ungekuwa aliuawa na walioenda kumchukua na kujitambulisha kuwa walikuwa ni wanausalama.
 
Sasa ni wakati wa Kabundi kuwachia ngazi maana anafanya uchochezi
July 11, 2019
Bonn, Germany

Waziri Harrison Mwakyembe mwenye dhamana ya kusimamia habari Tanzania katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani DW, ametofautiana na kauli ya waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi.

Harrison Mwakyembe amesema hawezi kusema kwa uhakika kilichomtokea mwandishi wa habari aliyetoweka ktk mazingira ya utatanishi na kuongeza aliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili walichukulie kwa uzito suala hilo.

Mh. Harrison Mwakyembe akaongeza kuwa suala hilo kwa vile aliwasiliana na kuliwakilisha kwa vyombo vya usalama, anasubiri ripoti kamili toka vyombo hivyo.

Wakati huohuo wanaharakati wameanza kuichagiza serikali ya Tanzania kutoa ripoti kamili kuhusu yaliyomkuta mwanahabari huyo aliyetoweka baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi, kuthibitisha kifo cha mwandishi wa habari huyo Bw. Azory Gwanda.
 
!
!
Kabudi Anafahamu Kilichomtokea Azory. Na Ameshakisema.
Sasa Haya Mengine Ni Kumfurahisha Mkuu Tu Kila Mmoja Anakuja Na Maelezo Yake. Ni Huyu Huyu Mwakyembe Alinukuliwa Akisema Kama Mtu Kaondoka Mwenyewe Wamfanyaje
Nae Mwakyembe angehojiwa kwa kiingereza,si ajabu angeenda mule mule kama Kabudi.Kudanganya kwa lugha ya kigeni inaonekana ni vigumu sana,rejea mahojiano ya Mkapa kuhusu mauaji ya Wazanzibari
 
Back
Top Bottom